Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20230503_052357_Opera%20Mini.jpg
 
ETI HAALAND ATAFIKA EURO BILIONI 1
.
Ndo hivyo. Wakala wa straika wa Manchester City, kiboko ya nyavu Erling Haaland amesema mteja wake atakuwa mwanasoka wa kwanza kuwa na thamani ya Euro 1 bilioni (Sh 2.6 trillion)
.
Wakala wa straika huyo wa Norway, Rafaella Pimenta alisema: “Anagharimu kiasi gani? Nataka kuwaambia atakuwa mwanasoka wa kwanza kuwa na thamani ya bilioni. Hebu fikiria tu kile anachofanya wakati akiwa na umri wa miaka 22 tu. Hii nguvu yake ni balaa, atakwenda kuvunja rekodi zote.”
.
Man City ipo kwenye msako wa mataji matatu Haaland ndani ya msimu huu kwenye michuano yote ngazi ya klabu amefunga mabao 50.

Screenshot_20230503_070419.jpg
 
LONDON IS RED
.
FT: ARSENAL 3-1 CHELSEA
17’—️ Odegaard
31’—️ Odegaaard
34’—️ Jesus
65’—️ Madueke
.
Mbio za Ubingwa EPL
1. Arsenal — (34) — 78pts
2. Man City — (32) — 76pts
.
Screenshot_20230503_070536.jpg
 
Wabunge wa Uganda wamekubali kufanya marekebisho yaliyopendekezwa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni kuhusiana na sheria za vitendo vya ushoga Uganda na wametoka na rasimu ya pili itakayorudi kwa Rais ili kutiwa saini, hatua hii inakuja baada ya Rais Museveni kukataa kutia saini muswada wa kwanza uliopendekezwa na Bunge.

Chini ya muswada huo mpya uliopendekezwa tabia za ushoga bado itakuwa kinyume cha sheria lakini Watu wanaojitambulisha kama LGBTQ+ bila kufanya vitendo vya ushoga hawataadhibiwa.

Kosa la ushoga uliokithiri pamoja na vitendo vya ngono baina ya Ndugu bado litaadhibiwa kwa adhabu ya kifo, pia Wananchi wanahitajika kisheria kuripoti vitendo vya ushoga ikiwa vinafanywa dhidi ya Watoto na Watu walio katika mazingira magumu ambapo adhabu ya kutotoa ripoti ni faini au kifungo cha miezi sita.

Muswada huo pia umependekeza hukumu ya kifo kwa kosa la kufanya ngono zembe ukijua kuwa una maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU).

Mswada huo hapo awali ulipendekeza adhabu ya kifungo cha miaka 20 kwa wanaojitambulisha kama LGBTQ+ ila kwa sasa hawataadhibiwa na sheria lakini wale ambao wanajulikana au watathibishwa kuhusishwa na mapenzi ya jinsia moja ndio wataadhibiwa kisheria.
Screenshot_20230503_140001.jpg
 
Wakati kiongozi wa Kanisa la Good News International nchini Kenya, Mchungaji Paul Mackenzie na wenzake wakiwa wanashikiliwa na polisi wakihusishwa na vifo vya zaidi ya watu 110 vilitokea karibu na eneo la kanisa lake, mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili, Faustin Munishi ‘Malebo’ kwa mara ya kwanza amezungumza namna walivyoshindwana kutokana na mafundisho yake potofu ya kidini.

Munishi amesema alikutana na Mackenzie mwaka 2015 na kuwa marafiki wakubwa na kwamba wakati huo alikuwa mtumishi mwema aliyekuwa akimiliki kanisa na kituo cha televisheni lakini 2019 alishindwana nae baada ya kuona ameanza kuwadanganya watu kupitia mafundisho aliyokuwa akiyatoa..

Kiongozi huyo aliyejifanya kuwa kiongozi wa kiroho yuko chini ya ulinzi wa polisi kwa madai ya kuhubiri fundisho hatari linalowahimiza wafuasi wake kujiua kwa njaa ili waende mbinguni.
Screenshot_20230503_140248.jpg
 
Watu zaidi ya 15 wamenusurika kifo baada ya gari ya dogo la mizigo kugongana na daladala inayofanya safari zake kati ya Moshi mjini na Mwika mkoani Kilimanjaro katika eneo la Shaa Tours.

Mwananchi Digital ilifika eneo la ajali ambapo majeruhi wote wamechukuliwa na kupelekwa Hospitali ya Mkoa ya Mawezi.

Hata hivyo jitihada za kumtafuta Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro zinaendelea.

Screenshot_20230503_140359.jpg
 
Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson ni miongoni wa wabunge waliowasilisha maombi ya kugawa majimbo yao ili kuwa mawili kutokana na ukubwa na wingi wa watu.

Taarifa hiyo imetolewa leo bungeni na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Ummy Nderiananga wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Viti Maalum Sophia Mwakagenda.

Katika swali lake Mwakagenda ameuliza ni lini serikali italigawa jimbo la Mbeya mjini ambalo linaongozwa na Spika wa Bunge Tulia Ackson kutokana na ukubwa wake.

“Mheshimiwa Tulia Ackson alishawasilisha kwenye mamlaka nia ya kuomba jimbo hilo ligawanywe, serikali inatafakari maombi hayo na wakati utakapofika vigezo vitatazamwa,” amesema Ummy.

Screenshot_20230503_140506.jpg
 
Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ametangaza kuwa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya mwaka 2023 iliyosainiwa na Rais Samia Suluhu Hassan Januari 31, 2023 imeanza kutumika kuanzia Mei Mosi mwaka huu.

Sheria hiyo iliyopigiwa kelele na wanaharakati wa masuala ya haki za binadamu imeanzisha vitu vitatu ambavyo ni Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, bodi ya masuala ya taarifa binafsi na ulinzi wa faragha ya watu.

Akizungumza na wandishi wa Habari, wakili Benedict Ishabakaki amesema sheria hiyo inalazimisha wakusanya taarifa wote yakiwemo makampuni ya simu, hospitali, vyuo vikuu n.k kusajiliwa na tume ya ulinzi wa taarifa binafsi.

“Lazima uende ujisalimishe kwamba mimi ni mmoja wa wakusanya taarifa za watu ili uweze kusajiliwa. [..] Kwa sheria hii sasa imenyima kutoa taarifa za Mtanzania yoyote nje ya nchi bila aidha ya ridhaa ya tume ama bila ya ridhaa ya mtu husika,” amesema.
Screenshot_20230503_140641.jpg
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Mifugo na Uvuvi kurudisha utaratibu wa kuiwekea hereni za kielektroniki kwa ajili ya utambuzi na udhibiti wa uingizwaji wa mifugo kutoka nje ya nchi bila vibali.

Amesema hayo Jumanne Mei 02, 2023 alipotembelea maonesho ya wadau wa mifugo na uvuvi yanayoendelea kwenye viwanja vya Bunge, jijini Dodoma.

“Wizara iliingiza mfumo wa kuvisha hereni. Hereni ya kielektroniki inaonesha tarehe aliyozaliwa, yuko maeneo gani na maendeleo yake. Ilikuwa na kasoro tukarekebisha, sasa wizara rudisha ule utaratibu.

Lakini wekeni vikao na wadau, utaratibu unarudi kwa sura ipi, sura ile iwe ni sura inayomwezesha mfugaji kuona kama kuna umuhimu wa kuweka alama ili kubainisha ng’ombe wa ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania,” amesema.

Aidha, amesema mifugo mingi inayotoka nje inatumia rasilimali za Tanzania ikiwemo malisho ya mifugo ambayo iko mahususi kwa ajili ya mifugo iliyopo nchini na kupelekea bajeti kutokidhi mahitaji ya mifugo.
Screenshot_20230503_140730.jpg
 
Baraza la Habari Tanzania (MCT) limesema katika kipindi cha miaka 10 tangu mwaka 2012 wandishi wa habari 272 wamekumbwa na madhila tofauti kazini ikiwemo ajali, kupigwa, kunyang’anywa vifaa vya kazi, kutekwa na kuuawa.

Aidha, MCT imesema taasisi inayoongoza kwa matukio mengi dhidi ya uhuru wa vyombo vya habari ni polisi yenye matukio 51, ikifuatiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) yenye matukio 21.
Screenshot_20230503_140819.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom