Yaan tuoge J3, j5 na alhamis 🤣🤣
👏 👏Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi amempongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Salvatory Mabeyo kwa kutekeleza vema majukumu yake katika kipindi chake chote cha utumishi ndani ya Jeshi hilo.
Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo alipozungumza na Jenerali Mabeyo ambaye alifika Ikulu Zanzibar kumuaga Rais kufuatia kumaliza muda wa utumishi wake ndani ya Jeshi mwisho wa mwezi wa sita kwa mujibu wa sheria.
Rais Dkt. Mwinyi amemtakia kila la heri Mabeyo katika maisha yake ya kustaafu hasa ikikumbukwa amelitumikia kwa mrefu Jeshi hilo na kufanya mambo mengi yatakayoacha alama.
Kwa upande wake Jenerali Mabeyo amesema Jeshi la Ulinzi Tanzania litaendelea kumkumbuka Rais Dk. Mwinyi kwa busara na hekima zake katika kuzishughulikia changamoto mbalimbali ndani ya Jeshi hilo ambalo hatimae limepata mafanikio makubwa.View attachment 2252751View attachment 2252752
Blues 💙Dembele Kutua Darajani
.
Chelsea ndio inaongoza kwenye harakati za kuiwania saini ya staa wa Barcelona na UfaransaOusmane Dembele, 25, kuelekea dirisha lijalo la majira ya kiangazi.
.
Dembele mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwisho wa mwezi huu na hadi sasa hakuna muafaka uliofikiwa kati yake na mabosi wa Barca juu ya kumuongeza mkataba mpya.View attachment 2252753
Heri tu 🤣🤣DE GEA KUMVUA UNAHODHA MAGUIRE
.
David de Gea amependekezwa kuwa nahodha mpya wa Manchester United msimu mpya utakapoanza chini ya kocha Erik ten Hag.
.
Kwa mujibu wa taarifa Ten Hag atawapa nafasi wachezaji kuchagua nahodha mpya baada ya kurejea Carrington mwishoni mwa mwezi huu.
.
Hiyo ni taarifa mbaya kwa Maguire ambaye amekuwa na wakati mgumu tangu alipovalishwa kitambaa cha unahodha huku mashabiki wa timu hiyo wakimponda kutokana na kiwango chake kibovu.View attachment 2252754
Binti ndio unaamka au umeshtuka unarudi tenaYaan tuoge J3, j5 na alhamis![]()
Mfyuuuu yaani huipendi team yetuHeri tu![]()
Yaan hapa ndiyo Kumekucha mazima…Binti ndio unaamka au umeshtuka unarudi tena
HapanaMfyuuuu yaani huipendi team yetu
Hahahaah yaani me ikifika tu saa kumi na moja kasoro kama nipo kitandani lazima tu niwe macho sijui sababu mwili umeshazoea kuamka alfajiriYaan hapa ndiyo Kumekucha mazima…
Mwili unazoea nahisi, unakuwa uhitaji hata alarm.Hahahaah yaani me ikifika tu saa kumi na moja kasoro kama nipo kitandani lazima tu niwe macho sijui sababu mwili umeshazoea kuamka alfajiri
Kweli aiseeMwili unazoea nahisi, unakuwa uhitaji hata alarm.
Unashtuka tu ushaamka, na hakuna aliyekuamsha.