Makapuku Forum

Makapuku Forum

Baada ya mvutano wa miezi zaidi ya miwili kuhusu masuala ya kimkataba kati ya mchezaji Feisal Salum, 'Fei Toto' na klabu ya Yanga, Jumatatu Machi 13, 2023 huenda ikawa mwisho wa sakata lote ambapo kiungo huyo anatarajia kukutana na Rais wa Yanga, Hersi Said na Mfadhili wa timu hiyo, Gharib Said Mohamed 'GSM'.

Kikao hicho kitakachofanywa kwa siri kubwa kitakuwa na ajenda mbili hadi tatu, ambapo ya kwanza ni GSM kutaka kummwagia mkwanja mrefu mchezaji huyo na kuboresha mkataba wake zaidi ya ule wa kwanza ili abaki Yanga.

Pili wataangalia namna ya mchezaji huyo anavyoweza kuvunja mkataba na kuambiwa kiasi gani cha fedha anapaswa kuwalipa Wanajangwani hao ili kuondoka kwa amani.
Screenshot_20230311_051957_OGInsta%2B.jpg
 
Gavana wa Taliban wa jimbo la Balkh kaskazini mwa Afghanistan, Mohammad Dawood Muzammil amekutwa akiwa ameuawa katika ofisi yake iliyopo mji mkuu wa mkoa, wa Mazar-e Sharif.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Msemaji wa Taliban, Zabihullah Mujahid amesema kuwa gavana huyo aliuawa kama shahidi katika mlipuko wa maadui wa Uislamu.

Muzammil alikuwa ameongoza vita dhidi ya IS katika wadhifa wake wa awali kama gavana wa jimbo la mashariki la Nangarhar na ndiye afisa mkuu wa Taliban kuuawa tangu wanamgambo hao warejee madarakani mwaka 2021.

Screenshot_20230311_052048_OGInsta%2B.jpg
 
Mkuu wa upelelezi wa jeshi la Lithuania, Elegijus Paulavicius amesema kuwa rasilimali ilizonazo Urusi zinatosha kuendeleza vita nchini Ukraine kwa kasi ya sasa kwa miaka miwili.

Amesema kuwa muda ambao Urusi itaendeleza vita hiyo itategemea pia na uungwaji mkono wa jeshi lao kutoka mataifa kama vile Iran na Korea Kaskazini.

Paulavicius alitoa kauli hiyo alipokuwa akiwasilisha muhtasari wa tishio la kitaifa na mashirika ya kijasusi ya Lithuania, ambayo pia yalidai wadukuzi wanaohusishwa na serikali ya Urusi na China walijaribu mara kwa mara kuingia katika kompyuta za Serikali yao mwaka 2022.
Screenshot_20230311_052718_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom