Makapuku Forum

“Tumeongea nao wachezaji na uzuri wanajua Mashabiki wanahitaji nini kutoka kwako, muhimu kwa Mashabiki ni kuwa na subra tu” Juma Mgunda, Kocha wa muda Simba SC.
 
TUCHEL AKUNJA PAUNI 13 MILIONI CHELSEA
.
Thomas Tuchel ameripotiwa kuweka kibindoni mkwanja mrefu, Pauni 13 milioni (Sh 35 Bilioni) kama fidia ya kufutwa kazi Chelsea.
.
Tuchel, 49, alitupiwa virago huko Stamford Bridge na bosi mpya bilionea Todd Boehly baada ya timu hiyo kuanza msimu huu vibaya. Bilionea Boehly ni kama amefuata tu nyayo za mmiliki wa zamani wa The Blues, Roman Abramovich ambaye alikuwa akiwafungulia mageti ya kutokea makocha wake.
.
Ripoti zinafichua kwamba Tuchel kwa kuondolewa kazi jambo hilo litamfanya alipwe Pauni 13 milioni, huku benchi lake la ufundi wakilipwa Pauni 2 milioni.

…………..
 
REKODI YA BIG BULLETS KIMATAIFA
.
Nyasa Big Bullets
Msimu uliopita iling’olewa hatua ya awali na Amazulu ya Afrika Kusini
kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya awali kushinda ugenini bao 1-0 kabla ya kulala 3-1 nyumbani.
.
Msimu wa 2019-2020 ilitolewa na FC Platimun ya Zimbabwe
na msimu wa 2018-2019 ilitolewa kwa penalti 4-3 na Gor Mahia ya Kenya
baada ya sare ya 1-1 mechi zote.
 
AKPAN KUIKOSA BIG BULLETS
.
Kiungo Mnigeria Victor Akpan ameachwa jijini Dar es Salaam huku wenzake 24 wakitua salama mjini Lilongwe tayari kupigania timu kwenye mechi ya kwanza ya raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayopigwa kesho Jumamosi.
.
Bado haijajulikana sababu ya Akpan kuachwa Dar.


……………………
 
TANZANIA
itasimama kwa dakika 90 kushuhudia wawakilishi watatu katika Ligi ya Mabingwa Afrika, SIMBA, YANGA na KMKM leo wakitupa karata zao za kwanza katika raundi ya kwanza ya mashindano hayo jioni hii na usiku.
.
Lengo ni moja tu ushindi wa idadi kubwa ya mabao ili kukamilisha hesabu mapema
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…