Makapuku Forum

Makapuku Forum

MIKEL Arteta amesema kwamba Declan Rice ataiongezea Arsenal mzuka wa kubeba ubingwa msimu ujao. Kiungo huyo ghali kabisa kwenye historia ya Arsenal juzi Jumatatu alifanya mazoezi ya kwanza na wenzake.

Arteta alisema: “Tutakachopata kutoka kwa Declan ni uwezo wake wa kuongoza. Namwona kama tu atakayehamashisha kuweka mambo vizuri na kufanya timu icheze vizuri. Hiyo itaongeza ubora mkubwa. Kwa namna anavyozungumza, kuna kitu ataleta kwenye timu.”

Arteta, 41, aliongeza: “Presha ipo kwetu sasa. Baada ya tulichofanya msimu uliopita, watu watataka kuona nini kitafuata na tumefanya usajili muhimu pia. Hakuna kilichotofauti na wengine, lakini ukiwa Arsenal unapaswa kukabiliana na presha.”

Usajili wa Rice na ule wa Jurrien Timber na Kai Havertz umeifanya Arsenal kutumia Pauni 200 milioni kwenye dirisha ili la uhamisho wa majira ya kiangazo huko Ulaya.

Screenshot_20230720_082558_Instagram.jpg
 
Straika wa Tottenham Hotspur, Harry Kane anadaiwa hafikirii na hana mpango wa kujiunga na Paris St-Germain katika dirisha hili la usajili licha ya taa-rifa kudai mabosi wa timu hiyo wanamwangalia kama mbadala wa Kylian Mbappe ambaye huenda akaondoka kabla ya dirisha la usajili Ulaya kufungwa.

Kane ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwakani anatajwa kuwa na nafasi kubwa ya kutua katika kikosi cha Bayern Munich
Screenshot_20230720_082648_Instagram.jpg
 
Simba imenasa mrithi wa Jonas Mkude baada ya kunasa saini ya kiungo Mtanzania aliyekuwa Tusker, Hamis Abdallah.
.
ACHANA na kuharibu kwake mipango ya wapinzani kwa ukabaji wake wa kibabe ndani ya uwanja Ujio wa Hamis utaongeza chachu ya ushindani kwenye eneo la kiungo la Simba.
Screenshot_20230720_125316_Instagram.jpg
 
Mabosi wa Singida Fountain Gate hawatanii kwani wanaonyesha kutoshiriki tu mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao, bali kushindana.
.
Hilo ni wazi kwani wapo mbioni kukamilisha usajili wa mshambuliaji Thomas Ulimwengu ambaye ni mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba Mazembe.
.
Habari ambazo ninazo ni kwamba mchezaji huyo na mastaa wengine ambao hawajatambulishwa tayari wapo kwenye mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea mkoani Arusha kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.
Screenshot_20230720_125447_Instagram.jpg
 
WAKATI kundi la mwisho la wachezaji wa Simba likijianda kupaa leo kwenda kambini Ankara, Uturuki, winga anayerejeshwa Msimbazi kutoka Al Ahly, Luis Miquissone anatajwa kufunika kwa dau la mshahara atakaokuwa analipwa kikosini.
.
Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya Simba zinaeleza kwamba winga huyo ndiye atakuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi akivuta mshahara wa Sh 34 milioni kwa mwezi.
.
Mabosi wa Simba, tayari wamempa Luis mkataba wa miaka miwili na anatarajiwa kuungana na Kocha ‘Robertinho’ kuanzia leo, Alhamisi pamoja na wenzake kambini Uturuki.
Screenshot_20230720_125547_Instagram.jpg
 
TAREHE kama ya leo mwaka 2020, Cristiano Ronaldo anakuwa mtu wa kwanza kufunga mabao 50 katika Ligi Kuu ya Italia (Serie A), Ligi Kuu ya Hispania (La Liga) na Ligi Kuu England (EPL) baada ya kufunga mabao mawili wakati Juventus ikishinda 2-1 dhidi ya Lazio.
Screenshot_20230720_125637_Instagram.jpg
 
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya imempa ajira ya mkataba Mariam Mwakabungu (25) kama sehemu ya kuthamini mchango wake kwa kujitolea kuokoa maisha ya Watoto wachanga (Njiti) waliokimbiwa na Mama zao katika Hospitali ya Amana ambapo amekuwa akiwakumbatia ili wapate joto na kuongeza uzito.

Waziri Ummy amesema Rais Samia amefurahishwa sana na upendo wa Mariam na licha ya kumpa milioni 2 jana ameridhia Serikali impe Mariam ajira ya mkataba, kwakuwa hana vigezo vya kuajiriwa moja kwa moja kwa sasa lakini wamemshauri ajiendeleze kwanza kielimu ili apewe ajira ya kudumu hapo baadae.

“Kwakweli Mh. Rais ameguswa sana na moyo wa Mariam, Madaktari wanasema ana moyo wa kujitoa na anapenda kufanya hiyo kazi, ataingizwa katika utaratibu huo ili aweze kupata sifa, kwa sasa ana miaka 25 bado ana muda anaweza kusoma uuguzi ngazi ya astashahada akawa Muuguzi wa Watoto njiti”

@AyoTV_ ilipotaka kufahamu kama Serikali inao mpango wa kutoa ajira hizo kwa Watu wengi zaidi ili kuokoa maisha ya Watoto njiti, Waziri Ummy amesema kwa sasa wataanza na wale wenye moyo wa kujitolea kwanza ndipo wafikirie kuwaajiri “Tukipata Watu wenye moyo kama wa Mariam kwakweli tutakua tunawaajiri kwa mkataba, nikitoa wito watafurika wengi kwasababu wapo Watu mitaani hawana ajira”

Rais Samia alimpa Mariam milioni 2 jana kama pongezi huku Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundation, Doris Molllel akimchangia pia Mariam ambaye amekaa Hospitalini hapo kwa mwezi mmoja sasa akifanya huduma hiyo ‘tumchangie chochote cha kumpa moyo kwenye 0782124700 (Alise Mwakabungu)”
Screenshot_20230720_125741_Instagram.jpg
 
Rais wa Kenya, Dk William Ruto, amesema yuko tayari kufanya mazungumzo kuhusu masuala yanayo waathiri Wakenya, na siyo yale yahusuyo kugawana madaraka na kiongozi wa Azimio la Umoja, Raila Odinga.

Mtandao wa Nation umelipoti leo kuwa Rais Ruto, akiwa katika Mji wa Kericho jana, alihutubia taifa katika siku ya kwanza ya maandamano ya kitaifa ya siku tatu, yakilenga kupinga ongezeko la kodi na gharama za maisha, huku akiwataka Polisi kuwashugulikia ipasavyo watu aliowaita wahalifu na wavurugaji wa amani ya nchi.

"Tuliawaambia wapinzani wetu kutushirikisha mazungumzo ya hoja zao kupitia uwakilishi wa wabunge wao, lakini wamechagua maandamano. Wanatakiwa kutumia njia zinazokubalika kisheria na kikatiba kuwasilisha madukuduku yao," amesema Rais Ruto.

Ruto aliongeza kuwa uongozi wake haukinzani na vifungu vya Katiba vinavyoruhusu maandamano lakini; "Hatutakuwa Taifa la vurugu na migogoro...mtu yeyote asitutimie vifungu hivi kuchochea machafuko, sisi ni taifa la Kidemokrasia na lenye amani," alisema Ruto muda mfupi baada ya kuzindua mradi wa uzalishaji maji wa Kimugu wenye thamani ya Sh1.5 bilioni (za Kenya).

Screenshot_20230720_131857_Instagram.jpg
 
Maandamano yanayohamasishwa na uongozi wa Azimio la Umoja yameingia siku ya pili kati ya tatu zilizotangazwa na kiongozi wa umoja huo, Raila Odinga kwa lengo kupinga ongezeko la kodi na kupanda kwa gharama za maisha.

Kupitia mitandao ya kijamii, Odinga aliutangazia Umma Jumatatu kuwa maandamano hayo yatafanyika kwa siku tatu mfululizo kuanzia jana Jumatano Julai 19, 2023 hadi Ijumaa Julai 21 mwaka huu.

Pamoja na picha kusambaa mitandaoni zikionyesha vijana wamebeba matairi ikiwa ni maandalizi ya kuendeleza maandamano hayo, miji inaonekana kutulia kutokana na maofisa wa polisi na vikosi vya kuzuia ghasia kusambazwa maeneo mbalimbali yanayohisiwa kuwa na makundi yenye lengo la kuandamana.

Mtandao wa Nation nchini humo umeripoti leo kuwa baadhi ya watu waliokomatwa jana akiwemo Seneta wa Kilifi nchini humo, Stewart Madzayo na Ken Chonga (Mbunge wa Kilifi Kusini), wanaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi huku wakitarajiwa kifikishwa mahakamani muda wowote kwa kosa la kuendesha maandamano kinyume na sheria.

Hata hivyo, baadhi ya maduka na huduma za kijamii ikiwemo shughuli za masomo zilizositishwa jana zimerejea katika hali yake wakati ambao juhudi za kudhibiti maandamo hayo hayo zinaendelea.

Screenshot_20230720_132017_Instagram.jpg
 
Nyota wawili wa Simba, Fabrice Ngoma na Clatous Chama wameondoka leo alfajiri kuelekea nchini Uturuki kwa ajili ya kuungana na wenzao katika maandalizi ya msimu mpya wa mashindano 2023/24.
.
Viungo hao wanatarajiwa kuwasili Ankara, Uturuki na kujiunga na wenzao leo usiku.
Screenshot_20230720_135648_Instagram.jpg
 
Mwanzoni ilisemekana kuwa ni zoezi la utayari lakini Jeshi la Polisi limethibitisha kwamba ni ajali ya kweli iliyotokea Bukoba Mkoani Kagera ya Ndege ndogo ya Jeshi kuanguka kando ya Ziwa Victoria baada ya Marubani kutaka kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Manispaa ya Bukoba.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera Blasius Chatanda amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa ndege hiyo ilikuwa na Marubani wawili ambao ni Meja Lenald Revocatus (45) na Luteni Alex Venance Moshi (30) na kusema hali za Marubani hao ni shwari na hakuna majeruhi wala kifo kilichotokana na ajali hiyo.

Screenshot_20230721_050244_Instagram.jpg
 
Watu wanne wa familia moja kutokea jimbo la Florida nchini Marekani wamepatikana na hatia kwa kosa la kuuza dawa ya kuondoa madoa sugu kwenye nguo ‘bleach’ yenye sumu kama tiba ya magonjwa mbalimbali yakiwemo Saratani ya Ubongo, Corona na virusi vya UKIMWI kupitia kanisa lao linaloendeshwa mtandaoni.

Mahakama ya shirikisho la jiji la Miami ilimkuta na hatia Mark Grenon (65) na Watoto wake watatu Jonathan (37) Joseph (35) na Jordan (29) na hatia ya kula njama ya kuwatapeli Raia wa Marekani na kuuza dawa za kuondoa madoa kwenye nguo kuwa kama dawa za kutibu magonjwa.

Shtaka hilo hubeba kifungo cha hadi miaka mitano jela ambapo hukumu yao inatarajiwa kutolewa Oktoba 6, 2023.

Kanisa la Familia ya Bradenton liitwalo ‘Genesis II, Church of Health and Healing’ liliuza kile kilichojulikana kama dawa ya muujiza na uponyaji kufikia thamani ya dola milioni 1 (Tsh Bil 2.4) ambapo Watu hawa waliwaaminisha Raia kuwa dawa hii ni tiba ya 95% ya magonjwa sugu yakiwemo Corona, ugonjwa wa kusahau kwa wazee ‘Alzheimer's’, Saratani ya ubongo, VVU/UKIMWI na vinginevyo waendesha mashtaka walisema kumbe muda wote walikuwa wanauza “chlorine di oxide” ambayo hutumika kama dawa ya kutibu maji na kusafisha nguo.
Screenshot_20230721_050418_Instagram.jpg
 
Mfanyakazi wa ndani ambaye jina lake limehifadhiwa, anatafutwa na Jeshi la Polisi nchini Kenya, baada ya kudaiwa kumuua bosi wake Rahab Karisa, kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali, siku moja baada bosi huyo kurejea nchini toka Italy.

Kwa mujibu wa tovuti ya Tuko ya nchini humo tukio hilo limetokea alfajiri ya leo Alhamisi Julai 20, 2023, kwenye makazi ya ofisa huyo yaliyopo eneo la Mnarani Classic Estate nje ya Mji wa Kilifi.

Akithibitisha kutokea kwa mauaji hayo, Kamanda wa Polisi Kaunti ya Kilifi, Fatuma Hadi, amesema wapelelezi katika eneo la tukio wamebaini majeraha ya kisu kwenye mwili wa marehemu, huku kisu hicho kikipatikana pembeni ya mwili wake.

"Tulitembelea eneo la tukio na kufanikiwa kupata kisu kilichotumika kuondoa uhai wa Rahab. Mwili wake una jeraha linaloonekana, lakini tunatarajia kupata majibu zaidi baada ya uchunguzi wa kitabibu kufanyika," amesema Kamanda Fatuma.

Amesema mpaka mauti yanamkuta, Karisa alikuwa Ofisa Mkuu wa Kilimo na Uchumi katika Kaunti hiyo na kwamba mwili wake uko katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Kaunti ya Kilifi, ambapo uchunguzi wa kitabibu unafanyika.

“Baada ya uchunguzi wa awali kufanyika, inadaniwa kuna pesa ambazo hazionekani na inawezekana ni moja ya sababu iliyomfanya mfanyakazi huyo kumuua bosi wake,” amesema na kuongeza;

“Baada ya kutekeleza mauaji hayo, msichana huyo ametoroka na sasa anasakwa na Jeshi la Polisi ili tumfikishe katika mikono ya sheria na apate haki yake kutokana na tukio hilo.”

(Imeandikwa na Sute Kamwelwe)
Screenshot_20230721_050650_Instagram.jpg
 
Mamlaka ya Udhibiti wa Mafuta na Maji (Ewura), imegundua mchezo ‘mchafu’ wa kuhodhi mafuta kwenye maghala, jambo linalosababisha kuwepo kwa changamoto ya upatikanaji wa bidhaa hiyo katika mikoa kadhaa nchini.

Mkurugenzi wa Ewura Dk James Andilile amesema kilichopo ni kwamba magari yanayopaswa kusafirisha mafuta, yanatumia muda mrefu yanapofika kwenye maghala hayo na hivyo kusababisha maeneo yenye uhitaji wa mafuta kukosa nishati hiyo katika muda muafaka.

“Unakuta gari linaenda ghala ‘A’ kuchukua mafuta, likifika linaelekezwa kwenda ghala jingine, hivyo muda unapotea,” amesema Dk Andilile alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 20, jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa bosi huyo wa Ewura, nchi ina mafuta ya kutosha na kwamba mamlaka ilikuwa ikijiuliza sababu za baadhi ya maeneo kukosa mafuta, jambo lililowalazimu kufanya ukaguzi katika ‘depo’ kubwa za mafuta kwa lengo la kujua maeneo yenye changamoto.

Dk Andilile amesema baada ya kutembelea ‘depo’ hizo wamegundua upangaji wa magari kuingia na kutoka ghala moja kwenda jingine ndiyo chanzo cha madereva kushindwa kufikisha mafuta kwa wahitaji katika muda muafaka.

Aidha Dk Andilile amewaonya wale wote wanaohodhi mafuta kwa kigezo cha kungoja bei ipande amesema wakibainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.

(Imeandikwa na Sute Kamwelwe)

Screenshot_20230721_050808_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom