Makapuku Forum

Makapuku Forum

BAADA ya kutupia bao kwenye mchezo wa Kilele cha Wiki ya Mwananchi, mshambuliaji Kennedy Musonda ametoa msimamo akisema ana kazi ngumu ya kufanya kwa vile anatambua kila mmoja ameweka matumaini kwake baada ya Fiston Mayele kuondoka.
.
“Uongozi ndio una nafasi kubwa ya kuthibitisha kuondoka kwa Mayele, mi sifahamu ila kwa upande wangu nina mtihani mkubwa na juzi nilikuwa nafahamu natazamwa zaidi na hili limekaa kichwani na nitapambana kuwapa raha mashabiki wa Yanga,” alisema Musonda na kuongeza;
.
“Eneo la ushambuliaji ndio siri kubwa ya ushindi nimefurahi nimepata nafasi ya kufunga japo sio mabao mengi lakini hilo moja limenipa nguvu na imani kuwa inawezekana na nitatakiwa kuwa imara zaidi kwa-sasabu natazamwa na wengi.”

Screenshot_20230726_053413_Instagram.jpg
 
Farhan Kihamu Jr

MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA, WAINATAKA PEPO HAWATAKI KUFA.

Atatokea Shabiki ghafla tu atahoji ile MOSPORTS kwenye jezi ya Simba imetoka wapi mbona hatujui imekuwaje, ile MO Foundation vipi mbona Tajiri anajaza tu matangazo yake.

Shabiki mwingine atahoji tu ile HAIER kwenye jezi ya Yanga mgongoni imekuwaje, ile GSM FOAM pesa ipo wapi, hitimisho utasikia Tajiri anatupiga sana.

Ni Shabiki huyo huyo atataka Simba imrejeshe Miquissone, atahitaji Yanga ipambane Mayele abaki, itataka Feisal alipwe mafao makubwa anayotaka ama Simba ifike fainali CAF, ni Shabiki huyo huyo bila yeye kutaka kuwa sehemu ya mchakato.

Shabiki huyo huyo atadai elfu 10 ni kubwa sana, lakini atazitaka timu zifike level ya Al Ahly, Mamelodi, Zamalek! Hajali Mashabiki na Wanachama wa Zamalek wanachangia vipi mchakato wa timu zao, hajali kuwa mtoto mdogo Al Ahly analipa karibia 104K ya Uanachama, ambapo hukh kwetu ni kadi za watu wanne.

Hajali kuna Mwachama wa Al Ahly analipa kadi Million 100, ana tiketi ya msimu, jezi zote za klabu na vifaa vyake! Hilo yeye hajali, anataka matunda bila kuwa sehemu ya mchakato, wanataka furaha bila kuwa sehemu ya maumivu,
Mwekezaji hawezi kuumia kirahisi anapohitaji na yeye ajipooze utasikia kelele.

Utasikia uchumi wa nchi zao na wetu sio sawa, haufanani! Basi hili ndio jibu la swali kuwa hatufanikiwi mbele yao kwakuwa wana nguvu kiuchumi, basi tukitolewa huko tusipigizane kelele wala tusiwasumbue Viongozi wa hizi timu kwakuwa tumekubali hatuwawezi na sisi ni Feeder, kila kinachotokea ni fluke! Si ndio maana yake?

Nje na hapo Viingilio vipande, kadi za Wanachama na Mashabiki zigombaniwe kama njugu ili upande huu wa wengi (majority) uongeze kwenye mifuko ya MO na GSM, kama hatutaki wapeni uhuru Matajiri, waweke pesa na waweke chochote wanachotaka ili timu ziendelee kusogea kwakuwa tunaukataa maumivu ya mchakato, tunaitaka pepo ila tunaogopa kufa.

Katazame Real Madrid, Al Ahly, Bayern Munich, Dortmund, Zamalek na timu zingine ambavyo Mashabiki na Wanachama wanazipa faida timu zao, ndio Maboss na wana nguvu sana.

Screenshot_20230726_053852_Instagram.jpg
 
Farhan Kihamu

Imani iliyotumika kumchukua Crispin Mhagama Ngushi kutoka Mbeya Kwanza kwenda timu kubwa Yanga, imani iiyotumika kuendelea kuamini uwezo wake licha ya kutotumika mbele ya Fiston Mayele na Kennedy Musonda, imani ya kutohemkwa na kutaka kumtoa nje ya kikosi, imani ya kumvulia na kuendelea kufanya mazoezi kwa bidii huenda msimu huu ikalipa, huenda.

Kuna sauti hazipazwi ipasavyo kuhusu Young Africans na imani yao kwa Wazawa, kuna namna sauti haiendi juu kuhusu Wananchi na Wachezaji wa kitanzania, wanajitahidi sana kupata walio bora na wachache sana hufeli kwa kipindi cha miaka miwili.

Kijana aichukulie hii kama second chance, the world is there for him to conquer

Screenshot_20230726_054122_Instagram.jpg
 
Farhan Kihamu

Ni miaka ya 1990 wakati huo Mwalimu ameshang’atuka madarakani na Jamhuri ipo chini ya Ali Hassan Mwinyi, ni zama za mwisho pia wakati Mwinyi anaelekea kukabidhi kijiti kwa Benny wa Kusini, miaka ya 90 wakati wa mfumo wa vyama vingi.

Ni safari ya kihisia kutoka uwanja wa Mission Mashimoni, Kilombero mpaka nchi ya visiwa saba vikubwa kwenye bahari ya Atlantic, nchi ya Ureno the Famous Land of the Merchants, ilikuwa jioni pale Lisbon.

Jioni ambazo Cristiano Ronaldo na Wachezaji wenzake wa timu za Vijana wawili walikuwa na maisha magumu sana, CR7 kutoka familia ya mlo mmoja wakitoka mazoezini wanakimbilia mgahawa wa MCDonalds kwa nyuma kuna Mhudumu ambaye huwapa msaada wa burger za masalia.

Nani aliyejua? Kama ambavyo JPM wa Chato alikuwa Rais, kama ambavyo Mama Samia Bint Makunduchi kutoka kuongoza Bunge la Katiba mpaka kusaini miswaada kuwa sheria na kuilinda Katiba, hakuwepo Sitti Bint Said ila Malaika wako walikuwepo.

Ikawa mazoea ya Mhudumu yule kuwapa msaada wa chakula Ronaldo na wenzake na hakujua anamsaidia nani! Hakujua anaisaidia dunia, anampa chakula Mwanasoka bora ajaye duniani, viatu vya Luis Figo na kitambaa cha Eusebio yeye ndie Mrithi.

Tupate tangazo kutoka @crdbbankplc kwanza, wafollow kwa michongo zaidi na zaidi @crdbbankplc @crdbbankplc kisha tuendelee Asante studio!

Ni miaka zaidi ya 25 imepita, Cristiano Ronaldo mwenye kila kitu, Mtoto mzuri Georgina na maisha mazuri! Anaketi mbele ya Gwiji Piers Morgan na kusema anamtafuta Binti yule aliyemsaidia chakula kipindi kile.

Ronaldo alisema kama yupo popote pale duniani basi anamkumbuka na ajitahidi amtafute, atakuwepo kwake Lisbon ama hata Turin, anataka kulipa fadhila ile kubwa aliyompatia kipindi hana kitu, anasema anakumbuka kila jema la Mtu.

Taarifa ile ilisafiri sana na ilifika kwa Binti yule Caldina Caldalas, ambapo alikutana na Wasaidizi wa CR7 akapandishwa ndege binafsi ya Gwiji mpaka Turin, akalala nyumbani kwake na sasa anamiliki mgahawa mkubwa zaidi Ureno, utajiri wa kutisha na maisha mazuri! Ronaldo alilipa wema ule aliotendewa.

The Man, The Myth, The Legend! I rest my case!
Screenshot_20230726_054227_Instagram.jpg
 
Farhan Kihamu

Una Zawadi Mauya, una Mudathir Yahya, una Salum Abubakar Sureboy, una Khalid Aucho, na bado una Jonas Mkude eneo la Kiungo, maisha yanataka nini tena?

Una Metacha Mnata, una Abou Msheri, una Djigui Diarra eneo la Goalkeeping! Well una Gift Fred, Dickson Job, Bakari Nondo na Ibrahim Bacca eneo la Beki wa kati, sijasema kuhusu pembeni kuna Kibabage, Muivory Coast, Joyce Lomalisa na Kibwana Shomari, wala sijataka kusogea mbele walipo wakina Nzegeli.
Screenshot_20230726_054340_Instagram.jpg
 
Mapema leo imetoka taarifa ya Wakala wa Sadio Mane kwenda Japan kwa ajili ya kufanya mazungunzo na uongozi wa Al Nassr
juu ya maslahi binafsi baada ya Mane kuruhusu

Mane alikubali kubakia Bayern Munich kwa hali yoyote ile lakini Bayern wanataka kumuuza
Screenshot_20230726_054516_Instagram.jpg
 
Marekani imemuwekea vikwazo Waziri wa Ulinzi wa Mali, Sadio Camara na Maafisa wengine wawili iliowatuhumu kwa kulisadia kundi la mamluki la Urusi la Wagner ambalo imesema linafanya kazi kama Jeshi la Wakala wa Urusi.

Marekani imemuwekea vikwazo Waziri huyo, Mkuuwa jeshi la anga Alou Boi Diarra, na Naibu wake Adama Bagayoko ikidai wamesaidia kuongezeka shughuli za kundi la Wagner nchini Mali.

Brian E. Nelson, Katibu wa Wizara ya fedha anayehusika na masuala ya ugaidi na ujasusi wa kifedha kwenye Serikali ya Marekani amesema Maafisa hao wamewaweka Watu wa Nchi hiyo katika hatari ya kundi la Wagner na unyanyasaji wa haki za binaadamu huku wakitoa njia ya ufujaji wa rasilimali za nchi yao kwa manufaa ya shughuli za kundi hilo nchini Ukraine.
Screenshot_20230726_054637_Instagram.jpg
 
Serikali ya Taifa la Afghanistan inayoongozwa na Taliban leo inatarajiwa kuyafunga Maduka ya urembo na saluni za kike zaidi ya elfu moja nchini humo ikidai pesa nyingi zinazotumika kwenye urembo zinasababishia hali ngumu kwa Familia masikini na pia baadhi ya huduma katika saluni hizo haziendani na maadili ya dini ya kiislamu.

DW Kiswahili inaripoti kuwa Wizara ya Kuamrisha Mema na Kuzuia Maovu nchini humo mwezi June mwaka huu ilitoa muda wa mwisho wa hadi leo kwa saluni zote kufungwa na kusisitiza kuwa muda huo ungewatosha Wafanyabiashara hao kumaliza kuuza au kutumia bidhaa zilizobakia.

Wizara hiyo imesema imetoa agizo hilo pia kwasababu vipodozi vingi vinawazuia Wanawake kutawadha vizuri kabla ya kuswali huku pia urembo mwingine kama kuongeza kope na kusuka nywele ukipigwa marufuku, Shirika la Habari la AFP limesema limeiona nakala yenye maagizo hayo ya mdomo ambayo yanatoka kwa Kiongozi Mkuu Hibatullah Akhundzada.
Screenshot_20230726_054726_Instagram.jpg
 
Mpiga Kinubi maarufu Mwanadada Siobhan Brady leo July 25, 2023 ameweka rekodi ya Dunia ya Guinness juu ya Mlima Kilimanjaro futi 19,000 kwa kupiga kinubi (kifaa kinachoheshimika nchini Ireland) kwa muda wa dakika 34 akiwa kileleni na kuvunja rekodi ya kupiga kinubi kwa muda wa dakika 18.

Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa @gersonmsigwa ametoa taarifa hiyo leo ambapo amesema awali Siobhan alipiga kinubi akiwa futi 16,000 katika Mlima Himalaya nchini India mwaka 2018.

Rekodi hii inaitwa “Guinness World Record for the Highest Harpist Concert” na imerekodiwa na kituo runinga cha Kimataifa kiitwacho National Geographic na sasa Kamati ya Dunia ya Guinness inasubiriwa kuthibitisha rekodi hiyo.
Screenshot_20230726_054835_Instagram.jpg
 
Droo ya kupanga mechi za awali za michuano ya Club Bingwa Afrika imefanyika leo na Tanzania ina wakilishwa na Simba na Yanga katika michuano hiyo.

Yanga SC anaanzia round ya awali atacheza dhidi ya Asas ya Djibout na ataanzia ugenini ambapo watacheza mchezo wa mkondo wa kwanza kati ya August 18, 19 au 20 na marudiano August 25, 26 au 27.

Simba SC wenyewe wanaanzia round ya pili kutokana na kufanya vizuri na kukusanya point nyingi misimu iliyopita ya michuano ya Kimataifa na watacheza na mshindi kati ya Power Dynamo ya Zambia na African Stars ya Namibia
Screenshot_20230726_054933_Instagram.jpg
 
Simba SC watazindua rasmi wiki ya Simba SC July 29 2023 ambayo wameipa kauli mbiu ya “Unyama Mwingi” wakiwa wana maana huu ni mwaka ambao watarudisha ubabe wao ambapo kilele ni August 6 watapocheza na Power Dynamo ya Zambia.

Simba SC imetangaza kuwa katika kilele cha Simba Day August 6 2023 watacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mabingwa wa Zambia Power Dynamo.

Viingilio vitakuwa ni Tsh 5000/= Mzunguuko, Machungwa Tsh 10,000/=, VIP C Tsh 20,000/=, VIP Tsh 30,000/= na VIP ni Tsh 40,000/= na Platnum Tiketi ni Tsh 200,000/= ambapo hii wataenda uwanjani na usafiri maalum na escort ya Polisi, vyakula na vinywaji wakiwa uwanjani.
Screenshot_20230726_055032_Instagram.jpg
 
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimeishauri Serikali kufuta adhabu ya kifo kwasababu adhabu yenyewe imethibitika hata na Tume ya Haki Jinai kuwa mbali na madhara yake haitekelezeki.

Akiongea leo kuhusu utekelezaji wa mapendekezo muhimu yaliyowasilishwa na Tume ya Haki Jinai kwa Rais Samia, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dkt. Anna Henga amesema Tume imekiri adhabu ya kifo ni katili, inayotweza utu wa Mtu na iliyo kinyume na haki za Binadamu hivyo isiwe adhabu ya lazima na ikitokea Mtu akahukumiwa kifo ikapita miaka mitatu Rais hajaidhinisha kunyongwa basi itenguke na kuwa kifungo cha maisha.

“LHRC kwa miaka mingi imekuwa ikiishauri Serikali kuridhia mkataba wa nyongeza wa kimaitaifa wa haki za binadamu wa kufuta adhabu ya kifo, kwenye mfumo wa haki jinai ulio na changamoto nyingi kama zilivyoainishwa ni rahisi kumhukumu Mtu adhabu ya kifo asiyekuwa na hatia”

“Pamoja na LHRC kuamini kwamba adhabu ya kifo iko kinyume na misingi ya Haki za Binadamu, hata Mahakama za kikanda zilikwisha toa msimamo juu ya adhabu ya kifo”
Screenshot_20230726_055121_Instagram.jpg
 
Mlinzi mwanamke katika kiwanda cha saruji cha Dangote Mtwara, anadaiwa kufariki baada ya kuvutwa na mkanda wa kusafirishia malighafi kiwandani hapo, wakati akitekeleza majukumu yake.

Taarifa ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara, ACP Nicodemus Katembo, imethibitisha kuwa tukio hilo limetokea usiku wa Julai 22, mwaka huu, wakati Asha Issa (24) akiwa katika majukumu yake ya ulinzi kiwandani hapo.

Kwa mujibu wa Kamanda Katembo, mkanda huo ambao ni wa kwenye mashine ya kuchakata saruji, ulisababisha mwili wa Asha kukatwa katwa vipande hadi kufa.

Kwa upande wake, daktari kitengo cha mifupa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara, Phinihas Jackson, pia amedhibitisha kupokea mwili wa marehemu ukiwa amehifadhiwa katika mifuko miwili.

Hata hivyo, mjomba wa marehemu, Athumani Mohammed, amesema taarifa za kifo cha mtoto wao wamezipokea kwa masikitiko.

"Tumepokea taarifa za binti yetu kufariki kwa masikitiko makubwa, japo taarifa zenyewe zimekuja bila kujitosheleza, kwa kuwa hawatukuambiwa chanzo cha kifo chake," amesema Mohammed.

(Imeandikwa na Mwandishi wetu)
Screenshot_20230726_055237_Instagram.jpg
 
Goodluck Chang'a (42) amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo ya Kariakoo, jijini Dar es Salaa, akikabiliwa na shtaka la kujipatia zaidi ya Sh2.6 milioni, kwa lengo la kumshonea suti nne za kiume Godfrey Jacob, matokeo yake alitoweka na fedha hizo.

Akisoma hati ya mashtaka Karani wa mahakama mbiyo, Linda Kivaju, mbele ya Hakimu, Gladness Njau alidai kuwa Julai 25, 2022 hadi Agosti 16, 2022 eneo la Posta jijini Dar es Salaam, mdaiwa alijipatia Sh1, 260, 000 kutoka kwa mlalamikaji Jacob.

Kivaju alidai kuwa mshtakiwa huyo alijipatia fedha hizo kwa lengo la kumshomea suti nne za kiume, kitu ambacho ambalo hakufanya na badala yake alitoweka na fedha hizo, jambo ambalo ni kinyume na sheria.

Baada ya kusomewa shtaka linalomkabili mshtakiwa huyo alikana kosa hilo.

Ndipo Jacob (mlalamikaji) aliieleza mahakama hiyo kuwa atakuwa na kielezo kimoja na kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 2, 2023 kwa ajili ya kusikilizwa.

Screenshot_20230726_055346_Instagram.jpg
 
Serikali imeamua kuondoa pingamizi la awali ambalo iliweka dhidi ya kesi ya kupinga makubaliano ya ushirikiano wa kiuchumi na kijamii baina ya Serikali ya Tanzania na Dubai (IGA), yanayohusu uwekezaji katika bandari nchini.

Serikali ilifikia uamuzi huo baada ya majadiliano baina ya mawakili wa Serikali na wa upande wa madai katika kesi hiyo, muda mfupi kabla ya kesi hiyo kuanza kusikilizwa.

Kesi hiyo imefunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya na mawakili wanne kutoka mikoa tofauti ambao ni Alphonce Lusako, Emmanuel Chengula, Raphael Ngonde na Frank Nyalus dhidi ya Serikali.

Wadaiwa katika kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), ambaye ni mshauri wa Serikali kwa masuala ya kisheria, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na Katibu wa Bunge la Tanzania, ambaye ni Mtendaji Mkuu na Mratibu wa shughuli za Bunge.

Serikali wakati ilipowasilisha majibu yake kwa njia ya maandishi dhidi ya madai hayo, Julai 14, mwaka huu, iliibua pingamizi la awali ikiiomba mahakama hiyo isiisikilize kesi hiyo na badala yake iiondoe mahakamani, huku ikibainisha sababu nne.

Hivyo Mahakama hiyo ilipanga kuisikiliza leo Julai 25, 2023 pingamizi hilo la Serikali sambamba na kesi ya msingi.

Screenshot_20230726_055835_Instagram.jpg
 
Kesi inayowakabili washtakiwa watatu akiwemo polisi jamii wa Mbezi Luis, Juma Mtali, anayekabiliwa na shtaka la kukutwa na vipande 30 vya meno ya tembo vyenye thamani ya Sh239 milioni, imeshindwa kuendelea kusikilizwa baada ya wakili wa utetezi, Samwel Shedrack kudai kuwa ana kesi nyingine ya jinai Mahakama Kuu.

Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa Serikali, Judith Kyamba kuieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa wana mashahidi wawili wapo tayari kuendelea.

Wakili wa utetezi, Samwel Shedrack alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Amir Msumi kuwa ana kesi ya jinai Mahakama Kuu ambayo kusikilizwa mfululizo, hivyo ameiomba Mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine.

“Nina criminal session (kesi ya jinai) Mahakama Kuu, imepangwa kusikilizwa mfululizo, hivyo naomba Mahakama hii ipange tarehe nyingine,” amedai Shedrack.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Msumi alisema kwa sababu wakili anayewawakilisha washtakiwa hao anatakiwa kwenye kesi nyingine ya uhujumu uchumi Mahakama Kuu, hivyo ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 9, 2023 kwa ajili ya kuendelea na usikilizwaji.

Mbali na Mtali washtakiwa wengine ni Kefas Mlenzi (30) mkazi wa Mbezi Luis na Greyson Muhapa (35).

Screenshot_20230726_055929_Instagram.jpg
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu watu wawili kifungo cha miaka miwili jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi, zenye uzito wa kilo 59.59.

Mahakama hiyo, pia imetoa amri ya ya kuteketezwa kwa dawa hizo za kulevya.

Waliohukumiwa ni wakazi wa Kibamba CCM, Scola Kashinde na James Shija, na hii ni baada ya kuingia makubaliano na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) ya kukiri kosa, ambapo kwa mujibu wa sheria mtu akipatikana hatia, adhabu yake ni kifungo cha miaka 30 gerezani.

Akitoka hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu, Mary Mrio; amesema mahakama hiyo imezingatia makubaliano yaliyoingiwa kati ya DPP na washitakiwa hao, na hivyo inawahukuku kifungo cha miaka miwili jela.

Katika kesi hiyo, washitakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo Machi 27, 2023; eneo la Kibamba CCM, Wilaya ya Ubungo, mkoani Dar es Salaam.

Imedaiwa kuwa polisi kwa kushirikiana na viongozi wa mtaa huo, walifanya upekuzi katika makazi ya washitakiwa hao ambapo walikuta bangi hiyo ikiwa imewekwa katika viloba vitano na madumu mawili.

Screenshot_20230726_060035_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom