Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mwenyekiti wa tawi la Simba SC katika Mji Mdogo wa Mchombe, Kata ya Mngeta, Halmashauri ya Mlimba, mkoani Morogoro, Benson Mwakasanga (48) amefariki dunia baada ya kudaiwa kushambuliwa na kundi la watu wasiojulikana usiku wa kumkia leo Julai 25, 2023; akiwa katika mavuno ya mpunga, shambani kwake wilayani Kilombero mkoani humo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama, amethibitisha kutokea kwa tukio, ambapo amesema kuwa tukio hilo limeripotiwa kwa jeshi hilo, na kwamba maafisa wa wake wanakusanya taarifa ili baadaye wazitoe kwa umma.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Julai 25, 2023, Msemaji wa tawi hilo, Supertus Duma, amesema Mwakasanga amekutwa amefariki dunia asubuhi ya leo huku mwili wake ukiwa na majeraha maeneo ya kichwani, kifuani na mikononi hali inayoashiria kuwa kabla ya kifo chake kulikuwa na mapambano.

Duma amesema aliongea naye jana saa 4 usiku wa Julai 24 na kupewa mipango ya kuandaa safari ya Simba Day na saa 5 usiku huo pia aliongea na mtoto.
Screenshot_20230726_060135_Instagram.jpg
 
Habari kutoka kwa Kiongozi wa Upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, zinasema licha ya juhudi za upatanishi za Rais Samia Suluhu Hassan alipozuru nchi hiyo, Serikali ya Kenya inadaiwa kuvuruga juhudi hizo kwa madai kuwa Rais wa Kenya William Ruto, alimfanya Rais Samia kusubiri kwa usiku mbili kabla ya kuweza kusuluhisha mzozo huo.

Raila ameviambia vyombo vya habari vya kimataifa kuwa Samia alikuwa nchini Kenya wiki mbili zilizopita.

"Kama tulivyoripoti hapo awali, wiki mbili zilizopita (wakati huo Rais Samia inasemekana alikuwa nchini Kenya), Rais Ruto alitangaza hadharani kuwa yuko tayari kufanya mazungumzo na mtu yeyote, akiwemo Kiongozi wa Azimio, ilimradi ajenda hiyo isihusishe kushikana mikono (handshake)," imesema taarifa hiyo.

Screenshot_20230726_060235_Instagram.jpg
 
Mpiga Kinubi maarufu Mwanadada Siobhan Brady leo July 25, 2023 ameweka rekodi ya Dunia ya Guinness juu ya Mlima Kilimanjaro futi 19,000 kwa kupiga kinubi (kifaa kinachoheshimika nchini Ireland) kwa muda wa dakika 34 akiwa kileleni na kuvunja rekodi ya kupiga kinubi kwa muda wa dakika 18.

Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa @gersonmsigwa ametoa taarifa hiyo leo ambapo amesema awali Siobhan alipiga kinubi akiwa futi 16,000 katika Mlima Himalaya nchini India mwaka 2018.

Rekodi hii inaitwa “Guinness World Record for the Highest Harpist Concert” na imerekodiwa na kituo runinga cha Kimataifa kiitwacho National Geographic na sasa Kamati ya Dunia ya Guinness inasubiriwa kuthibitisha rekodi hiyo. View attachment 2699310

X wangu huyo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom