Makapuku Forum

YANGA KUOGA MINOTI
.
Achana na yale mamilioni ya Rais wa Tanzania
Samia Suluhu Hassan kwenye kila bao lakini Yanga ikitinga robo fainali itapata mkwanja kutoka CAF.
.
Simba tayari imefika Robo Fainali na kujihakikisha kitita cha Bilioni 1.5 na Kama Yanga ikifika robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika itavuna Dola 350,000 ni Sh 800 milioni.
.
Lakini pia kama Yanga itashindwa kufuzu basi itapata fedha za kumaliza nafasi ya tatu na nne kwenye kundi ambapo kwa Yanga itakuja Dola 275,000 zaidi ya sh 600 milioni za Kibongo.

 
Mechi mbili (2) zilizopita za hatua ya Makundi ambazo Yanga imecheza Uwanja wa Benjamin Mkapa, imefunga magoli matano (5).

️ vs TP Mazembe
️vs Real Bamako

Wananchi wamefungwa goli moja tu wakiwa Uwanja Benjamin Mkapa kwenye mechi za hatua ya Makundi [
️ vs TP Mazembe].

Leo itakuaje vs Monastir_______?
 
Shaffih Dauda

Binafsi hakuna jambo ambalo nalisubiri kwa hamu kama kushuhudia Simba na Yanga zote zikiwa zimefuzu hatua ya mtoano ya mashindano ya CAF!

Simba tayari ipo Robo Fainali ya CAF Champions Legua, tunasubiri kuiona Yanga kwenye hatua ya Robo Fainali ya CAF Confederation Cup. Wananchi wana nafasi nzuri ya kwenda Robo Fainali.

Sikumbuki kama kitu kama hiki kimewahi kutokea, siwezi kusema haijawahi kutokea inawezekana imewahi kutokea lakini binafsi sijawahi kuona Simba na Yanga kwa pamoja zikiwa Robo Fainali ya michuano ya CAF ngazi ya klabu.
 
Shaffih Dauda

Ikitokea Yanga ikashindwa kupata matokeo ya ushindi kwenye mchezo wa leo dhidi ya Monastir, halafu TP Mazembe ikaifunga Real Bamako, basi timu ya kuungana na Monastir itajulikana kwenye mchezo wa mwisho Lubumbashi-DR Congo [TP Mazembe vs Yanga].

Lakini endapo TP Mazembe ikipoteza mechi yake dhidi ya Real Bamako, Yanga itakuwa imefuzu moja kwa moja hata kama ikipata matokeo ya sare mbele ya Monastir.

Yanga wanajua leo ndio Fainali yao ya kufuzu Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF ili mchezo wa mwisho dhidi ya Mazembe kule Lubumbashi iwe ni kukamilisha ratiba tu.
 
Scandal24

FOOTBALL ECONOMY || Respect

.
Mashabiki wa Yanga pamoja na viongozi wenu mjifunze kuheshimu wachezaji wakubwa, ni kweli hakuna mchezaji mkubwa kuzidi timu ila mchezaji mkubwa anaipa thamani timu.
.
Tuache zile kauli ya akitaka ende zake, tuache zile kauli za pengo lake litazibwa, ni kweli litazibwa lakini mnapaswa kumfanya mchezaji ajitoe kwa Heshima ya watu wanaomuheshimu.
.
Mashabiki wa Simba wanamuheshimu Chama, Viongozi na wanachama wanamuheshimu Chama pamoja na wachezaji wengine wakubwa. Mashabiki wa Yanga jifunzeni kuwa na Heshima.
.
Huenda mkashinda mechi, huenda mkachukua vikombe lakini kama hamuwaheshimu wanachezaji ambao ndio wanajeshi siku zote wataondoka vibaya na wala hawatajivunia kuvaa jezi yenu.
.
Sina Mengi, FEI TOTO anastahili HESHIMA.
.
NB:
Simba wametengeneza Mfalme, Yanga wanamdharau Mfalme.
.
 
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeishauri Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kuanza na mfumo wa Barabara zenye tozo katika mradi wa ujenzi wa Barabara njia nane kutoka Kimara Jijini Dar es Salaam hadi Kibaha Mkoa wa Pwani ili kuweza kuongeza mapato.

Ushauri huo umetolewa wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara kutembelea mradi wa Barabara wa njia nane ambapo waliongozana na Viongozi na Watumishi kutoka TANROADS kuona maendeleo ya mradi huo ulipofikia pamoja na kuona changamoto zilizopo, akipngea kwa niaba ya Wajumbe wa Kamati hiyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Selemani Kakoso ametolea mfano ujenzi wa Barabara hizo tangu awali kwamba ungeainisha Barabara moja ya kulipia ambayo ingekuwa ikipatia fedha Serikali na kutumika kwa aili ya ukarabati.

"Wajumbe hapa wameelezea umuhimu wa kuanza na Barabara zenye tozo, Mimi naamini kabisa kama tungekuwa tumejipanga kwa hizi hizi njia nane ni lazima tungekuwa na njia ambazo nyingine ni za kulipia, yaani Barabara za tozo ili tuongeze mapato, Dunini kote Barabara nyingi zinajengwa kwa mfumo huu”

“Sheria inatukataza kujenga Barabara za tozo kama hauna Barabara mbadala lakini hapa kuna njia mbadala kwanini msingelianza na hizi hapa tukawa na Barabara za kulipia?”
 
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la uwepo wa mvua kubwa kesho Jumatano March 22,2023 katika maeneo mengi ya Mikoa ya Lindi na Mtwara.

Athari zinazoweza kujitokeza ni baadhi ya Makazi kujaa maji pamoja na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi “Tafadhali zingatia na ujiandae”
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…