Maboresho mapya kutoka WhatsApp;
- Uwezo wa makundi umeboreshwa, ambapo kundi litaweza kua na idadi ya watu mpaka 512 kutoka 256 ambayo ndio ulikua uwezo wa mwisho hapo awali.
- Uwezo wa 'emoji reactions' kwenye meseji, hautakua na ulazima tena wa ku reply' meseji na emoji' kama ilivyokua awali. Uwezo wa emoji reactions' unamuwezesha mtu moja kwa moja kujibu ujumbe kwa emoji bila kufanya kama ana reply ili kujibu.
- Uwezo wa kutuma faili mpaka 02GB, hapo awali mwisho ilikua ni 100MB lakini kuanzia hivi karibuni utaweza kumtumia mtu mpaka ukubwa huo na faili zote zitakua na end to end encryption (yaani haziwezi kusomwa kwa njia ambazo si halali na watu wengine).
Una maoni gani kuhusu mabadiliko haya mapya?
View attachment 2224869