Farhan Jr
Kuna binadamu anaitwa Luís Filipe Hipólito Reis Pedrosa Campos ama Luis Campos napenda kumuita jina lake maarufu la The Wizard of the capital gain, huyu ndie aliepika ile Monaco dume
Yes alihakikisha Monaco inatumia pesa ndogo sana ya usajili kisha kwenda kufanya makubwa Ulaya, akahama baadae na kwenda Lille akasuka mfumo ule ule ukaipa ubingwa wa Ufaransa mbele ya PSG, Campos mtu hatari Director of football
Lakini niliwahi kumsikia kwenye interview yake moja aliwahi kusema changamoto kubwa anayopitia ni kitu kinaitwa familia ya mpira, kuna watu wapo kwenye mpira na wanaishi dunia yao kama kisiwa, hawapendi mabadiliko
Kuna watu ukigusa maslahi yao wanageuza nyeupe kuwa nyekundu, Campos aliwahi kusema ilifika muda walitamani afeli ili wazungumze namna hawawezi kutoboa kisa mfumo wake wa utawala, lakini haikuwa hivyo
Kuna muda napenda kumnukuu Fergie aliwahi kusema “One thing about football is not about football” ndio kitu kimoja kuhusu mpira huwa hakihusu mpira wenyewe
Kitu kimoja kuhusu Simba kutofanya vizuri hakihusu Simba, kitu kimoja kuhusu yote yanayotokea hivi sasa wala hayahusu mpira, niamini Mimi, ni matokeo ya kimfumo!
“One thing about football is not about football” Sir Alex Ferguson
“Kitu kimoja kuhusu mpira ni kama kisiwa kuna watu wana nchi yao na maisha yao” Luis Campos