Makapuku Forum

Makapuku Forum


1652978718285.jpeg

....happy almost Furahiday dear MF, tuwe na an easy one​
 
Rais Samia leo anashiriki mkutano wa hadhara Mkoani Tabora ambapo kupitia hotuba yake amesema "Kuna kauli iliyotolewa na Rais Mpendwa wetu Dr. John Pombe Magufuli kwamba zaidi ya Tani moja ya mazao yanapoasafirishwa yasitozwe tozo, tozo ziende kwenye mazao yanayozidi Tani moja, hiyo ilikuwa ni kauli ya Rais na Rais hajafuta hiyo kauli kwahiyo jambo hilo linasimama kama lilivyo chini ya Tani moja hakuna kutoa tozo, zaidi ya Tani moja tozo zitolewe kama kawaida"

"Naomba Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi msimamie haya kwasababu inawezekana kabisa Migambo wenu huko wanakwenda kutoza tozo hakuna risiti wala mapato hayaingii kwenye maeneo yenu naomba mkayasimamie hayo"

"Waliosimama hapa wote ni Mawaziri Vijana wenye kasi katika kufanya kazi yao niwatie moyo Mawaziri wangu ambao mko hapa Bashe, Bashungwa, Mbarawa Aweso, Makamba na wengine ambao hawapo hapa akina Mwigulu na wengine wote chapeni kazi kwa maendeleo ya Nchi"

"Kunaweza kukawa kuna maneno mengi sana lakini hampati maneno kama ninayoyapata Mimi Kiongozi wenu lakini hayanivunji moyo najenga Nchi nanyi nataka mjenge Nchi chapeni kazi Vijana wangu kwa maendeleo ya Nchi"
Screenshot_20220520-032536_OGInsta%2B.jpg
 
Rais Samia leo anashiriki mkutano wa hadhara Mkoani Tabora ambapo miongoni mwa waliosimama kuzungumza mbele yake ni Mbunge wa Nzega Vijijini, Dr. Hamis Kigwangalla.

Kigwangalla amesema "Rais nikupongeze sana kwa jitihada zako za kurekebisha mifumo ya utawala bora nchini, katika kipindi kilichopita Mh. Rais tulipata tabu ya Wawekezaji kukimbia Nchi yetu na wengine kuondoa mitaji yao"

"Kwa sasa ukilinganisha na kipindi cha mwaka mmoja uliopita ukilinganisha na kipindi hiki ambacho umetumikia kama Rais tumeshuhudia kukua kwa mitaji ya uwekezaji kutoka nje ya Nchi kuingia Tanzania kwa zaidi ya mara 6 kutoka Trilioni 1 kipindi cha kabla wewe hujawa Rais mpaka kufikia kiwango cha Trilioni 7 katika kipindi hiki ambacho wewe umeliongoza Taifa hili"
Screenshot_20220520-032725_OGInsta%2B.jpg
 
Rais Samia leo anashiriki mkutano wa hadhara Mkoani Tabora ambapo miongoni mwa waliosimama kuzungumza mbele yake ni Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba.

Lipumba amesema "Mh. Rais Samia Hotuba yako uliyoitoa Bungeni ilitupa matumaini makubwa ya maendeleo kwa upana wake ukasema hii hii Nchi ni yetu sote hakuna mwenye hati miliki ya Nch hii na ukasisitiza demokrasi ni nyenzo ya kuleta maendeleo, ni matumaini yetu katika kipindi chako suala la ujenzi wa demokrasia litaendelea kwa kasi inayostahiki"

"Tunakushukuru umekutana na Vyama vya Siasa mara mbili kwenye mkutano lakini pia tunatoa wito kwa Viongozi ngazi za Mkoa na Wilaya kukutana na Viongozi wa siasa na kuwasikiliza tujenge utamaduni wa siasa za kistaarabu na za kujenga hoja"

"Ombi langu ni kwamba katika uchaguzi unaokuja wa 2025 tusirejee kwenye kile ambacho Rais Kikwete alikiita Tsunami ya 2020, tufanye uchaguzi ulio huru na wa haki na kwa kazi kubwa unayofanya ya kuleta maendeleo naamini ukishiriki uchaguzi wa 2025 ukawa huru na wa haki una nafasi nzuri tu ya kuweza kushinda uchaguzi"

"Mh. Rais Mimi nakuomba ujiwekee lengo usilitangaze ila ujiweke lengo la kushinda Tuzo ya Mo Ibrahim ya kuiongoza Nchi kwa utawala bora, kujenga demokrasia kuheshimu haki za Binadamu na kujenga uchumi unaoongeza ajira na kuwaondoa Wananchi kwenye umasikini"
Screenshot_20220520-032816_OGInsta%2B.jpg
 
Waziri wa Ulinzi Dr. Stergomena Tax leo Bungeni Dodoma amesema hali ya usalama wa mpaka kati ya Msumbiji na Tanzania ni ya wastani kutokana na mashambulizi yanayofanywa na kundi la kigaidi la Ansar Al Sunna Wal Jamaah (AASWJ) maeneo ya Kaskazini mwa Msumbiji, katika Jimbo la Cabo Delgado linalopakana na Mkoa wa Mtwara.

"Kundi hilo limekuwa likiathiri usalama kwa kuharibu na kupora mali za Wananchi, katika kupambana na changamoto hii, JWTZ imeendelea kuimarisha ulinzi kwa kufanya operesheni za ndani ya nchi na kukabiliana na kundi hilo"

"Aidha, JWTZ inashiriki operesheni chini ya Mwamvuli wa SADC nchini Msumbiji katika jitihada za kudhibiti ugaidi, operesheni hizi zimeendelea kuimarisha ulinzi katika eneo la Mpaka, kudumisha amani na utulivu, operesheni zimesaidia kupunguza nguvu ya kundi hilo la kigaidi"

"Hata hivyo, kundi hilo linatekeleza mashambulizi kwa kuhamahama na kubadili mbinu za kimapigano licha ya hali hiyo, vikundi vyetu vinaendelea kupambana kuhakikisha kundi hilo halileti madhara zaidi"
Screenshot_20220520-032913_OGInsta%2B.jpg
 
Dosari katika mfumo wa elimu nchini, zimetajwa kuchangia watoto kushindwa kubadilika kulingana na mazingira, badala yake wanaishi na matarajio makubwa bila kujua namna ya kuyafikia.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Shule za Msingi za Paradise Mission iliyopo mkoani Mbeya na Patrick Mission ya Dar es Salaam, Ndele Mwaselela wakati akizungumza na Mwananchi katika mahojiano maalumu, Alhamisi ya Mei 19, 2022.
Screenshot_20220520-033116_OGInsta%2B.jpg
 
Benki ya NMB imefungua rasmi dirisha la kupokea maombi ya ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa sekondari na vyuo vikuu kupitia ‘NMB Nuru Yangu Scholarship and Mentorship Program’

Mkurugenzi wa Bodi ya NMB Fiundation, Ruth Zaipuna amesema ufadhili huu unawalenga wanafunzi waliofanya vizuri na wanaotoka kwenye familia zenye changamoto ambao watapata ufadhili wa kusomeshwa bure kwa mwaka 2022/2023 - ikiwemo kulipiwa gharama za ada, vitendea kazi na nauli.

Jumla ya wanafunzi 200 watanufaika na programu hii, ambapo 50 watakua wa masomo ya shahada (undergraduate) na 150 wa kidato cha tano na sita (A-level).

Programu hii inatekelezwa chini ya NMB foundation
Screenshot_20220520-033210_OGInsta%2B.jpg
 
Balozi wa Tanzania nchini Kuwait, Said Mussa akiwasilisha hati za utambulisho kwa Naibu Amiri na Mwanamfalme wa Kuwait, Sheikh Mishal Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah jijini Kuwait.
Screenshot_20220520-033336_OGInsta%2B.jpg
 
DEUSTCHER MAESTRO, THE GERMANY MAESTRO

Mashabiki wa Chelsea walimpa heshima leo hii Kocha wao Thomas Tuchel, chini yake wametwaa;

UEFA CHAMPIONS LEAGUE
UEFA SUPERCUP
CLUB WORLD CUP
Screenshot_20220520-035700_OGInsta%2B.jpg
 
ZAWADI MAUYA IS GREEN AND YELLOW FOR TWO MORE YEARS 🟡🟢

Klabu ya Yanga imefikia makubaliano ya kuongeza mkataba na Kiungo wake Zawadi Mauya kwa kandarasi ya miaka miwili mpaka 2023/24
Screenshot_20220520-035805_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom