Makapuku Forum

Makapuku Forum

Sababu za Simba SC kuachana na Bernard Morrison ni mwenendo mbaya wa kiwango chake, kuchagua mechi za kucheza vizuri, utovu wa nidhamu, kutoroka kambini usiku, mawasiliano na watu wa Yanga SC.

Morrison alisajiliwa Simba miaka miwili iliyopita akitokea Yanga.

Screenshot_20220514-101301_OGInsta%2B.jpg
 
Klabu ya Manchester City imezindua sanamu la aliyekuwa mchezaji wao Sergio Kun Aguero nje ya uwanja wa Etihad ikiwa ni kumbukumbu ya miaka 10 ya bao lake la dakika za mwisho dhidi ya QPR lililoipa taji timu hiyo mnamo Mei 13, 2012.

Aguero ndani ya miaka kumi ndani ya Man City
Mechi-390
Mabao-260
Assist- 73.View attachment 2223670
Anastahili kufanyiwa hivyo
 
Serikali imeuelekeza Uongozi wa Kampuni ya Gas Entec Tanzania ambayo inajenga Meli mpya ya MV Mwanza Hapa Kazi Tu kuzingatia makubaliano yote yaliyomo kwenye mkataba wa ujenzi wa Meli hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Mei 14, 2022 katika kikao kati yake na Balozi wa Korea ya Kusini nchini, Kim Sun Pyo kwenye ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Gas Entec Tanzania aitwaye Kwak, ambaye amekiri mapungufu katika utekelezaji wa mradi huo na aliahidi kuwa kampuni yake itaongeza kasi ya ujenzi ili ukamilike kwa wakati na Meli hiyo iweze kuwahudumia Wananchi kama ilivyokusudiwa.

Waziri Mkuu ameelekeza kuwa Wataalamu wa Kampuni ya Gas Entec Tanzania warejeshewe pasi zao za kusafiria ambazo zilizuiwa na Serikali kutokana na mapungufu yaliyojitokeza katika mwenendo wa ujenzi wa Meli hiyo.
Screenshot_20220515-031113_OGInsta%2B.jpg
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Innocent Bashungwa ametoa siku 30 kwa Meneja wa TARURA Mkoa wa Dar es salaam kufanya upembuzi yakinifu wa Barabara ya Suca - Golani katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo yenye urefu wa kilometa 7.5 ili itengewe bajeti na kujengwa kwa kiwango cha lami.

Bashungwa ametoa maagizo hayo kwa Meneja huyo Mhandisi Geofrey Mkinga wakati wa ziara katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kukagua barabara ya Suca - Golani inayohudumia kata mbili ya Saranga (Jimbo la Kibamba) na Kata ya Kimara (Jimbo la Ubungo).

Amesema baada ya Rais Samia Suluhu Hasaan kusikia kilio cha muda mrefu cha mawasiliano barabara hiyo amemuagiza kufika katika eneo hilo na kuhakikisha anatatua kero hiyo ya Wananchi.
Screenshot_20220515-031206_OGInsta%2B.jpg
 
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka ameelezea kushangazwa na ukimya wa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi katika kuelezea mafanikio ya Serikali na kusema wengi wao wapo kimya na kwamba kufanya hivyo ni kutomtendea haki Rais Samia.

“Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya kote nchini mna jukumu la kuyaeleza mafaniko ya Serikali ya Mama Samia, sasa hivi mpo kimya hamumtendei haki Rais wetu, katika utafiti wangu miaka miwili iliyopita kila RC na DC alikuwa akitoa taarifa za mafanikio ya Serikali kinyume na hali ilivyo sasa"

Shaka amesema hayo leo Mjini Babati katika mkutano wa ndani wa kujitambulisha mbele ya Wanachama wa CCM, kama Mlezi mpya wa Chama hicho kwa Mkoa wa Manyara akichukua nafasi ya Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda .

Amesema katika kipindi cha mwaka mmoja cha uongozi wake Rais Samia amefanya makubwa kana kwamba amekaa miaka mitano ikiwemo kuifungua Tanzania kiuchumi na kidiplomasia "Rais Samia ni kinara wa demokrasia katika ukanda huu wa Afrika Mashariki hilo liko wazi lazima tuyaseme mafanikio hayo, tangu aingie madarakani amechukua hatua kadhaa za kulainisha uhasama na kuponya vidonda"
Screenshot_20220515-031407_OGInsta%2B.jpg
 
Rais Samia kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa Tanzania, amempongeza Mohamed Bin Zayed kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa tatu wa Falme za Kiarabu "Nakuhakikishia kuendelea kwa ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na UAE"

Kuchaguliwa kwa Sheikh Mohamed kunakuja kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) Sheikh Khalifa bin Zayed Al Nahyan ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 73.

Sheikh Khalifa ambaye amekuwa akiugua kwa miaka kadhaa kulikosababisha kwa muda mrefu aache kujihusisha na shughuli za kila siku alimuachia mikoba Kaka yake ambaye ni Mwanamfalme wa Abu Dhabi Mohammed bin Zayed ambaye ndiye alionekana kama Mtawala kwa muda huo.

Sheikh Khalifa ambaye ni nadra kuonekana kwenye picha rasmi au kwenye hafla za umma kwa miaka mingi, alimrithi Baba yake na Mwanzilishi wa UAE Sheikh Zayed mnamo mwaka 2004, alipata kiharusi muongo mmoja baadaye na kumweka mbali na Watu tangu wakati huo.
Screenshot_20220515-031826_OGInsta%2B.jpg
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Deus Seif amesema Walimu waliielewa vizuri kauli ya Rais Samia Suluhu aliyoitoa kwenye Maadhimisho ya Mei Mosi kuhusu ahadi ya nyongeza ya mishahara ambapo wamemshukuru kwa kuitimiza ahadi hiyo na kuridhia nyongeza ya 23.3% ya mishahara kwa Watumishi "Tulisema tuna imani na Mama naona jambo limekamilika".

"Baada ya kauli yako ya Mei Mosi, Mh. Rais, Walimu tulikuelewa na tukasema tupo pamoja nawe, tunachapa kazi, kama uliweza kuwapandisha madaraja (vyeo) katika katika kipindi cha mwaka 2021/2022 pekee 92.9% ya Walimu wote ambao ni takribani 260,000, hata hili la kuongeza mishahara tulijua tu litafanikiwa"

"Kama umetoa ajira kwa awamu nne, ya kwanza Walimu 13,000, ya pili 7000, ya tatu 6000 na ya nne ni hii ya juzi 12,000 ambayo ni sawa na 15% ya Walimu waliopo na kupandisha Madaraja (Vyeo) Mwaka jana Walimu 127,000 na mwaka huu zajdi ya 60,000, watakaonufaika na Daraja la Mserereko ni Walimu 52,0000 ambapo jumla ya walionufaika ma Madaraja ni sawa na 92.9%, hata hili la mishahara tulijua litakamilika tu"

Itakumbukwa Rais Samia kupitia Mei Mosi, Dodoma aliwahikikishia Wafanyakazi kuwa jambo la nyongeza ya mishahara mwaka huu lipo kama alivyowaahidi mwaka jana na kusema mahesabu yanaendelea ili kujua itapandishwa kwa kiasi gani ambalo leo ameridhia nyongeza ya mishahara kwa 23.3%.
Screenshot_20220515-031939_OGInsta%2B.jpg
 
Rais Samia ameridhia mapendekezo ya nyongeza ya mshahara ikiwemo kima cha chini kwa Watumishi wa Umma kwa 23.3%.

Mapendekezo hayo yaliyowasilishwa Ikulu ni mwendelezo wa Kikao cha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alichokifanya Mkoani Dodoma na kupokea taarifa ya Wataalamu kuhusu nyongeza ya mshahara.
Screenshot_20220515-032054_OGInsta%2B.jpg
 
Mwanamke kutokea Jimbo la Pennsylvania nchini Marekani ameishtaki TikTok kuhusu kifo cha Mtoto wake wa miaka 10, kwa mujibu wa CBS Mama huyo aitwaye Tawainna Anderson amewasilisha kesi hiyo, takriban miezi mitano baada ya Binti yake Nylah, kushiriki katika ‘Blackout Challenge’ kwenye mtandao huo.

Challenge hiyo huwataka Watumiaji wa TikTok kujikaba hadi kuzimia, ambapo Nylah kabla ya kifo chake anadaiwa alishiriki challenge hiyo.

Desemba 7, Nylah aliripotiwa kukutwa akiwa amepoteza fahamu chumbani kwa Mama yake ambaye anasema alimkuta Binti yake amejining’iniza kwa kutumia kamba ya mkoba wake ambapo alimpeleka Hospitali akalawaza ICU hadi kifo chake mnamo Desemba 12.

Mama huyo amesema , TikTok inawapumbaza Watoto kwa ajili ya faida ya kampuni bila kujali afya zao "Nataka kuiwajibisha kampuni hii, ni wakati wa hii michezo hatari kufikia mwisho, ili Familia nyingine zisiwe na huzuni tunayoishi nao kila siku"
Screenshot_20220515-032811_OGInsta%2B.jpg
 
Siku ya jana katika Jamhuri ya Czech kulizinduliwa Daraja refu zaidi duniani la watembea kwa miguu (Sky Bridge 721) linaloning’inia mita 95 juu ya sakafu ya bonde na lina urefu wa kati ya mita 1,110 na 1,116 juu ya usawa wa bahari.

Daraja hilo limetengenezwa kwa nyaya na kujengwa kwa takribani miaka miwili iliyopita kwa urefu wa mita 721.

Kabla ya kutengenezwa kwa Daraja hilo, rekodi ya dunia ya Guinness ilitaja Daraja la Baglung Parbat Footbridge lililopo Nepal kuwa ndio Daraja kubwa zaidi kabla ya rekodi hiyo kuvunjwa sasa na Sky Bridge 721 ktoka Jamhuri ya Czech.
Screenshot_20220515-033204_OGInsta%2B.jpg
 
Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amepiga marufuku uongezaji wa gharama za vibao vya anuani za makazi kwa kuweka cha juu na kutaka zoezi hilo lisimamiwe kwa haki bila dhuluma kwa Wananchi.

Agizo hilo limetolewa na kwa nyakati tofauti katika Mikoa ya Njombe, Mbeya na Iringa alipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa zoezi hilo.

Kwa mujibu wa Nape, kuna Viongozi ambao tayari wametengeneza alichokiita dili la upigaji kupitia mpango huo na kusema Viongozi hao watashughulikiwa pale itakapobainika.
Screenshot_20220515-033409_OGInsta%2B.jpg
 
Muhubiri maarufu wa Arusha wa Kanisa la Ngurumo ya Upako Dr. GeorDavie amesema kwenye kanisa lake huwa inatokea anapanga kiwango cha sadaka cha chini wanachotakiwa kukitoa Waumini au Wahudhuriaji wa ibada.

Kwenye Interview na Mtangazaji Millard Ayo ambayo ipo yote kwenye youtube ya millardayo, Dr. GeorDavie amesema yafuatayo “katika kanisa kunakuwa na Watu wana viwango tofauti vya maisha kwahiyo ukisema toa unavyojisikia kuna mwingine utakua umemfunga lakini ukiweka kile kiwango kuanzia hapa kwenda mahali flani basi mwingine anasema hapa hata mimi najisikia nimeheshimika”

Hii ni sehemu ndogo tu ya majibu aliyoyatoa Muhubiri huyu kuhusu hili la kupanga kiwango cha sadaka ikiwemo mistari ya biblia aliyoitumia.
Screenshot_20220515-033729_OGInsta%2B.jpg
 
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Kundi la Nchi saba zilizoendelea zaidi kiuchumi duniani (G7) wameahidi kuisaidia Ukraine katika vita yake na Urusi huku Umoja wa Ulaya ukiahidi kuongeza msaada kwa Ukraine kwa zaidi ya dola nusu bilioni.

Mawaziri hao wamekutana nchini Ujerumani katika mkutano wao wa siku tatu ambapo mmoja wao ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian amesema kundi la G7 limeungana zaidi katika nia yao ya kuendelea kwa muda mrefu kuisaidia Ukraine kupigania uhuru wake hadi itakaposhinda.

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amesema umoja huo umeahidi kutoa euro milioni 500 zaidi kama msaada wa kijeshi kwa Ukraine ambapo pesa hizo zitafanya jumla ya misaada iliyotolewa na Umoja wa Ulaya kwa Ukraine kufikia euro bilioni mbili.
Screenshot_20220515-040742_OGInsta%2B.jpg
 
UNAAMBIWA Ujerumani ni miongoni mwa Nchi chache duniani ambazo Waendesha Baiskeli wake wanafata sheria mbalimbali kama wanavyotakiwa kufata Waendesha magari.

Ni jambo la kawaida kabisa kukuta Waendesha baiskeli wakiwa wamesimama kwenye barabara maalum za kuendeshea baiskeli nchini humo wakisubiri taa za barabarani ziwaruhusu kupita kama yanavyopita magari.

Usafiri wa baiskeli ni usafiri muhimu na unaotumiwa na wengi Nchini Ujerumani ambapo hadi mwaka 2017 Baiskeli zilizokuwa zinamilikiwa na Watu mbalimbali zilikua milioni 72 huku idadi ya Watu nchi nzima hadi mwaka 2020 ikiwa ni milioni 83.
Screenshot_20220515-040919_OGInsta%2B.jpg
 
Baada ya Yanga kutangulia nusu fainali Kombe la Azam Shirikisho watani wao Simba nao leo wametinga hatua hiyo kibabe wakiichapa Pamba FC ya Mwanza mabao 4-0 katika Uwanja wa Mkapa na wote watasafiri kutoka Dar hadi Arusha kupiga nusu fainali kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Screenshot_20220515-041227_OGInsta%2B.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom