Makapuku Forum

Makapuku Forum

“Niwaambie katika maboresho tunayoyafanya, hakuna nguvu kazi au ajira itakayopotea, wote ambao wako kwenye mashirika aidha watamezwa kwingine au yatakuja mashirika mengine ambayo yana maana zaidi sasa hivi kuliko wakati yalipoanzishwa, na kwahiyo hakuna ajira itakayopotea, naomba msihofu.”- Rais Samia Suluhu
Screenshot_20230819_151404_Instagram.jpg
 
“Serikali iko kwenye mchakato wa kutunga sheria itakayobadilisha hadhi ya Ofisi ya Msajili wa Hazina kuwa Mamlaka ya Uwekezaji wa Umma. Na pia tunaangalia uwezekano wa kuanzishwa kwa Mfuko wa Uwekezaji wa Umma ili kuondoa utegemezi kutoka mfuko mkuu wa Serikali.” – Rais Samia Suluhu
Screenshot_20230819_151453_Instagram.jpg
 
“Taasisi na mashirika yetu mengi kwa miaka kadhaa yamekuwa mzigo na tegemezi kwa Serikali. Na ndio maana mara nyingi nimesema mashirika yanakula Serikalini lakini hayarudishi kitu Serikalini, kwa maana hiyo yanakuwa mashirika manyonyaji.” – Rais Samia Suluhu Hassan
Screenshot_20230819_151535_Instagram.jpg
 
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mstaafu, Profesa Mussa Assad amesema ni wakati sasa wajumbe wa bodi katika taasisi za umma wakapatikana kwa utaratibu wa usaili ili kupata viongozi watakaoongeza tija kwa taasisi.

Wakati huo huo, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amependekeza watendaji wa mashirika hayo wateuliwe na bodi ili iwe rahisi kubadilishwa pale ambapo bodi haitaridhishwa na utendaji wao.
Screenshot_20230819_151634_Instagram.jpg
 
Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi, amesema anahitaji kuona safu yake ya ushambuliaji inakuwa ‘moto’ katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Al Sabieh (Asas FC) kutoka Djibouti
.
“Tungependa kuanza vizuri mashindano haya ya CAF, ukipata ushindi katika mechi ya kwanza, kazi inakuwa nyepesi kuelekea mchezo unaofuata wa marudiano, siku hizi hakuna timu ndogo, soka limebadilika, tunahitaji ushindi katika kila mechi,”
.
“Tutaingia uwanjani kwa kuwashambulia sana wapinzani wetu ili kuhakikisha tunapata mabao ya mapema, tunataka ushindi mkubwa harau pia wapinzani wetu,”
Screenshot_20230819_151729_Instagram.jpg
 
Staa mpya wa Azam FC, Yanick Bangala hajaonekana uwanjani kwenye mechi za ushindani tangu alipotua kikosini, lakini unaambiwa ataanza kukiwasha mechi za kimataifa wakati kesho Wanalambalamba watakapokuwa wageni wa Bahir Dar Kanema ya Ethiopia.
.
Timu hizo zinavaana kwenye mechi ya kwanza ya raundi ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika na staa huyo aliyesajiliwa kutoka Yanga kabla ya kupata jeraha la nyama za paja katika mazoezi ya kwanza na timu, sasa amepona na ni kati ya wachezaji 23 waliopo Ethiopia.
.
Kocha mkuu wa Azam, Youssouf Dabo alithibitisha hilo na kusema huenda akaanza kumtumia kwenye mechi na Kanema. “Aliumia, ila kwa sasa amepona na tupo naye, hivyo kama nitaona anastahili kucheza mechi hii, basi nitampa nafasi kwani ni mchezaji mzuri na mzoefu kwenye michuano ya kimataifa,” alisema Dabo
Screenshot_20230819_151819_Instagram.jpg
 
Simba bado iko sokoni na sasa imepanga kumshusha kiungo mkabaji, Efoe Novon raia wa Togo huku wakipanga kumtoa kwa mkopo straika wao raia wa Zambia Moses Phiri.

Novon kwa sasa anaitumikia Klabu ya ASKO Kara ya kwao Togo, ambayo alijiungana nayo tangu Novemba Mosi, 2020, akitokea katika Klabu ya AS Togo Port.

Msimu huu Simba itakuwa na mashindano mengi ambayo watashiriki kuanzia ligi kuu, Kombe la Shirikisho la Azam, Ligi ya Mabingwa Afrika, Super League na Kombe la Mapinduzi hivyo inahaha kuhakikisha inajenga kikosi imara cha watu wa kazi kazi.

Muda wowote kuanzia sasa uongozi wa Simba unaweza kumalizana na mchezaji Phiri ili apishe usajili mpya wa kiungo mkabaji raia wa Togo, Novon ambaye anaonekana kuhitajika kwa ajili ya kukata umeme kwenye klabu hiyo.

Screenshot_20230819_151916_Instagram.jpg
 
Wakati wadau na mashabiki wa soka wakijiuliza hatima ya beki Mamadou Doumbia ndani ya Yanga kutokana na kutoonekana kikosini pia akiwa hajapewa ‘Thank You’.
.
Taarifa za kuaminika kuwa hawajamalizana. Yanga ilimsaini Doumbia katika dirisha dogo la msimu uliopita sambamba na kiungo Mudathir Yahya na mshambuliaji Kennedy Musonda ambao wanaendelea kukiwasha, lakini beki huyo raia wa Mali haonekani kikosini. Baada ya Yanga kufanya siri na baadhi ya viongozi kuulizwa na kushindwa kuweka wazi juu ya Doumbia aliyesaini mkataba wa miaka miwili, mmoja ya vigogo wa timu hiyo (jina tunalo), amefunguka kuwa bado hawajamalizana, lakini wapo kwenye hatua nzuri.
.
Chanzo hicho cha kuaminika kilisema hatua iliyopo ni kumtafutia timu ili kumuuza ingawa timu nyingi zimeoyesha kutotaka huduma yake ikishindikana watamtoa kwa mkopo na wako mbioni kukamilisha hilo.
.
Kilichotokea kwa Doumbia ni kama kilichotokea kwa Gael Bigirimana aliyesajiliwa na Yanga msimu uliopita, lakini akatemwa dirisha dogo na kushindwa kuafikiana kiasi cha hivi karibuni kurejea kikosini kimyakimya au ilivyo kwa Peter Banda wa Simba inayeelezwa amempisha kipa Ayoub Lakred, huku akiwa bado yupo kikosini akisikilizia hatima ya kutafutiwa timu iwe kwa mkopo au kuuzwa.
Screenshot_20230819_152008_Instagram.jpg
 
Kocha wa klabu ya Barcelona Xavi Hernandez amesema mshambuliaji kijana ndani ya klabu hiyo Ansu Fati hawezi kujiunga na mahasimu wao klabu ya Real Madrid.

Kocha Xavi amesisitiza kua mchezaji Ansu Fati bado ataendelea kua mchezaji muhimu ndani ya klabu hiyo, Hivo taarifa za yeye kujiunga na klabu ya Real Madrid sio za kweli na ni jambo ambalo haliwezekani.

Kocha huyo anasema Ansu Fati ni kama nembo au urithi wa klabu hiyo kwahiyo sio jambo jepesi kwa yeye kuondoka ndani ya klabu hiyo, Lakini pia hiyo ni kutokana na kijana huyo kuibuliwa kutoka kwenye akademi ya klabu hiyo.

Kuna taarifa mbalimbali ambazo zimekua zikimhusisha Ansu Fati kuondoka ndani ya klabu ya Barcelona, Hii ikiwa inatokana na mchezaji huyo kukosa nafasi ya kudumu ndani ya klabu hiyo tofauti na matarajio ya wengi yalivyokua.
Screenshot_20230819_152130_Instagram.jpg
 
Kuelekea mchezo wetu ujao dhidi ya Dodoma Jiji FC, tutawakosa wachezaji wawili [Henock Inonga na Aubin Kramo] ambao wanachangamoto kidogo za majeraha.

Inonga alipata changamoto kwenye mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Singida Fountain Gate FC ambapo alianguka dakika ya 89 na kuumia bega baada ya pale alishindwa kuendelea na mchezo kutokana na maumivu makali akatolewa nje.

Ameshamaliza awamu ya pili ya matibabu na leo tunatarajia ataanza mazoezi ya pamoja na wenzake [group training] na tutaangalia kama atakuwa tayari kuingia kwenye machaguo ya mwalimu. Hiyo yote itategemea na namna ambavyo ataweza kufanya mazoezi.

Dkt. Edwin Kagabo, daktari wa Simba.
Screenshot_20230819_152221_Instagram.jpg
 
Aubin Kramo hajaonekana kwenye mechi tatu na hiyo inatokana na changamoto aliyopata kwenye mazoezi ya mwisho wakati tukijiandaa na mchezo dhidi ya Singida Fountain Gate FC.

Kwa bahati mbaya goti lake ‘lili-twist’ vibaya na kupata changamoto ya ligament ambazo zinaweka stability kwenye goti, baada ya uchunguzi na vipimo ambavyo tumevifanya tumegundua jeraha lake sio kubwa sana.

Timu ya madaktari tukampa mapumziko na ku-focus na matibabu lengo kuu likiwa ni kuondoa hatari ambayo ingeweza kusababisha kuumia zaidi na kukaa muda mrefu nje.

Anaendelea vizuri na ameshamaliza matibabu awamu ya kwanza ya awamu na ya pili kwa hiyo leo tutakuwanae kwenye mazoezi tukiendelea kumfanyia ufatiliaji kuona hali yake ikoje.

Dkt. Edwin Kagabo, daktari wa Simba.
Screenshot_20230819_152318_Instagram.jpg
 
Wawakilishi wa mlinzi wa kati wa Man United Raphaël Varane wapo kwenye mazungumzo na Al Ittihad ambao wameonesha nia ya kumsajili Varane .

Kwa upande wa Mchezaji bado anahitaji kubaki Ulaya kwa msimu mmoja licha ya Benzema na Kante kumshawishi aachane na United .

NB : Neymar pia alisema anahitaji kubaki Ulaya kwa msimu mmoa lakini baada ya ahadi ya ndege sasa hivi yupo Saudia ,chochote kinaweza kutokea speaking of maokoto
Screenshot_20230819_152448_Instagram.jpg
 
Mshitakiwa katika kesi ya kumbaka, kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka mitatu (jina linahifadhiwa), amemlaumu shetani kwa vitendo vyake, baada ya kutiwa hatiani kwa makosa hayo, na Mahakama ya Mombasa.

Mtuhumiwa huyo Ramadhan Atenya, amemlaumu shetani kwa kitendo hicho akisema kuwa alipagawa na pepo mchafu na hivyo kujikuta akifanya kitendo hicho.

Hata hivyo, Hakimu Mkuu wa Mombasa, Martha Mutuku, alikataa madai na utetezi huo, na hivyo kuamua kuwa upande wa mashtaka umethibitisha kesi hiyo inayomkabili pasipokuwa na shaka yoyote.

“Madai ya shambulio la pepo mchafu, hayana uhusiano wowote na mtoto mdogo aliyedhulumiwa. Upande wa mashtaka umeonyesha kuwa mtuhumiwa kwa kweli ametenda makosa hayo,” amesema hakimu huyo.

Hakimu Martha amebainisha kuwa ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka umemtia hatiani mtuhumiwa na kwamba alitambuliwa kuwa ndiye alieyefanya makosa hayo.

Kiongozi wa Mashtaka, Alex Gituma, ameiomba mahakama impe mtuhumiwa huyo adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.

“Watoto wamedhulumiwa kutokana na vitendo vya watu kama mtuhumiwa. Naomba mahakama hii isimuonee huruma mtuhumiwa. Anapaswa kutumika kama funzo kwa wengine ili kulinda watoto dhidi ya unyanyasaji wa kimapenzi,” amesema Gituma.

Awali, mahakama iliambiwa kuwa mtoto huyo wa miaka mitatu, alikuwa akicheza nje ya nyumba yao wakati alipofanyia vitendo hivyo vya kikatili na mshtakiwa huyo. Upande wa mashtaka umedai kuwa mtuhumiwa alitenda makosa hayo Februari 5, mwaka jana.

Mahakama imeelekeza mtuhumiwa aendelee kushikiliwa rumande akisubiri siku ambayo mahakama itatoa hukumu juu ya kesi hiyo.

Screenshot_20230819_152556_Instagram.jpg
 
Mhubiri Ezekiel Odero wa Kenya, ametoa mpya katika mahubiri yake yalikuwa mubashara katika moja ya luninga za nchi hiyo, pale aliposema kuwa baadhi ya wanamuziki wa Bongo Flava, huenda wakabaki kuwa watu wa kuwapa wanawake ujauzito bila kuwaoa.

Mtandao wa gazeti la Taifa Leo, umebainisha kuwa mhubiri huyo, ameyasema hayo wakati akimwombea mwanaume ambaye alizungumzia jinsi alivyo na mazoea ya kuachana na wanawake wote anaokutana nao hasa baada ya kuwapachika mimba.

Wakati wa mahubiri yake, Mchungaji Ezekiel alitafakari changamoto zinazowakabili wale waliotelekezwa na waume au wake zao na kuachiwa majukumu ya kuwalea watoto.

Papo hapo akamrejelea msanii maarufu wa Bongo Flava bila kumtaja jina.
“Kuna wasanii maarufu wa Bongo ambao wana mazoea ya kuwapa ujauzito wanawake tofauti. Amezaa watoto kadhaa na wanawake tofauti,” mchungaji Ezekiel amesema

Mchungaji huyo alieleza kuwa safari ya maisha ya msanii huyo imemkuta akiwa amezaa watoto na wanawake tofauti na kisha kuwatelekeza.

“Alichukua mmoja kutoka Kenya na kumpachikika mimba kisha kumtupa. Roho ya kuoa hana. Hana roho ya ndoa,” akasema.

Screenshot_20230819_152652_Instagram.jpg
 
Padre Asterius Mutegeki (33) mzaliwa wa kisiwa cha Bumbire, wilaya ya Muleba mkoani Kagera, aliyefariki kwa ajali ya pikipiki Agosti 18,2023 anatarajiwa kuzikwa Juamatatu.

Akizungumza leo Agosti 19, 2023 na Mwananchi Digital, Askofu msimamizi wa kitume wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Methodius Kilaini amesema kuwa, maziko ya Padre Asterius yanatarajiwa kufanyika Agosti 21, 2023 katika makaburi ya Mapadre Rubya Wilaya ya Muleba.

Askofu Kilaini amesikitishwa kifo cha Padre huyo ambaye alipata daraja la upadri Julai, 2022, hadi anakumbwa na umauti, alikuwa anafanya kazi katika Parokia ya Ishozi wilaya ya Misennyi.

Amesema, Padre Asterius alikuwa mtoto wa kwanza katika familia yao, baba yake ni Wincheslaus Barongo, Diwani wa Kata ya Bumbile, Wilaya ya Muleba, na alikuwa Padre wa kwanza kutokea kisiwa hicho.
Screenshot_20230819_152746_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom