Farhan Jr Kihamu
GODFREY BONNY NDANJE, hisia kali kwenye mchana wa jua kali kabla ya kuanza safari ya kurejea Ifakara stendi ya Makali imenipasa kwanza nishike daftari kwa tahadhali kuandika kuhusu Kiungo huyu hatari, naomba muda tafadhali.
GBN zimebarikiwa zile mvua za Tukuyu, hazikunyesha kustawisha Parachichi pekee bali Mbuyu mmoja kwenye eneo la Kiungo cha mpira, kitovu chako kilifukiwa kwenye ardhi ya Tukuyu Stars na ukawaahidi kuwa legacy will live on na Tukuyu itaishi daima kwenye ramani ya mpira Tanzania.
Ndanje! Ungekuwa hai ningesema Mbula Tukete, lakini haupo tena! Syosa amenye Kyala sina budi kusema! Kyala Nnunu napaswa kuandika, Kiungo mwenye Upara The Pride of Kusini and Nyakyusa land, mikono inatetemeka sioni cha kuandika Ndanje.
Umepumzika sasa kwenye migomba huko Tukuyu lakini kumbukumbu zako zitaishi daima, sijui unacheza mpira huko ulipo basi kutakuwa na mechi bora sana kati yako na Patrick Mafisango, kama kuna maisha mengine huko basi Ndanje endelea kuburudisha kwa hicho kipaji chako.
Wanyakyusa na Wahehe ni Rafiki zangu, wamenilea kwenye ardhi zao! Nawahusudu sana kama navyohusudu kipaji chako, Nkamu pumzika kwa amani, ulishamaliza kazi yako ya namna ya kuwa Kiungo wa mpira mwenye maamuzi magumu na pass za uhakika, umekata sana risiti za Niyonzima na Mafundi wengine.
Miaka imesogea na mvua zinaendelea Tukuyu, naamini kuna siku mbegu nyingine itamea, iwe Msasani, Bagamoyo, Ushirika, KKK, Kiwira au Ntokela ila naamini Bonny mwingine atazaliwa! Pumzika GBN.
Tukuyu will rise again, the Legacy of Nyakyusaland will live on forever japo Madogo zako wanauza Iphone Makumbusho siku hizi🫡
Syosa Amenye Kyala[emoji1317]!