Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,081
- 464,013
Watoto wawili wa Familia moja Anuari Salum (5), Mwanafunzi wa Darasa la Awali Shule ya Msingi Manzese na Nurat Shabani (12) Mwanafunzi wa Darasa la Sita Shule ya Msingi Mazinyungu Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro wamefariki baada ya kugongwa na gari wakati wakiwa pembezoni mwa Barabara wakisubri kuvuka.
Ajali hiyo imetokea eneo la Mazense Kata ya Mkwatani Wilayani Kilosa, Morogoro Barabara ya Kilosa - Dumila ambapo gari dogo lenye namba za usajili T I63 DJH liliacha njia na kuwafuata Watoto hao wakiwa pembezoni mwa Barabara.
Akiongea na @ayotv_ kwa njia ya simu RPC wa Morogoro, Alex Mkama, amesema chanzo cha ajali ni mwendokasi wa Dereva aliyekuwa anaendesha gari hilo, Endishi Christian (41).
Dereva huyo kwa sasa anaendelea kushikiliwa na Polisi na upelelezi utakapokamilika atafikishwa Mahakamani.