Waziri wa Afya Ummy Mwalimu @ummymwalimu amesema tafiti zimebaini kuwa takribani Watanzania 5,800 mpaka 8,500 wanahitaji huduma za kusafisha damu (dialysis) au huduma za kupandikizwa figo.
Waziri Ummy amesema hayo Jijini Dar es Salaam wakati akiongea na Waandishi wa habari akiwa jengo la Wagonjwa wanaosafishwa figo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo amesema hadi kufikia January 31, 2023 Wagonjwa 3,250 walikuwa wanapatiwa huduma ya kusafishwa damu (dialysis) na Wagonjwa 335 wamepandikizwa figo.
“Kati ya waliopandikizwa figo Wagonjwa 103 wamepandikizwa nchini ambapo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imepandikiza wagonjwa 70 na Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma imepandikiza wagonjwa 33”
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Jumanne Muliro Jumanne amekabidhi magari mapya matatu ya usalama barabarani (Pro Box) yaliyonunuliwa na Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Kipolisi wa Temeke kwa thamani ya Tsh. Milioni 48 huku kila gari moja likigharimu Tsh. Milioni 16 ambapo Kampuni ya ASAS @asas_dairies ikiwakilishwa na Faraji Abdi @faraj_asas imechangia zaidi ya Tsh. Milioni 9 katika kuboreshwa kwa magari hayo ikiwemo kuweka rangi za kipolisi, ving’ora, matairi mapya na matengenezo mengine.
Kamanda Muliro amewaonya Askari watakaotumia vibaya magari hayo kuwa wataadhibiwa “Uzito wa makosa ya tuhuma tutakazozipata utakazokuwa ukizifanya wewe Askari Polisi huku ukilitumia gari hili la Polisi ambalo Kamati ya Usalama Barabarani ya Mkoa wa Temeke imeamua kuyanunua galafu wewe ukaenda kufanyia vitu vya ovyo maamuzi ya kitendo ulichokifanya yatalingana na uzito wa udhalilishaji ulioufanya kwenye Jeshi la Polisi lakini pia kwenye udhalilishaji wa usalama barabarani”
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema takwimu zinaonesha idadi ya Wanawake na Vijana hasa Wanawake wanaoshiriki kwenye shughuli zinazohusiana na TEHAMA sio nzuri sana kwa takwimu ambapo amesema idadi ni ndogo ukilinganisha na Wanaume kwa Tanzania, Africa na Kidunia.
Akiongea baada ya kufungua Kongamano la Wanawake wa Tanzania Katika TEHAMA (Tanzania Women and Technology Conference) @techwomentz lililoandaliwa na @LpdigitalTz chini ya CarolNdosi Jijini Dar es salaam, Nape amesema “Kwa takwimu na hasa hapa Tanzania zaisi ya 51% ya population ya Tanzania ni Wanawake kwahiyo wasiposhiriki vya kutosha maana yake jamii kubwa ya Watanzanja itakuwa haijashiriki, Waathirika wakubwa wa unyanyasaji mtandaoni ni Wanawake na tunadhani kama Serikali tunawajibu wakuchukua hatua kali”
Ubalozi wa Tanzania Nchini China umesema Kampuni ya Kichina inayotengeneza Mabasi ya Yutong inatarajia kufungua Karakana yake jijini Dar es salaam ili kutoa huduma kwa ufanisi kwa Wateja wao.
Taarifa hii imetolewa leo Jijini Beijing katika mkutano wa Balozi Mbelwa Kairuki na Afisa Mtendaji Mkuu wa Yutong Africa ambapo Karakana hii itakuwa na ukubwa wa kuwahudumia Wateja wenye mabasi ya Yutong katika nchi za Afrika Mashariki.
Baadhi ya mitambo ya kampuni binafsi ya kufua umeme (IPTL) inadaiwa kuibiwa na watu wanne akiwemo askari Polisi aliyekuwepo lindo siku ya tukio.
Mitambo hiyo iliyopo Tegeta jijini Dar es Salaam, ilisitishwa kutoa huduma ya kuzalisha umeme kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) mwaka 2013 baada ya kutoelewana kwa wahusika wa mkataba wa makubaliano.
Kulingana na taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii, watuhumiwa wa tukio hilo wanashikiliwa na Polisi katika Kituo cha Oysterbay jijini Dar es Salam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amethibitisha tukio hilo.
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limetaja sababu ya kuwaondoa kazini waliokuwa wafanyakazi wake katika kitengo cha uhakiki wa shehena ni marekebisho ya sheria.
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Julai 2022 lilifanya marekebisho ya sheria ya uwakala wa meli ambayo ilifuta baadhi ya majukumu ya Tasac na kwenda kwenye sekta binafsi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Ijumaa Machi 10,2023 jijini Dodoma, Mkurugenzi Mkuu wa Tasac, Kaimu Mkeyenge amesema kumekuwa na malalamiko katika mitandao ya kijamii kwamba waliokuwa zaidi wafanyakazi 400 wa shirika hilo mikataba yao ilivunjwa bila ya kufuata utaratibu wa kisheria ikiwa umebaki muda wa mwaka mmoja.
Amesema kufuatia mabadiliko hayo Agosti 11, 2022 Tasac ililazimika kuvunja mikataba ya kazi wa vitendo kwa jumla ya vijana 290 waliokuwa wakifanya kazi ya uhakiki wa shehena na sio zaidi ya 400 kama ilivyoripotiwa.
China imeweka rekodi mpya duniani kwa kuunda meli kubwa yenye uwezo wa kubeba makontena 24,116 pamoja na mizigo ya tani zaidi ya 240,000.
Taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya Gazeti la Umma la nchini humo leo Machi 10, 2023 kupitia mtandao wa ‘swahili people’, imeeleza kwamba kukamilika uundaji wa meli hiyo huko Shanghai, China, ni rekodi mpya ukilinganisha na meli iliyoundwa mwaka jana yenye uwezo wa kubeba makontena 24,000.
Kampuni tanzu ya Shirika la Uundaji Meli la China imesema tayari kazi ya uundaji imekamilika kwenye kituo cha uundaji wa meli cha Changxing cha Shirika la Uundaji Meli la China.
“Hii ni meli kubwa zaidi iliyoundwa na kukamilika duniani, ambayo imevunja rekodi ya “Meli ya Changyi” iliyokamilika Mwezi Juni, Mwaka 2022 yenye uwezo wa kubeba makontena 24,000,” imenukuliwa sehemu ya taarifa hiyo.
Majerehi 40 kati ya 44 waliokuwa wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Geita kufuatia ajali ya basi iliyotokea katika eneo la Ibandakona Kata ya Kasamwa wilayani Geita wameruhusiwa kutoka hospitalini baada ya hali zao kutengemaa.
Ajali hiyo ilitokea Machi 7,2023 na kusababisha vifo vya watu 10 na majeruhi 48, wanne kati yao walipewa rufaa na kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Bungando kwa matibabu zaidi.
Akizungumzia hali ya majeruhi waliobaki wodini Kaimu Mganga mfawidhi wa Hospitali hiyo Pasclates Ijumba amesema hadi mchana wa leo wamebaki majeruhi wanne na hali zao zinaendelea vizuri.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.