SIMBA imekuwa na utaratibu mara kwa mara wa kuwatafutia baadhi ya mastaa wao sehemu za kuishi na wachezaji wengi wa timu hiyo wanaishi kwenye Apatimenti maeneo ya Mbezi jijini Dar es Salaam. Hizi ni za kishua Zaidi.
.
Kundi kubwa la wachezaji wa Simba pamoja na baadhi ya watu wa benchi la ufundi wanaishi kwenye eneo hilo ambalo inaidaiwa kuna makubaliano maalumu kati ya timu hiyo na uongozi wa Apatimenti hiyo.
.
Chanzo kinaonyesha kuwa kila mmoja analipa kitita cha dola 700 kwa mwezi mmoja. Sawa na Sh1.6Milioni. Mastaa wanaoishi hapo ni Sadio Kanoute, Peter Banda, Pape Sakho, Jean Balek, Augustine Okrah na wengine wengi wanaotoka nje ya nchi.
.
Mastaa hawa wa Simba kwenye usafiri wengi wamekuwa wakikodi kutoka kwenye makampuni mbalimbali, lakini wakati mwingine wamekuwa wakitumia ya wachezaji wenzao au marafiki. Ingawa tunajua kwamba kwenye mikataba yao kuna sehemu kuna makubaliano ya kupewa gari ila baadhi yao hutaka kupewa fedha tasilimu na kuweka mifukoni na kutumia ya kukodi.