Makapuku Forum

NUKUU NO 1#


Sitagombea kiti cha urais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu wa October mwaka huu (1990)

Nimeamua kustaafu, sikulazimishwa,
Ni uamuzi wangu. Baada ya kulitumikia taifa katika nafasi mbali mbali nimekiomba Chama changu kumteua mwanachama mwingine.
Haya yalisemwa na aliyekuwa Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar (SMZ)Idris Abdul Wakil, mbele ya waandishi wa habari nyumbani kwake mjini dar es salaam Agosti 12,1990
Akiahidi kuwa tayari kukabidhi madaraka kwa Rais mpya atakayechaguliwa. Abdul Wakil alizaliwa mwaka 1925, Zanzibar
Na kufariki Dunia Mach 15,2000.

Alikuwa Rais wa Zanzibar kuanzia October 24,1985 hadi October 25,1990
 
NUKUU NO 2#

Africa inaendelea kusonga mbele katika maendeleo. Jambo la msingi ni sasa ni kuendeleza biashara Kati ya nchi moja na nchi nyingine.

Kitu chochote kinachoonesha uwezo wetu ni cha kufurahisha sana.
Lililobaki ni kuungana zaidi kwa barabara, simu na reli ili biashara Kati ya mataifa ya kiafrica iimarike.

Maneno haya yalisemwa na aliyekuwa makamu wa Rais wa Botswana, Dr. Quett Masire, alipozungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege dar es salaam July 10,1972.

Masire alizaliwa Julai 23,1925 Botswana. Amepata kuwa Rais wa Botswana
 

Sikujua km nilikuwa na Rais uchwara Zenji
...........
 
Huyu anastahili pongezi
Hakuwa na uchu wa madaraka kabisa
 
NUKUU NO 3#

Ziara yangu ya Tanzania imekuwa ni tukio la kunifurahisha

Lakini kwa vile Ziara yangu sasa inanichukua katika nchi nyingine, siwezi kusahau jambo jingine kuhusu Africa ambako mamilioni ya wanaume, wanawake na watoto hawana huduma nzuri za afya na Elimu.

Maneno haya yalisemwa na aliyekuwa kiongozi wa kanisa katoriki Duniani Papa John Paul wa pili. Alipokuwa akihitimisha Ziara yake ya siku tano nchini, ambapo alitoa mwito kwa mataifa mbali mbali Duniani kuungana na Africa kubolesha maisha ya watu hasa masikini

Alikuwa akizungumza katika uwanja wa kimataifa Kilimanjaro (KIA) mbele ya aliyekuwa waziri mkuu na makamu wa kwanza wa Rais, Joseph Warioba alikwenda kumuaga uwanjani hapo, September 5,1990.

Alizaliwa Mei 18,1920 na kufariki Dunia April 2,2005
 
Huyu kusema kweli ndio namsikia leo, sasa bila KF ningemjulia wapi??
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…