Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa
Mabalozi mbalimbali ambapo amemteua Gelasius Byakanwa kuwa Balozi, kabla ya uteuzi huo Byakanwa alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kisha baadaye akawa Afisa Mkuu Ubalozi wa Tanzania, Korea ya Kusini.
Rais Samia amemteua pia Meja Jenerali Ramson Godwin Mwaisaka kuwa Balozi, kabla ya uteuzi huo, Meja Jenerali Mwaisaka alikuwa Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Wanamaji (WTZ), amemteua Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli kuwa Balozi, kabla ya uteuzi huo Meja Jenerali Simuli alikuwa Mkuu wa Utumishi Jeshini (JWTZ).
Wengine walioteuliwa kuwa Mabalozi ni Mohamed Awesu, Dkt. Mohamed Juma Abdallah ambaye alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kaskazini Unguja, Hassan Mwamweta ambaye alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mwandamizi na Mkuu wa Utawala, Ubalozi wa Tanzania, Uturuki, wengine ni Imani Salum Nialikai na Khamis Mussa Omar.
Uteuzi huu wa Mabalozi umeanza May 10, 2023 na wataapishwa kwa tarehe itakayopangwa baadae.