Farhan Jr
A story to tell, picha ambazo zina maandishi mengi kwenye mikono yangu! Nilikuwa nina uwezo wa kufahamu vitu vya kuvisoma ila sikuwahi kuuishi utamaduni tofauti na kufahamu maisha ya nchi nyingine.
Sikuwahi kuona namna gani Makocha wanaandaa Wachezaji kuelekea mechi kubwa ama Wachezaji wanajiandaa vipi kuelekea mechi kubwa zaidi ya kusoma vitabuni.
Ukiniuliza kama Mimi Kijana kutoka Morogoro niliwahi kuiota picha hii nitakuwa naongopa, sikuwahi kufikiria nitafika nchi hii ya mpira, kwa ajili ya mpira na kukutana na watu wa mpira.
Siku moja nitaandika juu ya hii picha, sote tulimtazama Coach Nabi hapo baada ya Press Conference, alizungumza vitu kama Baba ambaye kila Kijana anapaswa kusikia.
Kwangu safari hii ni darasa kubwa sana sana sana, nina mengi ya kuandika kama sio hivyo basi nina mengi ya kusimulia siku moja nikiwa kijijini kwangu huko Ifakara, Morogoro.