Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,400
- 465,165
Mkazi wa Kijiji cha Miule wilayani Tandahimba, amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 20 jela, baada ya patikana na hatia ya kukutwa na kucha za mnyama ajulikanaye kwa jina la Mhanga.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Nicodemus Katembo, amesema kuwa, kesi hiyo ni kati ya kesi 76 zilizofikishwa katika mahakama mbalimbali na kutolewa hukumu.
“Yusuph Stephen Mkwemba (42) alikutwa na kucha hizo ambazo ni nyara za Serikali nyumbani kwake, zenye thamani ya Sh1.52 milioni. Mahakama imemtia hatiani na kumfunga kwa kuwa ni kosa kisheria kuwa na nyara hizo,” amesema.
(Imeandikwa na Florence Sanawa)