MOUNT NA WENZAKE 14 WAPO SOKONI
.
Chelsea inaripotiwa kuwa na mpango wa kupitisha panga kwenye kikosi chake na kuna orodha ya mastaa wasiopungua 15 watafunguliwa mlango wa kutokea huko
Stamford Bridge kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi.
.
The Blues chini ya mmiliki wake, Todd Boehly hivi karibuni ilimteua Mauricio Pochettino kuwa kocha wao mpya, ambako ataanza kazi rasmi Julai Mosi, lakini tayari imeshafahamika majina ya wachezaji ambao safari itawahusu kwenye dirisha lijalo la majira ya kiangazi huko Ulaya ili kupunguza idadi ya wachezaji waliopo Stamford Bridge.
.
Kilichoelezwa ni kwamba mastaa hao wanaohusishwa na mpango wa kuondoshwa Chelsea ni pamoja na mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang, Mason Mount, Trevoh Chalobah, Conor Gallagher, Ruben Loftus-Cheek na Callum Hudson-Odoi. Wengine wenye uwezekano wa kuachwa waondoke ni N’Golo Kante, Hakim Ziyech, Christian Pulisic, Mateo Kovacic, Kalidou Koulibaly, Cesar Azpilicueta, Edouard Mendy na Denis Zakaria, ambaye ataruhusiwa kurudi kwenye klabu yake ya Juventus baada ya mkopo wake kufika mwisho na Chelsea haijafurahishwa kumchukua.