1983 - Ricardo Quaresma anazaliwa.
Ni winga wa zamani wa Barcelona, Inter milan, Chelsea na Porto.
Wakati anakuwa alichukuliwa kama mmoja wa wachezaji mahiri watakaokuja kuwika wakikuwa.
Lakini hakuwahi kukidhi matarajio ya wengi. Yumo kundi moja na Javier Saviola, Pablo Aimar na wengineo walioshindwa kung'aa ukubwani baada ya kung'aa udogoni.