Makapuku Forum

Makapuku Forum

Jamaa yangu analia sana,anakuja mtu shambani anatoa pesa ambayo ni robo ya matumizi yako ya Kilimo, Ile kuvuna kuleta k,koo kilio kikawa kikubwa

Kwa sasa ukitaka kufanya business yoyote lazima ufanye utafiti wa kina

Naskia Tikiti imeliza watu sana miezi hii ya June na kuendelea
Najiskia kulia aisee .. Mi tikiti langu ndo linatoa maua
 
angalia hii kama unafumba macho hivi,sema unaona nini cha tofauti
14516539_1146484255389267_7501908237481177413_n.jpg
Namuona sweetiepie
 
Ujerumani zilitengana mara tu baada ya kumalizika kwa vita kuu ya pili ya dunia hapo mwaka 1945.

Chanzo kikuu ni Ujamaa na Ubepari.
Ujerumani Mashariki wakafata mrengo wa Kijamaa.
Ujerumani Magharibi wakafata Ubepari.

Na ukumbuke Dunia ulikuwa inapitia kipindi kigumu baada ya kumalizika kwa vita kuu ya dunia, kwani kuliibuka pande kuu mbili zenye nguvu hali iliyopelekea kuibuka kwa vita baridi kati ya Urusi ( Wajamaa ) na Marekani ( Mabepari ).

Uhasama wa Ujerumani Magharibi dhidi ya Ujerumani Mashariki ukachagizwa zaidi na Ujenzi wa ukuta maarufu wa Berlin. Ukuta uliozitenganisha nchi hizo.

Ukuta ambao ulisabibisha maelfu ya watu kupoteza maisha au kubaki na ulemavu wa kudumu pale tu walipojaribu kuvuka kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine.

Hali hiyo ilienda mpaka mwaka 1990 pale ambapo Ujamaa ulipodondoka huko Urusi, na kusababisha Ujerumani Mashariki ikose misaada toka kwa Wajamaa hivyo wakaona ni bora waungane na kurudi kama zamani na kuwa Ujerumani moja.

Lakini katika utengano huo, Ujerumani Magharibi ndio iliyopiga hatua kimaendeleo zaidi wakati wa utengano wao kuliko Ujerumani Mashariki.

Pia katika kipindi hiko cha 1945 - 1990 kulizuka Vita maarufu ya Vietnam, Kati ya Vietnam ya Kusini iliyofadhiliwa na Wamarekani dhidi ya Vietnam ya kaskazini iliyokuwa inaungwa mkono na Warusi.

Pia katika kipindi hiko cha 1945-90 ndipo kulipoundwa umoja wa Nchi zisizofungamana na upande wowote ( NAM ) lengo ni kutojitenga na upande wowote.

Hivyo basi, Utengano wa Ujerumani ulisababishwa na hali ya kutoelewana kati ya Ujamaa na Ubepari.
Bepari uko nondo sana linapokuja swala la historia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom