Alipishana na Inter Milan juu ya sera za usajili, hakuwa tayari kushuhudia nyota kadhaa wakubwa wakiondoka, akaamua kuondoka kwakuwa hapendi kuwa sehemu ya kufeli
Akaichukua Tottenham ikiwa chini sana, akaipika anavyotaka na kuongeza majembe kadhaa, kwasasa wapo top five wanapambania nafasi ya kushiriki UEFA
Anataka fungu majira ya kiangazi, tusubiri atamleta nani na nani
Klabu ya Manchester City imezindua sanamu la aliyekuwa mchezaji wao Sergio Kun Aguero nje ya uwanja wa Etihad ikiwa ni kumbukumbu ya miaka 10 ya bao lake la dakika za mwisho dhidi ya QPR lililoipa taji timu hiyo mnamo Mei 13, 2012.
Aguero ndani ya miaka kumi ndani ya Man City
Mechi-390
Mabao-260
Assist- 73.
Winga Bernard Morrison amefunguka baada ya kusimamishwa Simba hadi mwisho wa msimu; "Kwa moyo mzito natangaza kuwa nitakuwa nje hadi mwisho wa msimu kwasababu ya masuala ya kifamilia ambayo huenda yangeathiri kiwango changu ndani ya timu. Kuna mengi ya kusema ila kwenye hili ila niitakie kheri katika mechi zetu zilizobaki. Naimani na naomba yaishe mapema zaidi ili nijiunge tena na timu"
Baada ya kuandika ujumbe huo kwenye akaunti yake ya Instagram aliweka hashtag za Simba 'One team, One dream, nguvu moja' ambazo Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez alizitumia katika sehemu ya kutoa maoni (comment) kwenye ukurasa wa Morrison.