Hili ndo likawa PIGO kubwa kwa Yanga. Huwezi amini walihangaika kufukua mafaili ya zamani kupata picha ambazo wao pia walipeleka jezi mlimani. Wakasahau kwamba wao walipeleka jezi, siyo walizindua.
.
Wakasahau kwamba wao wana tamasha linakuja. Wakaacha kucheza ngoma yao, wakaanza kucheza ngoma ya Simba...wakawa wameingia kwenye mtego. Na Simba walivyokuwa makini...wakapeleka kibegi cha jezi mlimani na kuhakikisha kinazungumziwa njia nzima. Matokeo yake safari ya kibegi ikawa kubwa kuliko ya tamasha.
.
Hatimaye kikafika kileleni...jezi zikazinduliwa. Yanga na watu wote wakaanza kuzichambua jezi za Simba...kosa jingine. Tamasha limekaribia lakini hakuna anayelikumbuka sio Ally Kamwene, siyo Priva wala Manyara wote wako bize na jezi za Simba.
.
Kama kuna watu wa kulaumiwa, basi Yanga tujilaumu wenyewe. Hatukuwa na mkakati madhubuti wa kujaza uwanja...na tulizidiwa sana maarifa na wapinzani wetu, Simba. Angalia kilichotokea, tamasha lilipofika, Simba wakakaa kimya...hakuna tweet za Mo wala Barbara. Chama yuko Uturuki. UMAFIA.