Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 56 Mkazi wa Buzilayombo Wilayani Chato Mkoani Geita anatafutwa na Polisi kwa tuhuma za kumuuwa Mkewe aitwaye Kasaka January (48) kwa kumkata mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake chanzo kikidaiwa kuwa ni tamaa za mali zilizokuwa zinamilikiwa na Mwanamke huyo Mchapakazi.

Kamanda wa Polisi Geita ACP. Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mpaka sasa Mwanaume huyo amekuwa akiishi nyumbani kwa Mama huyo "kiini cha tukio hili ni tamaa ya mali, nichukue nafasi hii kutoa wito kwa Jamii tutafute kwa jasho letu kila siku naendelea kusema kwamba matukio kama haya ni matukio ya kutokuwa na hofu ya Mungu"

RPC Safia amesema Mwanaume huyu amekuwa akiishi akiishi nyumbani kwa Mama huyo na Watoto ambao sio wa kwake na kwamba Mwanamke huyu alikuwa ni Mchakarikaji aliyemzidi Mume wake kipato ambapo mkasa uliibuka baada ya kupotea kwa betri za Mwanamke huyo ambazo hutumika kwenye shughuli za uvuvi.

"Baada ya betri kupotea Mama huyo alianza kutoa taarifa na kusema ameshamjua Mtu aliyezichukua betri hizo ndipo Mwanaume huyo akajishitukia na kuchukua uamuzi huo"
Screenshot_20230420_144501.jpg
 
Mbunge wa Arusha Mjini (CCM), Mrisho Gambo amehoji kwanini Taasisi ya Kuzia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) haiwakamati watu waliohusika na ubadhirifu wa fedha za waendesha bodaboda jijini Arusha.

Gambo ameyasema hayo leo Alhamis Aprili 20, 2023 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mwaka 2023/2024.

Akichangia hoja hiyo, Gambo amesema kuna masuala yako wazi lakini mchakato wake unakuwa mrefu sana.

Amesema mwaka 2017/2018 kuna mchakato ulianzishwa Arusha bodaboda walichangisha fedha kiasi cha Sh400 milioni ambazo baadaye anadai ziliibiwa na baadhi ya watu.
Ametaja nyakati tofauti fedha zilizochukuliwa na watu ambao wanafahamika ikiwemo Juni 18 mwaka 2021, Sh39.5 milioni na Julai 8,2021 Sh 43.5 milioni, Sh 43.8 zilichotwa Agosti 31,2021 na Novemba 25, 2020 walichukua Sh15 milioni.

“Kuna orodha ndefu hoja ni kwamba fedha za bodaboda zimeibiwa na walioiba wanajulikana wameenda benki wametoa vitambushio vya Nida (vya Taifa) na wamechukua kwa majina yao lakini hadi leo halijapelekwa mahakamani na wahusika hawajakamatwa,”amesema.

Screenshot_20230420_144756.jpg
 
Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limetangaza mapato ya mechi ya Simba vs Yanga iliyopigwa Aprili 16 na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 iliingiza Sh410 milioni.

TFF imeeleza mgawanyo wa hela hizo ambapo VAT ni Sh62 milioni, Baraza la Michezo (BMT) Sh10 milioni, gharama za tiketi Sh22 milioni, uwanja Sh47 milioni na mchezo ni Sh22 milioni.

Taarifa iliyotolewa na TFF imeeleza kuwa wao wamepata Sh12 milioni, Bodi ya Ligi Kuu Sh25 milioni, FA mkoa wa Dar Sh18 milioni.

Timu mwenyeji wa mchezo huo Simba imepata Sh188 milioni ambapo kwa mujibu wa kanuni timu mgeni kama ilivyo Yanga huwa haipati kitu.
Screenshot_20230420_144858.jpg
 
Kutokana na mtindo wa maisha na malezi kubadilika nchini na duniani kwa ujumla, watoto wenye umri kati ya miezi sita hadi miezi 23 wapo hatarini kupata ugonjwa wa kisukari, ripoti ya Utafiti wa Afya, Viashiria na Malaria imesema.

Ripoti hiyo ya mwaka 2022 iliofanywa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imeonesha kundi hilo lipo hatarini kwa sasa kupata kisukari na kuongeza uzito uliopitiliza.

“Asilimia 30 ya watoto wenye umri wa miezi sita hadi 23 wanalishwa vinywaji vyenye sukari huku asilimia tisa ya watoto wenye umri huo wanalishwa vyakula visivyo na virutubisho muhimu,” imesema ripoti hiyo.

Takwimu hizo ni sawa na watoto watatu kati ya 10 wapo hatarini kupata magonjwa ya kisukari na moyo kutokana na aina ya vinywaji wanavyotumia katika umri huo.

Ripoti hiyo ya mwaka 2022 ilizinduliwa jijini Dodoma Januari 2023 na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ikiwa ni ya saba tangu ianze kutolewa ambapo ripoti ya kwanza ilitolewa mwaka 1999 ikionyesha hali ya Afya, Malaria na Ukimwi nchini.
Screenshot_20230420_145043.jpg
 
Maelfu ya wakaazi wa mji wa Khartoum nchini Sudani wamekimbia kutokana na mapigano kati ya jeshi na wapiganaji wa kikosi cha dharura cha Rapid Support Forces (RSF) yanayoonyesha kutokuwa na ukomo.

Mashuhuda wameripoti hali ya kuzagaa miili ya watu mitaani na balozi zikisema zaidi ya raia 270 wameuawa katika mapigano hayo baadhi wakisema kuwa maisha katika jiji hilo hayatowezekana tena kama vita hivyo haitofika ukomo.

Kulingana na rekodi za Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, mapigano kati ya jeshi la Sudani na mpinzani wake RFS yaliyofanyika kwa takribani siku tano yamesababisha vifo vya watu 300.

Wanajeshi wa Sudan na wanamgambo wa RSF walikuwa wamekubaliana kusitisha mapigano kwa saa 24 siku ya Jumanne lakini mapatano hayo yalishindikana.
Screenshot_20230420_145136.jpg
 
Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson ameiagiza Serikali kufanya tathimini ya kina ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (Tasaf) ili kuondoa changamoto za muda mrefu ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na wabunge.
Spika ametoa maagizo hayo leo Alhamis Aprili 20, 2023 wakati wa kipindi cha maswali na majibu bungeni baada ya wabunge wengi kulalamikia kuhusu changamoto.

Wabunge hao ni Aida Khenan (Nkasi Kaskazini-Chadema), Husna Sekiboko (Viti Maalum-CCM), Charles Kajege (Mwibara-CCM) na Mwita Waitara (Tarime Vijijini-CCM).

Dk Tulia ametoa agizo kwa Serikali kwa kusema kuwa changamoto za Tasaf zimeshakuwepo kwa muda na kwamba anadhani changamoto hizo zinatakiwa kupungua na si kuongezeka.

Amesema kwa namna ambavyo Serikali imefanya vizuri kwenye mpango huo, inabidi kufanya tathimini ya kina ili changato hizo ziondoke kwasababu wameshafanya kazi hiyo kwa muda mrefu.
Screenshot_20230420_145229.jpg
 
WYDAD KUMKOSA MKALI WAO
.
Habari njema kwa Simba kwamba wapinzani wao, Wydad Casablanca watakosa huduma ya mshambuliaji wao matata, Msenegal Junior Bouly ambaye ana kadi tatu za njano.
.
Kukosekana kwa Junior bila shaka ni habari njema kwa Onyango kwa sababu mshambuliaji huyo ndiye kinara wa mabao wa Wydad. Katika jumla ya mabao 6 iliyofunga katika hatua ya makundi, Junior amefunga mabao matatu peke yake.
.
Wydad ambayo inatumia mfumo wa 4-2-3-1 ni wazi kukosekana kwa Junior kutampa fursa Moutaraj nafasi ya kuanza katika mchezo wa Simba.
Screenshot_20230420_145712.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom