Makapuku Forum

Mawaziri na wabunge wakiwapongeza Waziri wa Nishati, January Makamba na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Stephen Byabato baada ya Bunge kupitisha bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/2024, jijini Dodoma leo.

Bunge limepitisha kiasi cha Sh3 trilioni kutumiwa na wizara hiyo katika mwaka ujao wa fedha.
 
Waziri wa Nishati, January Makamba amawaeleza Wabunge kwamba hataki kuwadanganya kuwa tatizo la kukatika umeme, litaisha mwakani au mwaka mwingine unaofuata.

Hata hivyo ametoa ahadi ya kuhakikisha kila mwaka wizara yake itakuwa inapunguza tatizo hilo kufuatia uwekezaji wa miradi mbalimbali ya umeme ambayo inaanza kukamilika.

Makamba ameyasema hayo Bungeni Dodoma wakati akijibu hoja za Wabunge waliochangia mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/2024, ambapo Sh3 trilioni tatu zimeidhinishwa.

 
Mratibu na Mwakilishi wa Mradi wa Mazingira UN nchini Tanzania, Clara Makenya amesema ni asilimia 0.5 ya maji duniani yanafaa kwa matumizi.

“Ni asilimia 0.5 tu ya maji duniani ndiyo yanafaa kwa ajili ya kutumiwa ikiwa na maana kuwa ni salama.

Rasilimali ya maji ni kitu sensitive na utaona hili kwa jinsi ilivyofungamana na sehemu nyingine kama uzalishaji umeme kwa kutumia maji.

Uhitaji wa kuwa na nishati jadidifu ni mkubwa zaidi lakini hautaendelea kutumia maji kama hayo maji hayatopatikana,” amesema Makenya.

 
Waziri wa Nishati, January Makamba amesema watu wanaofanya kazi ya kuwachafua na kuwasema mabaya yeye na wenzake wizarani hapo wao watalipa kisasi Cha kutoa matokeo chanya kwenye utendaji kazi zao katika sekta ya nishati.

Makamba ameyasema hayo wakati akijibu hoja za wabunge waliochangia mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/2024, jijini Dodoma leo.
 
Wafanyabiashara wa mahindi katika soko la Kimataifa la mazao Holili, Mkoani Kilimanjaro leo Juni Mosi wameandamana mpaka ofisi za Forodha mpakani mwa Kenya na Tanzania, baada ya shehena za mahindi kuzuiwa katika mpaka huo kuingia Kenya.

Wafanyabiashara hao wameeleza kukwama katika mpaka huo kwa siku nne baada ya kuzuiliwa kupeleka mahindi nchi jirani hali ambayo imezua sintofahamu kwa wafanyabiashara hao.

Mwananchi limefika katika eneo hilo na kushuhudia shehena hizo za mahindi zikiwa kwenye foleni ambapo muda mfupi baadaye magari hayo yaliruhusiwa kuendelea na safari.

Kufuatia hali hiyo, Gazeti hili lilimtafuta Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kilimanjaro, James Jilala kujua ni kwanini magari hayo yenye shehena hiyo yamezuiliwa ambapo amesema wao wamepata maelekezo kutoka juu kusitisha mahindi kutokutoka nje ya mpaka huo.

"Tulipata taarifa kutoka kwa viongozi wa juu kwamba tusitishe mahindi yasitoke nje ya nchi ya Tanzania na baadaye tumeletewa taarifa hilo zoezi limeahirishwa kwa muda wa siku kadhaa na wameambiwa ni baada ya muda ndio sasa litakuwa limekuja zuio," amesema Jilala.
 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT Center Limited, Godfrey Kirenga: Zao la mahindi katika mkoa wa Iringa, Mbeya na Songwe unaweza kufikia ufanisi w zaidi ya tani 10 kwa hekta.

Tumefanya mbinu hizi kwa kutumia wakulima kama 2000 na wameweza kufikia wastani wa tani 7 hadi 8 kwa hekta, hili ni ongezeko kubwa na ni ishara kuwa inawezekana.

Mfano mwingine ni Mkulima wa viazi mviringo mkulima wastani wake ni kati ya tani 5 hadi 7 kwa hekta lakini akitumia mbinu za kilimo bora tumeweza kuwafikisha hadi wastani wa tani 28 katika mkoa wa Njombe.

Katika hao wakulima kuna wengine wamefika hadi tani 50 kwa hekta kwa viazi mviringo na wako juu ya viwango vya dunia ambavyo ni tani 40 kwa hekta.”

 
CHENGA KAMA ZOTE
.
Wachezaji watano waliokuwa na wastani bora zaidi ya kupiga chenga kimafanikio kwa dakika 90 msimu huu katika Ligi Kuu England (wastani ni mchezaji aliyecheza dakika 900):
.
4.9 - Allan Saint-Maximin
3.5 - Adama Traore
3.4 - Kamaldeen Sulemana
3.2 - Luis Diaz
2.6 - Said Benrahma
 
Maisha safi wanayoishi mastaa mbalimbali wa Simba na Yanga hapa jijini Dar es Salaam. Wachezaji hawa wamekuwa wakiishi kwenye majumba ya kifahari.
 
Kwa mujibu wa daktari wa Simba amenambia Kama kila kitu kitakwenda sawa basi kesho Ijumaa wataruhusiwa kutoka Hospitali na kurejea nyumbani Tanzania.

 
Real Madrid wanaweza kumnunua Kane iwapo mshambuliaji wa Ufaransa Karim Benzema, 35, atakubali ofa nono aliyotangaziwa huko Saudi Arabia. (Times)
 
Chelsea wanataka kumuuza beki wa kati wa Senegal Kalidou Koulibaly, 31, ambaye alisajiliwa kwa pauni milioni 33 kutoka Napoli msimu uliopita wa joto. (Evening Standard)

 
BREAKING: Inter Milan wanajitahidi sana kumsajili beki wa Chelsea Trevoh Chalobah kwa £25m, na wanawasiliana kila siku na kambi yake.
󠁧

 
Arsenal wametoa ofa ya kuongeza mshahara wa William Saliba mara tatu zaidi katika mkataba mpya wenye thamani ya £120,000 kwa wiki, lakini wanahofia kumpoteza beki huyo wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 22 kwenda Paris St-Germain. Lakini inasemekana ataikataa pia ofa hii (Sun)

 
Kocha Robertinho.
“Tutaleta wachezaji ambao wana njaa ya mafanikio kwa hadhi ya Simba na sio vinginevyo. Simba ni klabu ya Makombe sio kuwa hapa tulipo.”

 
Manchester United, Barcelona na Inter Milan wana nia ya kumsajili beki wa pembeni wa Ufaransa Benjamin Pavard, 27, ambaye hataki kuongeza mkataba mpya pale Bayern Munich, wa sasa unakakamilika 2024. (L'Equipe).

 
Newcastle wamempa Bruno Guimaraes mkataba mpya wenye mshahara pauni 200,000 kwa wiki ili asiende Liverpool, Real Madrid au Barcelona zinazomtaka na kumfanya kiungo huyo wa kati wa Brazil, 25, kuwa mchezaji anayelipwa zaidi klabuni hapo. (Sun)
 
Joao Felix atapelekwa Newcastle kwa mkopo na klabu mama Atletico Madrid siku chache tu baada ya Chelsea kutangaza kutomsajili mshambuliaji huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 23 kwa uhamisho wa kudumu. (Mail)
 
Kocha wa PSG, Christophe Galtier amethibitisha kuwa nyota wake Lionel Messi ataondoka klabuni hapo mwisho wa msimu huu.

Akizungumzia hilo kocha huyo amesema anajivunia kumfundisha mchezaji huyo bora katika historia ya soka duniani.

"Jumamosi itakuwa mechi yake ya mwisho kwa Messi tutakapocheza dhidi ya Clermont," amesema Galtier

Messi anahusishwa asilimia kubwa kurudi klabu yake aliyotoka Barcelona baada ya kocha Xavi kuonyesha nia ya kumuhitaji msimu ujao.

 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…