Huyu Bwana anaitwa Ike Ekweremadu... alikuwa Seneta katika Bunge la Nigeria.
Mwaka jana Ike pamoja na mkewe Beatrice Nwanneka Ekweremadu walimsafirisha kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 21 kwa jina Daniel kutoka Nigeria kwenda Uingereza kwa madai kwamba walikuwa wanampeleka kumtafutia kazi na wangempa pesa Shilingi milioni 21 hivi kwa ajili ya kuanzia maisha. Kumbe jamaa alikuwa amepanga kwenda kumtoa figo ili apandikiziwe binti wao ambaye figo zake zilikuwa zimefeli.
Baada ya kufika hospitali na kijana kufanyiwa maandalizi ya upasuaji akashtuka, akasema mimi nimeletwa kufanya kazi mbona mnanisainisha upasuaji tena.
Madaktari wakamwambia we si mmekubaliana unakuja kuchangia figo. Figo tena.
Daniel akapiga kelele. Polisi wakafanya uchunguzi na kuwafungulia mashtaka Seneta Ike, mkewe pamoja na daktari waliyeshirikiana kuchora mchongo huo.
Seneta amehukumiwa kifungo cha miaka 9 jela, mkewe miaka 4 na daktari miaka 10.
Kijana huyo aliiambia mahakama kwamba hataki kufungua hata kesi ya kuomba fidia kwa sababu hataki kitu chochote kutoka kwa hao watu kwa sababu wana roho mbaya.
Kwa sasa Daniel anaishi mafichoni huko Uingereza. Kwa sheria za Uingereza mtu anayepaswa kuchangia viungo anapaswa kuwa ndugu wa karibu au mtu ambaye mmekuwa katika mahusiano kwa muda mrefu mfano mke au mume...!