Farhan Jr
FERGIE NA GUARDIOLA, MWANZO WA NA MWISHO WA ENZI.
Majira ya kiangazi huko nchini Uswisi, nyumba maalum ya UEFA wenyewe wanapaita UEFA Football House, pembezoni mwa Lake Geneva mandhari nzuri sana kama Lake Victoria jijini Mwanza, ndio ni makao makuu ya shirikisho la soka barani Ulaya kulikuwa na mkutano maalum wa Makocha Ulaya kujadili mpira na mabadiliko ya kimfumo na utawala.
Siti ya mbele ameketi Don Carlo Ancelotti, nyuma yupo Arsene Wenger The Professor, Marcelo Bielsa na Mafundi wengi ila Jose Mourinho ameketi pembeni ya Sir Alex Ferguson, ila nyuma yao yupo Pep Guardiola Sala amevalia suti yake ameketi kwa unyenyekevu sana! Mwanafunzi bora zaidi wa mchezo huu pendwa.
Wakati wa mapumziko Makocha wengi walikuwa wanapiga stori ila Pep alijitenga peke yake maana hana historia kubwa Ulaya na ni 2008 punde tu baada ya kupewa kibarua Barcelona, Pep ni Kijana mkimya aliyependa kujifunza sana kwa wakongwe.
Alikuwa ni Jose Mourinho aliyemfuata Pep na kumwambia sogea jumuika nasi, Pep akamwambia anatamani sana kuongea na Sir Alex Ferguson! Basi Jose Mourinho akamwambia Mzee atachukua kahawa ataelekea Balcony basi mfuate akienda kule ili useme nae, Pep alimshukuru sana Mourinho kumbuka ni wana sana hawa japo huwa wanapasuana sana
Ni kweli Babu Fergie alichukua kahawa kisha akatoka taratibu kuelekea Balcony kutazama mandhari ya Ziwa Geneva, zuri la kuvutia kama Victoria kasoro yake hili ni kuwa halina Wasukuma

! Ndipo Pep akaenda kuongea na Babu, alipofika akamsamilia kwa heshima sana! Babu akamjibu kwa upendo sana kwakuwa ni Mtu safi Mskochi.
Guardiola kumbuka alishasafiri mpaka Argentina kupata madini ya Marcelo Bielsa ‘Priest of the Nun’ kisha amekaa na Godfather Johann Cruyff na sasa ni zamu ya Fergie kumpa baraka zake, hawa hapa Watalaam wawili wanazungumza mpira wa miguu.
Dunia haikuwahi kufahamu kama msimu huo wa 2008/09 watakutana fainali pale Roma, ila wapiga picha haswa Steve Arnolds alipiga picha akijua ni ya kawaida kati ya Fergie na Shabiki wake tu, ila ilikuwa picha ya Fergie na mrithi wake kwenye ufalme wa mbinu na mamlaka kwenye soka la kisasa! Yes the Senior na Junior wake.
Babu Fergie akawa……
ITAENDELEA!