Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20230717_063140_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20230717_063158_Opera%20Mini.jpg
 
Winga machachari, Pape Ousmane Sakho ameomba kusepa kwenda kucheza soka la kulipwa barani Ulaya. Inaelezwa, Sakho amepata ofa kutoka Ubelgiji na Ufaransa, lakini bado ana mkataba na Simba hivyo memejimenti ya mchezaji huyo imeuandikia uongozi wa Msimbazi kuomba imruhusu kuvunja mkataba ili adili na ofa alizonazo.
.
Sakho amesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja inadaiwa ana ofa kutoka Stade Malherbe Caen na Grenoble zinazoshiriki Ligi Daraja la Pili Ufaransa, lakini ikielezwa kuna klabu ya Ubelgiji nayo inamtaka. Sakho amepata ofa hizo baada ya mfululizo wa kiwango bora ikiwamo kuitwa Timu ya Taifa ya Senegal pamoja na tuzo yake ya Bao Bora la CAF. Hadi sasa Sakho yupo zake kwao Senegal akisubiri hatma yake.
.
Kama Simba itashindwa kumuachia Sakho katika kipindi hiki, staa huyo atarejea kikosini, lakini hataongeza mkataba na atacheza hadi msimu umalizike kisha aondoke akiwa mchezaji huru.
Screenshot_20230717_064104_Instagram.jpg
 
Jeshi la Polisi Tanzania limepiga marufuku maandamano yaliyoitishwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) katika Wilaya zote za Tanzania ili kuiunga mkono Serikali juu ya uwekezaji katika bandari.

Msemaji wa Polisi, David Misime amesema “Julai 16, 2023 kupitia Vyombo vya Habari mbalimbali ikiwepo mitandao ya kijamii ameonekana Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) akitoa taarifa ya kuhamasisha maandamano katika Wilaya zote na wataanza na Dar es salaam July 18,2023 ili kuiunga mkono Serikali juu ya uwekezaji katika bandari, sheria ipo wazi kwa Mtu au kikundi cha Watu kinapotaka kuitisha maandamano taratibu zipi zinatakiwa kufuatwa”

“Pamoja na utaratibu huo wa kisheria, kuitisha maandamano Nchi nzima ni sawa na kutaka kuleta vurugu na hofu kwa Watanzania bila sababu yeyote ile kwani yapo majukwaa ya kuwasilisha jambo lolote lililo katika utaratibu wa kisheria bila kuhamasisha maandamano ya aina hiyo”

“Kwa msingi huo, Jeshi la Polisi linapiga marufuku maandamano hayo yasifanyike na hii ni pamoja na Watu wengine pia wenye nia kama hizo na badala yake wawasilishe hoja zao kupitia mikutano na vyombo vya habari”
Screenshot_20230717_064224_Instagram.jpg
 
Kikosi cha kutafuta Simba kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi (TAWA) na TAWIRI kilichokuwa Kijiji cha Ilamba Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa leo July 16,2023 kimefanikiwa kumuua simba mmoja Dume ambaye alimvamia Askari na kumjeruhi wakati akidhibitiwa kwa kulazwa usingizi ili arudishwe Hifadhini.

Afisa Uhusiano Mkuu wa TAWA, Vicky Kamata @vickykamatalikwelile amesema “Simba hawa walikuwa wawili ambapo mmoja alikimbia akabaki mmoja, katika harakati za kumdhibiti ili wamchome sindano ya usingizi na kumrudisha Hifadhi ya Ruaha, Simba huyo alitoka machakani kwa hasira na kumvamia Askari CR III Charles Mafuru na kumjeruhi kichwani na mkono,

“Askari mwingine alilazimika kumpiga risasi ya moto Simba huyo baada ya kuona amemuangusha Afande Charles na amekaa juu yake akijiandaa kumshambulia shingoni na kumuua, baada ya Askari kumuua Simba walimpeleka Mgonjwa Hospitali ya Wilaya ya Kilolo ambako alipewa matibabu na kuruhusiwa, hali yake inaendelea vizuri”

“Washiriki wa Doria hiyo iliyofanikisha kumuua Simba ni Dr. Mwakyusa (TAWA) , Dr. Emmanual (TAWIRI), CR III Charles Mafuru (TAWA), CR III Dologo Nkolo (TAWA), Cr III Paul Masatu (TAWA) na CR III Daniel Isangya (TAWA)”

“Matukio ya simba kuua mifugo kwa mara ya kwanza yalijitokeza June 13, 2023 eneo la Kalenga Iringa Vijijini na tangu muda huo wamesababisha vifo vya ng’ombe 36, nguruwe 10, mbuzi 12 na Kondoo 5, hakuna tukio la Mwananchi kuvamiwa na simba hao.

“Zoezi la kuwasaka Simba hao linaendelea ambapo jana kulionekana alama za simba na Mtoto wake eneo la Ihemi, ufuatiliaji ulibaini wameelekea Ifunda Wilaya ya Mufindi”
Screenshot_20230717_064406_Instagram.jpg
 
Jeshi la Polisi limepiga marufuku maandamano yaliyoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) yenye lengo la kuunga mkono uwekezaji katika bandari.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na msemaji wa Jeshi hilo, David Misime jana Jumapili Julai 16, 2023 imesema maandamano hayo ya nchi nzima yatazua taharuki zisizo na msingi na badala yake hoja zote ziwasilishwe katika vyombo husika.
Screenshot_20230717_064533_Instagram.jpg
 
Jeshi la Polisi Tanzania limepiga marufuku maandamano yaliyoitishwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) katika Wilaya zote za Tanzania ili kuiunga mkono Serikali juu ya uwekezaji katika bandari.

Msemaji wa Polisi, David Misime amesema “Julai 16, 2023 kupitia Vyombo vya Habari mbalimbali ikiwepo mitandao ya kijamii ameonekana Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) akitoa taarifa ya kuhamasisha maandamano katika Wilaya zote na wataanza na Dar es salaam July 18,2023 ili kuiunga mkono Serikali juu ya uwekezaji katika bandari, sheria ipo wazi kwa Mtu au kikundi cha Watu kinapotaka kuitisha maandamano taratibu zipi zinatakiwa kufuatwa”

“Pamoja na utaratibu huo wa kisheria, kuitisha maandamano Nchi nzima ni sawa na kutaka kuleta vurugu na hofu kwa Watanzania bila sababu yeyote ile kwani yapo majukwaa ya kuwasilisha jambo lolote lililo katika utaratibu wa kisheria bila kuhamasisha maandamano ya aina hiyo”

“Kwa msingi huo, Jeshi la Polisi linapiga marufuku maandamano hayo yasifanyike na hii ni pamoja na Watu wengine pia wenye nia kama hizo na badala yake wawasilishe hoja zao kupitia mikutano na vyombo vya habari”
View attachment 2690364
Wangeruhusu hayo maandamano ya ccm sisi nasi tungeunga huko huko ila tungekuwa kinyume nao.
 
KOCHA wa Bayern Munich, Thomas Tuchel ameweka wazi nafasi ya Sadio Mane ni ndogo sana kwenye kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria wa Bundesliga. Mabingwa hao wanajiandaa kumpiga bei Mane kwa kitita cha Pauni 17 milioni, ili wapate pesa ya kuongezea kwaajili ya kunasa saini ya Harry Kane.
.
Kwa mujibu wa Sport1, Tuchel alisema: “Hakuwa na matarajio makubwa baada ya kujiunga, ushindani ni mkali sana, nafasi ya kikosi cha kwanza imekuwa ngumu na mchezaji anaelewa pia, anaelewa mawazo yangu na klabu kwa ujumla.”
Screenshot_20230717_065122_Instagram.jpg
 
DEAL DONE | Kuelekea msimu ujao 2023|24, Ihefu SC imekamilisha usajili wa washambuliaji wawili kutoka Coastal Union na Tanzania Prisons

Ihefu imewasajili Amza Moubarack Ngamchia raia wa Cameroon kutoka Coastal Union na Ismail Mgunda kutoka Tanzania Prison.
Screenshot_20230717_122256_Instagram.jpg
 
Football Clinic ya Celta Vigo na Magnet Youth Academy yamalizika kwa Mafanikio.

Clinic mbili za mpira wa miguu zilizoendeshwa na makocha kutoka Academy ya Celta Vigo- Spain huku wakiwashirikisha makocha zaidi ya 25 kutoka kituo cha michezo cha Magnet Academy zimeleta mafanikio ambayo yanaendelea kuchochea maendeleo katika soka la vijana.

Pamoja na kusifu mpangilio na maendeleo ya wachezaji wa Magnet Academy, kiongozi wa Msafara huo Kocha Diego Salgado alisema Celta Vigo Academy inafurahia ushirikiano wao na kituo hiki cha Tanzania.

“Uwezo na muelekeo tuliouona kwa wachezaji wa Magnet ulifanya kazi yetu ya kufundisha kuwa rahisi zaidi.”

Kocha Diego, pia alishukuru ushirikiano na weledi wa makocha wa kutoka katika kituo cha Magnet. Kitu ambacho kiliwafanya waweze kuwafundisha vitu vingi zaidi makocha wa hicho kituo.

Mwenyekiti wa Kituo cha Magnet Ndugu Tuntu Mwambusi ameeleza kuridhika na namna mafunzo yalivyo endeshwa huku akitoa habari za awali kwamba kuna kati ya wachezaji 8-10 wanatarajiwa kuletewa mwaliko wa kwenda katika kituo cha Celta Vigo nchini Hispania kwa mafunzo ya muda mfupi.
Screenshot_20230717_122401_Instagram.jpg
 
WAKATI anaondoka Yanga akitoka kuwapa ubingwa wa Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na ASFC kwa msimu wa pili mfululizo na sasa unapoisoma habari hii ni kwamba Kocha Nasreddine Nabi ametua kwa mabingwa wa Morocco FAR Rabat kuanza kazi ya kuinoa timu hiyo.
.
Nabi wakati wowote kuanzia leo atasaini mkataba wa kuifundisha FAR Rabat. Timu hiyo ya jeshi la nchi haikuwa rahisi kupata saini ya Nabi kutoka na Wydad nao walikuwa wanamsaka kocha huyo akachukue nafasi ya Sven Vandenbroeck aliyetimka hivi karibuni na kutua CR Belouizdad ya Algeria.
Screenshot_20230717_122454_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom