Makapuku Forum

Anaanza kubishana na kauli zake mwenyewe

Alisema kila kitu kitapanda
 
Chenga ya mwili hii
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla ameelekeza Jeshi la Polisi kuanza mara moja msako wa kuwakamata Watuhumiwa wa wizi na unyang'anyi kwa kutumia silaha maarufu Kama Panya Road na kuwachukulia hatua kali za kisheria.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo Kufuatia taharuki iliyoibuka miongoni mwa Wananchi baada ya kutokea kwa matukio ya uhalifu maeneo mbalimbali ikiwemo Tabata, Chanika, Zingiziwa na Kunduchi ikihusisha Vijana wa kati ya miaka 13 hadi 21.

Hali hiyo imemlazimu RC Makalla kuitisha kikao kazi cha kukabiliana na uhalifu huo kikihusisha Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa, Wilaya, Wakuu wa Usalama, Makamanda wa Wilaya zote za kipolisi, Wakuu wa Vituo vya Polisi na Maafisa Polisi Jamii wa Kata na kuwapatia maelekezo.

Miongoni mwa maelekezo aliyotoa RC Makalla ni pamoja na Kamati za Ulinzi na Usalama ngazi ya Wilaya kufanya kikao na Wenyeviti wote wa Mitaa husika ajenda ikiwa kudhibiti uhalifu.
 
Kutokea Kata ya Kunduchi, Mtongani Manispaa ya Kinondoni Dar es Salaam, hizi ni picha za baadhi ya majeruhi kati ya 19 walioshambuliwa na kikundi cha Uhalifu maarufu kama Panya Road usiku wa kuamkia Mei 02, 2022.
 
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alilazimika kuondoka katika sherehe ya maadhimisho ya siku Wafanyakazi yaliyofanyika katika mji wa kaskazini-magharibi wa Rustenburg nchini humo jana, baada ya wafanyakazi kuvamia jukwaa na kumzomea.

Wafanyakazi hao walioajiriwa na mgodi wa Sibanye-Stillwater wanadai nyongeza ya mishahara ya randi 1,000 kwa mwezi badala ya randi 850 zinazotolewa na mgodi huo.

“Tumesikia mnataka randi 1,000, tutashughulikia suala hilo" Ramaphosa aliwaambia wafanyakazi waliokuwa wakiandamana.

Muda mfupi baada ya hapo Ramaphosa alilazimika kuacha kabisa hotuba yake wakati wachimba migodi waliokuwa na hasira walipovamia uwanja huo na kuwalemea polisi waliokuwa wakizunguka jukwaa kwenye Uwanja wa Royal Bafokeng, Walinzi wa Ramaphosa walimtoa nje ya ukumbi huo.
 
Jeshi la Urusi limedai limefanikiwa kuiangusha Ndege ya kivita ya Ukraine MiG-29 wakati wa vita vya angani katika eneo la Donetsk mashariki.

Msemaji wa Jeshi la Urusi amesema ulinzi wa anga wa Urusi pia uliharibu makombora mawili ya Tochka-U huko Luhansk, pamoja na kombora la Smerch huko Donetsk.

Ndege kumi zisizo na rubani za Ukraine pia zimeharibiwa, ameongeza Igor Konashenkov na kusema vikosi vya Urusi pia vimeshambulia malengo 38 ya kijeshi nchini Ukraine, yakiwemo maghala ya silaha na kambi za kijeshi.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…