Makapuku Forum

Makapuku Forum

NUKUU NO 4#

Serikali hii kwa kusudi lolote haiwezi kuuza uhuru wa jamhuri
Siasa yetu niya kutotegemea upande wowote katika haya magombano ya ulimwengu ambayo hayatuhusu.
Ikiwa taifa lolote linatumia Msaada wanaotupa kama msingi kwa kutuingilia katika mambo yetu tutakataa Msaada huo.

Maneno haya yalipata kutamkwa na Mwalimu Julius Nyerere, Mei, 1964
Julius Nyerere alizaliwa April 13, 1922 na kufariki Dunia Oct 14,1999
1473705744933.jpg

Mmoja kati ya viongozi bora duniani fahari ya Tanzania
...........
 
NUKUU NO 2#

Kwa kadri maisha yanavyokuwa ndivyo yanavyokupa nguvu zaidi ya kukabiliana nayo ili hatimaye kufikia kelele cha mafanikio
Maisha ni suala la mapambano, anayeshinda pambano ndio bingwa

Maneno haya yalisemwa na waziri mkuu wa zamani wa Cambodia, Lon Nol.
Lon Nol alizaliwa Nov 13,1913 na kufariki Dunia Nov 17,1985
1473706220387.jpg
1473706224952.jpg
1473706230101.jpg

Maneno kuntu
........
 
NUKUU NO 3#

Nawasifu wanajeshi wote wa Tanzania kwa uhodari, ushupavu na moyo wao thabiti wa kulinda taifa letu

Nawaomba waendelee kuwa na moyo huo pamoja na kusaidia wakazi wa vijiji vya ujamaa vilivyoko jirani na kambi zao katika mipango yao ya kuzalisha mali

Maneno haya yalisemwa na Edward Sokoine, akiwa waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa, Agosti, 1972

Edward Sokoine alizaliwa Agosti 1,1938 na kufariki Dunia April 12,1984 amewahi kuwa waziri mkuu wa Tanzania
1473706534362.jpg
1473706544519.jpg
1473706549813.jpg

Simba wa wamasai
Kiongozi shupavu
........
 
NUKUU NO 1#

Wananchi pamoja na serikali yao ya Muungano wanazikaribisha nchi jirani na nchi yoyote itakayokuwa tayari kujiunga na umoja huo ili kufikia hatua inayotakiwa.
Hatuwezi kwa mara moja kuunganisha Africa yote, ila kwanza ni juu yetu kuungana kidogo kidogo mpaka kufikia kitu kimoja.

Haya yalisemwa na Rais wa kwanza wa Zanzibar Abeid Amani karume, July 30,1964 katika mkutano wa hadhara mjini Unguja, Abeid Amani karume alizaliwa Agosti 4,1905 na kuuawa April 7,1972
1473707103390.jpg
1473707107570.jpg
1473707112538.jpg

Baba wa Taifa la Zanzibar
..........
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom