Makapuku Forum

Jemedari Said

KOCHA NASREDDINE NABI KAMA MGUNDA TU..!!!
Taarifa za uhakika zinasema Kocha NASREDDINE MOHAMED NABI naye anasubiri ruhusa (Approval) ya CAF kumuwezesha kukaa kwenye benchi hapo kesho kwenye mchezo wa Champions League.

Nabi ambaye msimu uliopita alikaa benchi kwenye mechi 2 dhidi ya Rivers United ana vyeti vya UEFA 'A' na UEFA-Pro alizosomea Belgium, lakini taarifa zake zilichelewa kupelekwa CAF.

Taarifa zinasema aliyekua Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga SC THABIT KANDORO wakati anaondolewa kwenye nafasi yake kumpisha SAAD KAWEMBA alikuwa anafanya usajili wa wachezaji na Viongozi wa benchi la ufundi.

Akiwa ameshamaliza wachezaji 7 kuwaingiza kwenye mfumo wa usajiri akakumbana na andiko la kuachishwa kazi, akamalizia wachezaji ila benchi la ufundi alikua bado hajaanza kabisa.

Kwahiyo waliochukua badala yake ni kama walipitiwa wakiamini kilakitu kiko sawa wakaja kukumbushwa na ujumbe kutoka CAF juu ya taarifa za kocha wao.

Habari zaidi zinasema taarifa zake (vyeti) zimeshawasilishwa CAF na wanasubiri Shirikisho hilo la Soka Afrika kuidhinisha tu ili akae benchini kesho.

Hali hii ni kama ambayo inamkuta Kocha Mkuu wa Simba SC JUMA MGUNDA ambaye nayeye anasubiria idhini ya CAF ili kesho akae benchini pale jijini Lilongwe kwenye mchezo dhidi ya Nyasa Big Bullets. Mgunda yeye amechlewa kuidhinishwa kwakuwa vyeti vyake vimechelewa kuwasilishwa kwakuwa ni kocha mpya.

BIN KAZUMARI (The voice of the voiceless)
 
HENRY ACHEKA KISA SPURS ITAKUWA BINGWA
.
ANACHEEEKA! Staa, Thierry Henry ameshindwa kujizuia na kuangua kicheko baada ya Clint Dempsey kusema Tottenham Hotspur itashinda ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.
.
Henry, Dempsey na Jamie Carragher waliulizwa wachague timu zao ambazo wanadhani zitashinda ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.
.
Carragher aliichagua Manchester City kama ambayo alivyofanya Henry, lakini Dempsey chaguo lake liliwachekesha wengi, aliposema:
.
“Nitakuwa tofauti kidogo, nitachagua timu isiyofikiriwa kabisa kama inaweza kutwaa ubingwa. Bingwa inaweza kuwa Tottenhma.” Maneno hayo yalimfanya Henry na Carragher kuangua vicheko na Henry kusema: “Acha niondoke.”
 
Hapa ndiyo anafanane na Mwanae Harry mno...
 
Thierry Henry 14 kichogo, alinioonza kuipenda arsenal
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…