Makapuku Forum

Polisi Tanzania rasmi imeshuka daraja kutoka Ligi Kuu Bara hadi Championship baada ya leo kukubali kichapo cha mabao 6-1 kutoka kwa Simba SC.

Polisi Tanzania anaungana na Ruvu Shooting ambayo nayo mechi ya kushuka daraja ilicheza dhidi ya Simba katika Uwanja wa Chamazi, Dar na kufungwa mabao 3-0 Mei 12.

Mabao ya Simba yamefungwa na Saido Ntibazonkiza (5) na Israel Mwenda (1) huku la Polisi Tanzania likifungwa na Henock Mayala (1).

 

Habari nzuri sana hizi
 
Rais Yoweri Museveni amesema yupo tayari kutoa ruzuku kwenye mbolea lakini sio kutoa ruzuku kwenye mafuta ya petroli ili Watu wakajazane na magari yao kwenye starehe zikiwemo ‘Night Clubs’ wakati tayari petroli ilishapunguzwa bei kutoka pesa za Uganda (UGX) 6,563 hadi 5,138.

Museveni (78) amesema wote wanaotaka kwenda kwenye starehe na magari yao gharama za mafuta zinatakiwa kuwa juu yao japokuwa anaweza kutoa ruzuku endapo tu bei zitayumbishwa na vikwazo vinavyowezwa kuwekwa kwao na Nchi za Magharibi ambazo hazijapendezwa na maamuzi ya Nchi hiyo kupitisha sheria dhidi ya Wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Rais Museveni ameyasema haya wakati akilihutubia Taifa kuongelea changamoto mbalimbali zinazolikabili ikiwemo mfumuko wa bei za vyakula, gharama za maisha na ufisadi na jinsi ya kuzitatua changamoto hizo wakati huu ambao Nchi za Magharibi zinatishia kuiwekea Serikali yake vikwazo vya kiuchumi baada ya kupitisha sheria dhidi ya wanaoshiriki vitendo vya ushoga.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…