Makapuku Forum

MARTINEZ NDO BASI UBELGIJI
.
Kocha wa timu ya taifa ya Ubelgiji
aliyeinoa kwa muda mrefu, Roberto Martinez, ameachia ngazi baada ya kutolewa kwenye fainali za Kombe la Dunia zinazoendelea huko Qatar, huku ikielezwa ubovu wa kikosi na masupastaa kutojituma vikitajwa kumwangusha.
.
Martinez alithibitisha mchezo dhidi ya Croatia waliotoka suluhu kuwa ulikuwa mwisho kwake kukalia kiti cha ukocha. Martinez alisema kuondolewa mapema katika michuano hiyo lilikuwa pigo kubwa kwake na Wabelgiji kwani wameshindwa kutinga raundi ya 16 bora na kuzua gumzo Kubwa.
 
MASIKINI NEYMAR! SASA KUONDOLEWA KIKOSINI
.
Taarifa zimeripoti kuwa Neymar JR
huenda akaondolewa kwenye fainali ya Kombe la Dunia zinazoendelea kutokana na majeraha yanayomsumbua kwani hajapata nafuu kama ilivyotarajiwa.
.
Mchezaji huyo aliondolewa kwenye mechi ya ufunguzi Brazil ilipocheza dhidi ya Serbia baada ya kuumia kifundo cha mguu, ingawa madaktari wa Brazil walisema atakuwa nje ya uwanja hadi mechi za hatua ya makundi zitakapomalizika.
.
Lakini sasa taarifa zinadai huenda Neymar akaondolewa kikosini baada ya vipimo vya madaktari kutoka vikionyesha kwamba jeraha la staa huyo ni kubwa na hatakuwa fiti kuendelea na michuano hiyo.
 
Binamu nimekumiss mnoooo
ila hiyo ya kunicheck mburahati kiukweli nimecheka sanaaaa ebu fanya ukujee tu tatizo binamu yangu siasani kunakuweka busy sanaaaa
Sa' binamu unacheka nini?! Au ume-mind nimetoa siri kwamba tulikuwa tuna-meet sana Mburahati getoni kwako?!

Ujue nitaandika tena kwa herufi kubwa, and bolded ili kama kuna kivulana chako hapa, basi kipate ujumbe kwamba huwa tunakutana!

My intention is clear... natamani uachike ili uwe wangu peke yangu, binamu! Matakwa ya aunt angu na uncle ako LAZIMA yaheshimiwe.
 
Binamu niache bwana mburahati si ndio kwetu unataka niachike ili iweje tena jamani
 
Binamu niache bwana mburahati si ndio kwetu unataka niachike ili iweje tena jamani
Kumbe ukiachika, binamu yako si ndo napata fursa ya kuteleza na ganda la ndizi!! Mambo yakiwa magumu, jungu lililojaa fitina linaloruhisiwa kupika mtafaruku! Btw, sa' wewe hofu yako nini hata ukiachika?!
 
Kumbe ukiachika, binamu yako si ndo napata fursa ya kuteleza na ganda la ndizi!! Mambo yakiwa magumu, jungu lililojaa fitina linaloruhisiwa kupika mtafaruku! Btw, sa' wewe hofu yako nini hata ukiachika?!
Hofu naipata wapi hata nikiachika na binamu yangu yupo kwa ajili yangu tu
 
Afya ya Gwiji wa soka duniani Pele, inatajwa kuwa katika hali mbaya na hakuna matibabu yoyote ya mionzi ambayo yanaweza kumfanya awe sawa, huku taarifa zikiripoti kuwa amewekwa kwenye uangalizi maalum wa kupunguza maumivu na asipate changamoto ya pumzi kwa wakati huu ila hakuna tiba ambayo inaweza kutatua changamoto yake.

Prayers for the King of football
 
Nyota wa Brazil
Gabriel Jesus atazikosa mechi zilizosalia za Brazil kwenye kombe la dunia kutokana na majeraha huku pia Alex Telles nae anatarajiwa kuikosa pia michuano yote.
 
Nyota wa Ghana, Andre Ayew alielekea moja kwa moja hospital baada ya mechi jana kwakuwa Mtoto wake alizimia baada tu ya yeye kukosa penati na bahati nzuri alipatiwa matibabu na amerejea vyema.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…