Makapuku Forum

Makapuku Forum

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametoa hotuba Bungeni leo kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara ya Afya 2022/2023 ambapo amesema "Katika kipindi cha July 2021 - Machi, 2022, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imehudumia Wagonjwa 367,213, kati ya hao, wa nje (OPD) walikuwa 328,938 na wa kulazwa (IPD) 38,275, Wagonjwa wa misamaha walikuwa 46,591 ambao waliigharimu Hospitali Tsh. Bilioni 14.1"

"Katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022, Hospitali imetoa huduma ya upandikizaji figo kwa Wagonjwa 6 ambapo gharama ya huduma hiyo ni Tsh. Milioni 30 kwa mmoja ambapo huduma hiyo hugharimu Tsh. milioni 120 nchini India, waliopandikizwa figo tangu huduma hiyo ilipoanzishwa nchini mwaka 2017, wamefikia 70, hivyo Wagonjwa 70 waliopata huduma hii Muhimbili wangegharimu Tsh. 8,400,000,000 iwapo wangepata huduma hiyo India, kwa kuanzisha huduma hii nchini Serikali imeokoa Tsh. 6,300,000,000"

"Katika kipindi cha Julai 2021 mpaka Machi, 2022, Hospitali imetoa huduma ya upandikizaji vifaa vya usikivu kwa Watoto 14 ambapo gharama ya huduma hiyo ni Tsh. Milioni 36 kwa Mgonjwa mmoja ambapo huduma hiyo hugharimu Tsh. Milioni 100 nchini India, Wagonjwa waliopandikizwa vifaa vya usikivu tangu huduma ilipoanzishwa nchini 2017, wamefikia 49 kwa gharama ya Tsh. Bilioni 1.764, hivyo Watoto 49 waliopata huduma hii Muhimbili wangegharimu Tsh. bilioni 4.9 Kwa kuanzisha huduma hii hapa nchini Serikali imeokoa jumla ya shilingi bilioni 3.136"
Screenshot_20220516-182026_OGInsta%2B.jpg
 
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametoa hotuba Bungeni leo kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara ya Afya 2022/2023 ambapo amesema "Wizara imeendelea kuboresha afua mbalimbali ambazo zinahamasisha Wananchi kwenda kupima na kutambua hali zao za maambukizi ya VVU/UKIMWI, ili waweze kupatiwa huduma za ushauri, upimaji, matunzo na huduma za dawa kwa haraka pale inapoonekana kuwa wameambukizwa"

"Hadi kufikia Desemba 2021 Jumla ya Wateja 1,519,013 sawa na 84.6% ya Watu 1,795,905 wanaokadiriwa kuishi na Virusi vya UKIMWI nchini walikuwa wanatambua hali zao za maambukizi "

"Kati yao, Wateja 1,507,686 sawa na 99.3% walikuwa wameanza kutumia dawa za kufubaza Virusi vya UKIMWI, aidha hadi sasa 95.8% ya Wateja waliokuwa wanatumia dawa za ARV nchini walikuwa wamefubaza wingi wa Virusi vya UKIMWI"

"Hadi kufikia mwezi Machi, 2022 idadi ya vituo vinavyotoa huduma ya Tiba ya UKIMWI (CTC) vimefikia 6,759 kutoka vituo 5,555 mwaka 2015 na kati ya hivyo CTC kamili ni 3,075 na vituo vya huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto (RCHS) vinavyotoa huduma ya kutoa dawa ya kufubaza Virusi vya UKIMWI vipo 3,684, Wizara ilisaini mwongozo wa utekelezaji wa utoaji dawa kinga na kuanza kwa huduma hiyo, ambapo hadi sasa jumla ya walengwa 13,285 walianza huduma hiyo katika Mikoa yote nchini"
Screenshot_20220516-182119_OGInsta%2B.jpg
 
Serikali ya Finland imetangaza kuwa itawasilisha ombi la kujiunga na muungano wa kujihami wa NATO baada ya Chama tawala nchini humo kuunga mkono hatua hiyo, Bunge la Finland linatarajiwa kuunga mkono uamuzi huo katika siku chache zijazo.

Uamuzi huu unakuja wakati ambapo Urusi inaivamia Ukraine na inaonesha mabadiliko makubwa katika msimamo wake wa muda mrefu wa kutoegemea upande wowote.

Rais wa Finland Sauli Niinisto amesema anakubaliana na Serikali na kwamba atashauriana na Bunge kabla ya kutangaza uamuzi huo.

Wakati wa mkutano wa pamoja na Wanahabari akiwa na Waziri Mkuu Sanna Marin, Niinisto ameitaja siku hii kuwa ya kihistoria na kusema enzi mpya inafunguka, Chama cha Kisoshalisti cha Sweden pia kinatarajiwa kuunga mkono uamuzi huo wa kujiunga na NATO.
Screenshot_20220516-182217_OGInsta%2B.jpg
 
Rais wa zamani wa Somalia aliyeshindwa katika uchaguzi wa 2017 amerejea madarakani baada ya kumpiku Rais wa sasa, katika kinyang'anyiro cha muda mrefu kilichoamuliwa na Wabunge katika duru ya tatu ya upigaji kura.

Hassan Sheikh Mohamud, aliyehudumu kama Rais wa Somalia kati ya mwaka wa 2012 na 2017, ameshinda uchaguzi huo katika mji mkuu Mogadishu, wakati kukiwa ulinzi mkali uliowekwa na mamlaka ili kuzuia mashambulizi makali ya Wanamgambo wa itikadi kali.

"Linapokuja suala la chuki za aina yoyote, niko tayari kuzitatua, kama tu nilivyosema wakati natangaza kugombea Urais mwanzoni mwa wiki hii, hakuna kisasi wala ufuatiliaji wa kisiasa unaomlenga Mtu yeyote, Nchi hii ina kanuni na sheria za kutosha na kama tofauti zozote zikitokea, tutapitia sheria zilizotungwa na nchi hii"

Amesema ushindi huo ni wa Watu wa Somalia na huo ni mwanzo wa enzi ya umoja, demokrasia ya Somalia na mwanzo wa vita dhidi ya rushwa na kusema anaona kazi ngumu mbele baada ya kushinda Urais.

Duru ya kwanza ya upigaji kura ilikuwa na Wagombea 36, ambapo wane walisonga hadi duru ya pili baada ya kukosekana Mshindi aliyepata angalau theluthi mbili ya kura 328, upigaji kura kisha ukaingia katika duru ya tatu ambapo ushindi wa zaidi ya nusu ya kura ulitosha kumchagua Mshindi.
Screenshot_20220516-182310_OGInsta%2B.jpg
 
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kuwa kama kuna mtendaji anadhani kuwa kutakuwa na upigaji kwenye fedha za umma katika Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, basi anajidanganya.

Kimesema kuwa fedha zinazotolewa na Serikali ni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwa ni kutekeleza ahadi zilizotolewa na chama hicho katika kuwaletea Watanzania maisha bora.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatatu, Mei 16, 2022 na Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka ambaye amesema wabadhirifu wa fedha na mali za umma watashughuliwa mchana.

Shaka ametoa kauli hiyo baada ya kukagua miradi ya maendeleo mkoani Manyara anakoendelea na ziara ya kukagua uhai wa chama hicho.

“Nataka kuwaambia kuwa wanaodhani kuna mlango wa upigaji wa fedha za umma katika Serikali ya Mama Samia basi hayo ni mawazo potofu na dhaifu sana. Serikali iko makini muda wote na inafuatilia mienendo ya mapato na matumizi ya fedha zake. Rais Samia ameteua wasaidizi ambao moja ya majukumu yao ya msingi ni kuhakikisha wanaishi na kufanyia kazi maono yake ambayo ni kuijenga nchi,” amesema Shaka
Screenshot_20220516-182420_OGInsta%2B.jpg
 
Rais Samia Suluhu Hassan amepiga simu na kuzungumza na Wamachinga ambapo ameahidi kutoa Sh10 kwa ajili ya uendeshaji wa ofisi za wamachinga katika mikoa.

Rais Samia alipiga simu hiyo leo Mei 16,2022 kupitia kwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Makundi Maalum, Dorothy Gwajima wakati wa mkutano wa mafunzo kwa viongozi wa Shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania (Shiuma) kutoka mikoa yote Tanzania uliofanyika jijini Dodoma.

Mkuu huyo wa nchi amepiga simu baada ya Naibu Katibu Mkuu wa Shiuma, Josephu Mwanakijiji kueleza changamoto ambazo wamekuwa wakikutana nazo huku simu hiyo ikiibua shangwe kwa machinga wote waliokuwepo ukumbini.
Screenshot_20220516-182524_OGInsta%2B.jpg
 
Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Odinga amemteua Martha Karua kuwa mgombea mwenza wa urais na kumfanya mwanasiasa huyo mkongwe kuwa mwanamke wa kwanza kuwania nafasi hiyo kwa tiketi ya chama kikuu cha siasa.

Karua, aliyekuwa Waziri wa Sheria, anatoka eneo la kati ambalo lina idadi kubwa zaidi ya wapiga kura waliosajiliwa nchini Kenya.

Iwapo atachaguliwa mwezi Agosti mwanasiasa huyo mkongwe atakuwa naibu wa rais wa kwanza mwanamke wa Kenya.
Screenshot_20220516-182701_OGInsta%2B.jpg
Screenshot_20220516-182716_OGInsta%2B.jpg
 
Valerian Massawe (36) kutoka Kiluvya, Pwani ameandika historia ya kuibuka mshindi wa zawadi ya kitita cha fedha Sh1.2 bilioni kutoka Kampuni ya michezo na burudani ya SportPesa baada ya kutabiri kwa usahihi mechi 13 za Jackpot ya wiki iliyopita ya Kampuni hiyo.

Massawe ambaye anajishughulisha na kazi ya fundi makenika, alitangazwa leo Jumatatu Mei 16, 2022 kuwa mshindi wa Jackpoti hiyo na Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi SportPesa, Tarimba Abbas.

“Ni furaha yangu kubwa sana kwa niaba ya kampuni kumtangaza kwenu Florian Valerian Massawe kuwa ni mshindi rasmi wa Jackpot yetu akiwa amejishindia Sh1.2 bilioni.”

“Ikiwa ni takribani miezi 14 tangu kumtangaza mshindi wa mwisho wa Jackpot ambapo alipelekea Jackpot yetu kukua kwa kasi mpaka kufikia Bilioni 1 ikiwa ni mara ya kwanza kwenye historia ya Tanzania. lakini leo kwa furaha kubwa lile jambo letu limetimia,” alisema Tarimba.
Screenshot_20220516-182835_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom