Makapuku Forum

NUKUU NO 1#

Sanaa ya Uongozi au sifa kuu ya kiongozi mzuri ni uwezo wa kusema "hapana" na si ndiyo'.
Ni rahisi kusema "ndiyo" kuliko kusema hapana.
Wakati mwingine ni vyema kukubali kushindwa ukawa umetenda sahihi kuliko kukazania kushinda ukawa umetenda hovyo.

Haya maneno yalisemwa na waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair.

Alizaliwa Mei 6,huko Edinburgh, Scotland. Alikuwa kiongozi wa Chama cha Labour kuanzia mwaka 1997 hadi Juni 2007.

Ndiye mwingereza wa kwanza kushika Uongozi wa Chama cha Labour akiwa na umri Mdogo
 
I real miss her
Age is ain't nothing but a number
R I P beautiful
 

Mzinguzi
........
 

Coolio - See you when you get there
 
NUKUU NO 2#

Kansa ya Uongozi ndani ya CCM isingekuwa ni jambo la kutisha sana kama tungekuwa tumeanza kuona Chama kizuri cha upinzani kinachoweza kuiongoza nchi yetu badala ya CCM.

Ubovu wa Uongozi ndani ya CCM ndio uliofanya nikapendekeza tuanzishe mfumo wa vyama vingi.
Nilitumaini kuwa tunaweza kupata Chama kingine kizuri ambacho kingeweza kuiongoza nchi yetu badala ya CCM au ambacho kingekilazimisha CCM kusafisha Uongozi wake kwa kuhofia kuwa bila kufanya hivyo kitashindwa katika uchaguzi ujao.
Lakini bado sijakiona Chama makini cha upinzani, wala dalili zozote za kuondoa kansa ya Uongozi ndani ya CCM.

Ni maneno ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, kama yalivyo katika kitabu chake kinachoitwa Uongozi wetu na hatima ya Tanzania alichokiandika mwaka 1994.

Mwalimu alifariki Oct 14,1999
 
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…