Makapuku Forum

Makapuku Forum

Wizara ya Utumishi wa Umma na Kazi Nchini Rwanda imewatangazia Waajiri na Waajiriwa wote Nchini humo wa Sekta za Umma na Sekta Binafsi kwamba kesho Ijumaa April 21,2023 ni Siku ya Mapumziko ya Kitaifa hivyo Watu hawatoenda kazini ili kuwapa fursa ya kusherehekea Sikukuu ya Eid El Fitri.

Wizara imesema imechukua uamuzi huo baada ya Jumuiya ya Waislamu Rwanda (RMC) kuthibitisha kwamba mwezi umeandama na kesho ni Eid.
Screenshot_20230421_041127.jpg
 
Naibu Kadhi Mkuu wa Kenya Sukyan Omar ametangaza kuwa mwezi umeonekana kwenye maeneo kadhaa ya Kenya ikiwemo Mandera na Wajir na hivyo kesho Ijumaa April 21,2023 itakuwa ni Eid Al Fitr Nchini Kenya.
Screenshot_20230421_041252.jpg
 
Mufti Mkuu na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakari Zubery ametangaza kwamba mwezi haujaonekana leo hivyo kesho Waislamu wataendelea kufunga Ramadhan kukamilisha siku 30 na Eid Al Fitri itakuwa Jumamosi.

“Tumefuatilia katika vyanzo vyetu pamoja na Watu ambao tunashirikiana nao Kenya, Zanzibar kote Mwezi haujaonekana na kwetu Tanzania Mikoa yote tumewasiliana nao lakini Mwezi haukuonekana, nimelithibitisha hilo na natangaza kwamba kesho tunaendelea kufunga na Eid itakuwa Jumamosi”
Screenshot_20230421_041434.jpg
 
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limesema kuwa baada ya kufanya ukaguzi kwenye maduka mbalimbali kote Nchini limejiridhisha kwamba toleo namba 22318RB la bidhaa za Johnsons Baby Powder iliyodaiwa kuwa na uchafuzi wa madini ya asbestos yanayosababisha saratani, halikuingia Nchini na halipo popote katika soko la Tanzania.

Tayari Kampuni inayozalisha bidhaa hizo imetangaza rasmi kusitisha matumizi ya kiambato cha talc katika uzalishaji wake duniani kote na badala yake kutumia kiambato cha comstarch ambapo tayari TBS imechukua hatua ya tahadhari kuhusiana na suala hilo hivyo imewalekeza Wananchi kutoendelea kutumia bidhaa za Johnson's Baby Powder zenye kiambato cha talc kama ilivyokishaelezwa awali kupitia Vyombo vya habari.

Screenshot_20230421_041545.jpg
Screenshot_20230421_041606.jpg
Screenshot_20230421_041628.jpg
 
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Khamis Sued Kagasheki kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole kuanzia tarehe 18 Aprili, 2023, Kagasheki amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwemo Uwaziri wa Maliasili na Utalii na Ubunge wa Bukoba Mjini.
Screenshot_20230421_042418.jpg
 
Wahenga walisema kikulacho kinguoni mwako. Usemi huu umemfika mwanamke mmoja wa Kenya aliyetambuliwa kwa jina moja la Mercy baada ya mumewe kuoa shoga wa mkewe.

Taarifa iliyotolewa na mtandao wa Tuko wa Kenya umebainisha kwamba licha ya usaliti huo, fedha zilizotumika kufanikisha ndoa hiyo ni za Mercy ambazo alikuwa akimtumia mumewe, mama huyo alipokuwa nje ya nchi.

Mercy ambaye ni mama wa watoto watatu amesema alikwenda kufanya kazi nje ya nchi na akiwa huko alikuwa akimtumia mumewe fedha kwa ajili ya kujenga nyumba na kuendesha miradi mbalimbali.

“Kumbe wakati natuma fedha zile kwa ajili ya ustawi wa familia yangu, mume wangu alikuwa anazitunza na akazitumia kumuoa rafiki yangu wa karibu,” amesema Mercy.

Mercy aliyefunga ndoa na mwanamume huyo miaka nane iliyopita amesema ametuma fedha kwa miaka mitatu kwa lengo la kununua ardhi na kujenga nyumba.

“Najisikia maumivu kwa sababu mshahara wangu nilimtumia lakini amelipia mahari na kumuoa rafiki yangu na sasa ameniacha na watoto hawa,” amesema .
Screenshot_20230421_042800.jpg
 
Am Makaveli

SAMUEL ETO'O FILLS PIGENI MHURI MASELA HATUMDAI HUYU MTU.

Samuel Etoo, Kwanza tulimuuliza Mhenga mmoja hapa Banda Umiza, tulitaka kujua kuhusu hii Afrika na soka lake. Ni mhuni sana anatupa simulizi kishkaji kuhusu Kazadi Mwamba wa nchi ya zamani ya Zaire, anasogea zama za kina Jean Manga Onguene, Thomas Nkono na Theophile Abega kisha anamalizia simulizi tamu ya kizazi cha kina George Weah na Rogger Milla

Banda Umiza wanasikia majina ya kutisha sana, Mzee anazungumzia viumbe kama Abeid Pele, Mohamed Aboutrica, Didier Yves wa Ivory Coast na wengine wengi. Mwisho anavua ile kofia yake anataka mitaa na masela wa Banda Umiza wajue anaongea nini. Anataka kila mtu apate hisia ya Mshambuaji wa mpira kisha anatupa onyo kali atatufukuza humu ndani siku akisikia tunaongea kuhusu Afcon bila kumtaja Simba asiyefugika

Yes ni miaka 42 iliyopita kitongoji kimoja huko Douala Cameroon kinamleta huyu mtu. One of the best ever, Samuel Eto'o Fils dunia ilimpokea March 10 1981. Weka kituo kwanza. Turudi sasa kwenye Afcon yenyewe, kuna matusi mengi sana na mabalaa mazito aliyafanya kule Nigeria mwaka 2000 na pale Mali mwaka 2002

Hiyo miaka yote Cameroon anachukua Afcon mbele ya Nigeria ya mtu kama Jay Jay Okocha, na ile Senegal ya El Hadji Diouf lakini stori sio Cameroon kuchukua hayo makombe, stori ni huyu Simba asiyefugika

Banda Umiza haliwezi kusahau Eto'o alikuwa mnyama sana hatumii nguvu nyingi kama Didier Drogba, anasprint kushoto au kulia ni skills nyingi na chenga za maudhi huyu mtu, pale Hispania kwenye dimba la Estadio Remaroda usiku mmoja.......

Screenshot_20230421_044246.jpg
 
Amri Kiemba

“Kwa mazingira na namna ambavyo hizi timu zilivyo [Simba na Wydad Casablanca] na kwa heshima ya mpira wa miguu Simba inaweza kushinda kwa Mkapa.”

“Kwa takwimu sasa ndio unakuja kugundua ugumu wa mechi, ugumu unaletwa na timu ambazo zinacheza. Wydad ni bingwa mtetezi lakini ameanza kwa nguvu kuutetea ubingwa.”

“Kuna timu inachukua ubingwa halafu msimu unaofata anakuwa hoi! Wydad anatetea kama ndio anautafuta ubingwa, hicho ntio kitu ambacho kinaweza kuleta tofauti.”

“Ukiangalia bingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika RS Berkane, msimu huu ipo hoi na imetolewa hatua za mapema.”

“Wydad ni timu ngumu kwa Simba lakini kwa historia ya Simba uwanja wa Mkapa inaonekana ni mechi ngumu pia kwa Wydad kuzuia kile ambacho Simba imekuwa ikikifanya uwanja wa Benjamin Mkapa.”

“Inawezekana kumbukumbu za Raja bado zipo kwa watu wengi, inawezekana kilichoikuta Simba mbele ya Raja tayari kimekuwa somo ambalo wakati wanakutananao hawakuwanalo.”

“Nyakati ambazo Simba ilifanikiwa kushinda mbele ya Al Ahly, AS Vita na hata kutoka sare na TP Mazembe, walikuwa wanaziheshimu hizo timu na historia zao lakini kwa Raja, Simba walikuwa wazi sana kama wanacheza mechi ya Ligi Kuu!”

“Sioni Simba wakifanya hivyo tena dhidi ya Wydad kufunguka bila kujua wanawazuiaje.”

“Kwa hiyo Simba kushinda uwanja wa Benjamin Mkapa inawezekana lakini matokeo ya jumla yatategemea zaidi mechi ya pili.”

Screenshot_20230421_044759.jpg
 
Malisa gj

Mechi imeingiza 410M then mwenyeji anapewa 100M na ushee? Karibu 240M zimepotelea kwenye makato. Yani makato ni makubwa kuliko mtaji. Biashara kichaa.!

Hata mchanganuo haueleweki. Uwanja 47M, gharama za mechi 22M, ticket 22M. What the difference? Kama uwanja na ticket vimelipwa hizo gharama nyingine za mchezo ni zipi nyie vishohia?

Hiki ki-TFF cha Karia ni cha hovyo zaidi kuwahi kutokea tangu ikiitwa FAT. Bora hata enzi za Ndolanga na "wapigaji" wenzie kuliko hili genge la sasa.

Mwaka juzi Karia aliulizwa mafanikio ya TFF akasema Simba kufika robo fainali klabu bingwa Afrika. Yani jibu la ki-tabularasa kabisa. Timu ligi kuu ziko ngapi? Kwanini ujipime kwa Simba pekee? Na so far TFF imefanya nini specific kwa Simba ambacho ni tofauti na vilabu vingine?

Bila shaka saivi akiulizwa swali hilo atasema mafanikio ya TFF ni pamoja na Yanga kufika robo fainali shirikisho. Wakati anajua hakuna chochote specific ambacho TFF imefanya kwa Yanga wala Simba. Ni juhudi zao binafsi, uongozi, wachezaji na benchi na ufundi. TFF hawajachangia chochote zaidi ya kula pesa za viingilio, kumfungia @hajismanara na kutoa adhabu za ki-imla kwa yeyote mwenye maoni tofauti na genge lao.

Kwa kifupi TFF ya Karia inadidimiza soka kuliko kuendeleza. Timu inapata 410M unapiga panga 240M, halafu ikifanya vizuri kimataifa unajikomba kwayo. Idiot.!

@shaffihdauda_ amepigania sana soka la mtaani kupitia #NdondoCup. Alistahili Nishani ya heshima, lakini anaishia kupigwa majungu na haohao wanaojifanya kuendeleza soka. Soka gani mnaendeleza wakati kila mdau mnampiga vita?

Tar 26 April 2021 Karia aliliambia gazeti la The Citizen kuwa FIFA imewapa TFF $5M sawa na TZS 11 Bilioni kwa maendeleo ya soka nchini. Jiulize wamefanyia nini? Wameshindwa kuweka hata digital screen pale kwa Mkapa. Wameweka board za mabati ambapo mchezaji akijigonga anapata tetenasi. Azam hawana pesa za FIFA lakini uwanja wao wameweka digital screen. Wanalipana mishahara mikubwa lakini wameshindwa kufunga screen? Ukihoji unafungiwa kujihusisha na soka. Upuuzi!

Hii iwe chachu kwa vilabu vikubwa kama Simba na Yanga kujenga viwanja vyao. Huu upigaji umezidi. Kati ya TFF na andazi, nachagua andazi. Stupid (in SSH's voice).!
Screenshot_20230421_050648.jpg
 
Anaandika Joram Kiango,
______

Bilionea’ Femi Otedola katika mahojiano ya simu, aliulizwa na mtangazaji wa redio, "Bwana ni nini unachoweza kukumbuka kilikufanya kuwa mtu mwenye furaha maishani?"

Femi alisema: “Nimepitia hatua nne za furaha maishani na hatimaye nikaelewa maana ya furaha ya kweli.

Hatua ya kwanza ilikuwa ni kujilimbikizia mali na mali. Lakini katika hatua hii sikupata furaha niliyotaka.

Kisha ikaja hatua ya pili ya kukusanya vitu vya thamani na vitu. Lakini niligundua kuwa athari ya jambo hili pia ni ya muda mfupi na uangazaji wa vitu vya thamani haudumu kwa muda mrefu.

Kisha ikaja hatua ya tatu ya kupata miradi mikubwa. Wakati huo nilikuwa nikishikilia 95% ya usambazaji wa dizeli nchini Nigeria na Afrika. Pia nilikuwa mmiliki mkubwa wa meli barani Afrika na Asia. Lakini hata hapa sikupata furaha niliyokuwa nimeiwazia.

Hatua ya nne ilikuwa wakati rafiki yangu aliniuliza ninunue viti vya magurudumu kwa watoto fulani walemavu. Karibu watoto 200 tu.

Kwa ombi la rafiki, mara moja nilinunua viti vya magurudumu. Lakini rafiki huyo alisisitiza kwamba niende naye na kuwakabidhi watoto viti vya magurudumu. Nilijiandaa na kwenda naye.Hapo nilitoa viti hivi vya magurudumu kwa watoto hawa kwa mikono yangu mwenyewe. Niliona mwanga wa ajabu wa furaha kwenye nyuso za watoto hawa. Niliwaona wote wakiwa wamekaa kwenye viti vya magurudumu, wakizunguka huku na huko na kujiburudisha.

Ilikuwa ni kana kwamba walikuwa wamefika kwenye eneo la picnic ambapo wanashiriki ushindi wa jackpot.

Nilihisi furaha ya kweli ndani yangu. Nilipoamua kuondoka mtoto mmoja alinishika miguu. Nilijaribu kuifungua miguu yangu taratibu lakini mtoto alinitazama usoni na kunishika miguu kwa nguvu.

Niliinama na kumuuliza mtoto: Je! unahitaji kitu kingine? Jibu alilonipa mtoto huyu halikunifurahisha tu bali pia lilibadilisha mtazamo wangu wa maisha kabisa.

Mtoto huyo alisema: “Nataka kukumbuka uso wako ili nitakapokutana nawe mbinguni, niweze kukutambua na kukushukuru.!
Screenshot_20230421_050915.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom