Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mie na kusoma wapi na wapi jamani. Shule zina wenyewe dada. Akina joh kisomo Heaven Sent na Lovelucky ndio mambo yao hayo.
Mmh mimi na ujohn kisomo wapi na wapi jamani [emoji2297][emoji2297]

Nina certificate yangu in hotel management hapa, kutoka jordan university sina habari, hayo mabachelor degree nimewaachia nyie [emoji16][emoji16]
 
Mmh mimi na ujohn kisomo wapi na wapi jamani [emoji2297][emoji2297]

Nina certificate yangu in hotel management hapa, kutoka jordan university sina habari, hayo mabachelor degree nimewaachia nyie [emoji16][emoji16]
Kwahiyo ukaona ubadili jina kimya kimya, hizi tabia za baba yako utaacha lini?
 
Kwahiyo ukaona ubadili jina kimya kimya, hizi tabia za baba yako utaacha lini?
Basi mama hili sibadili tena

Naona mlikuwa mnanisagia kunguni we na dada ako mnaua brand mjue

Kuna watu humu wananionaga mtakatifu sana hivyo nimeona nitumie na jina la kitakatifu zaidi ili nitambae na beat lao

Kwahiyo msiniharibie tafadhali

Tuishi Humu [emoji3][emoji3] [emoji2][emoji2]
 
Basi mama hili sibadili tena

Naona mlikuwa mnanisagia kunguni we na dada ako mnaua brand mjue

Kuna watu humu wananionaga mtakatifu sana hivyo nimeona nitumie na jina la kitakatifu zaidi ili nitambae na beat lao

Kwahiyo msiniharibie tafadhali

Tuishi Humu [emoji3][emoji3] [emoji2][emoji2]
Nilijua I'd ngeni auntie aliitag kumbe karma
 
Baraza zima la Mawaziri 26 la Sri Lanka limejiuzulu kufuatia maandamano makubwa ya kuipinga Serikali yaliyofanywa na Wananchi.

Mawaziri wote 26 wamejiuzulu isipokuwa tu Rais na Waziri Mkuu na sasa Nchi nzima kuna amri inayotaka Watu wabaki majumbani ambapo imetangazwa baada ya maandamano yaliyofanyika na vurugu karibu na makaazi ya Rais Gotobaya Rajapaksa.

Serikali pia ilikata mawasiliano ya mitandao ya kijamii katika jaribio la kuzuia maandamano hayo kuenea zaidi, Asasi inayochunguza shughuli za kimtandao, imesema Facebook, Youtube, twitter, Instagram na Whatsapp yote ilikuwa haifanyi kazi.

Taifa hilo la kisiwa katika Bahari ya Hindi linakabiliwa na mgogoro wa kiuchumi ambao umesababisha uhaba mkubwa wa chakula, mafuta na dawa na hii ni moja ya sababu za Watu kuandamana.
Screenshot_20220404-160609_Instagram.jpg
 
Kinda wa Kitanzania Kelvin John (19) ambaye alipandishwa na kuingizwa kwenye Timu ya wakubwa ya KRC Genk ya Ubelgiji jana amecheza mechi yake ya kwanza jana katika ushindi wa 5-0 vs Eupen ikiwa ni mechi ya Ligi Kuu Ubelgiji.

Kelvin John katika mchezo huo aliingia akitokea benchi dakika ya 81 kuchukua nafasi nafasi ya Mjapan Junya Ito na kwenda kumalizia dakika 9 zilizosalia “Nashukuru sana Mashabiki kwa sapoti nikicheza mchezo wangu wa kwanza KRC Genk, nafuraha sana asanteni wote” ———
Screenshot_20220404-160727_Instagram.jpg
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limewakamata Watuhumiwa waliojaribu ama kuhujumu miundombinu ya daraja jipya la Tanzanite Dar es Salaam.

Akizungumza na Vyombo vya Habari Kamanda wa Polisi Jumanne Muliro anasema Watuhumiwa hao wamekamatwa baada ya kukutwa wakijaribu kufungua baadhi ya vyuma na kutaka kuchukua kwaajili ya shughuli zao binafsi.

Jeshi la Polisi limesema uchunguzi ukikamilika watuhumiwa hao watafikishwa Mahakamani Aidha Jumanne Muliro amewataka Wananchi kutunza miundombinu na endapo uhalifu unapotokea basi usisite kutokea taarifa mapema katika kituo chochote cha Polisi.
Screenshot_20220404-160851_Instagram.jpg
Screenshot_20220404-160915_Instagram.jpg
Screenshot_20220404-160932_Instagram.jpg
 
Rais wa Ukraine Volodymr Zelensky ameongea na Mashabiki wa muziki waliofika kushuhudia Tuzo za Grammy kupitia video fupi ambayo ilioneshwa kama suprise wakati John Legend akiimba wimbo wake wa ‘Free’ akiwa na Msanii wa Ukraine Mika Newton.

Kupitia video Rais wa Ukraine aliwaomba Wasaniii kutokaa kimya kutokana na vita vinavyoendelea baada ya Ukraine kuvamiwa kijeshi na Urusi ambao aliwaomba wapaze sauti kupitia sanaa "Pazeni sauti kupitia muziki, tuungeni mkono kwa njia yoyote ila msikae kimya"
Screenshot_20220404-161058_Instagram.jpg
 
SIMBA KIMATAIFA HANA MPINZANI[emoji91][emoji91]

Na @emanuelmwayombojr

Huwezi tumia nguvu nyingi kuelezea ubora wa @simbasctanzania katika michuano ya Kimataifa kwa sababu katika Nchi yetu wamejitengenezea daraja la peke yao wakifika katika hatua ya kushiriki michuano hii.

Kizuri zaidi kwa sasa Simba wanajua wao ni washindani katika michuano hii iliyo chini ya CAF ndiyo maana hata mashabiki wao wanaamini wao ni moja ya timu bora Afrika hivyo hawapendi kabisa kusikia habari ya kuondoshwa mapema katika michuano hii kwa sababu hivi sasa Simba kung'olewa katika hatua ya awali katika michuano hii ni stori kubwa kwa kuwa kila mdau wa Kandanda ana amini Simba wanaweza kufanya makubwa katika ngazi hii ya mashindano ya Vilabu bora barani Afrika.

Simba tangu miaka ya nyuma kabla @moodewji hajatia maguu kuwekeza fedha zake walishaonyesha mwanga linapokuja swala la International competition wao ni mwamba wakiwa na bajeti finyu lakini vigogo wengi wa Afrika ilikuwa ni vigumu kutoka salama katika ardhi ya Mkapa hivyo kwa sasa baada ya uwekezaji mkubwa wameonyesha makucha yao kwamba wao ni wa Kimataifa.

Vilabu vingine Tanzania vinatakiwa kujifunza kutoka kwa Simba, kwa sababu Simba siku zote wanaamini wakiwa katika ardhi tukufu ya Tanzania hatoki Mtu hii imewajenga hata wachezaji wao kupambana kwa Nguvu zao zote kwa sababu wana amini wakiwa nyumbani wamebeba imani ya mashabiki lukuki.

Alfred the great (King of wessex) aliwahi kusema Huwezi kushinda vita kama bado hujajiamini kama unaweza Simba SC kwa sasa wanaamini michuano ya Kimataifa ni jukwaa Lao la kutamba ndiyo maana wanafanya vema kwa sasa na kuipaisha ligi ya Tanzania.

Bila ubora wa Simba katika michuano hii ligi ya Tanzania bado ingekuwa mafichoni ubora wa Klabu hii Kimataifa umesabibisha ligi yetu kuwa moja ya ligi inayotupiwa macho zaidi hapa Afrika kwa sasa hakuna Mchezaji yoyote atakaye kataa kucheza ligi ya Tanzania kwa sababu anajua ligi hii inafatiliwa.

Bila ubora Simba Kimataifa nani angetambua Tanzania ni moja ya ligi yenye ushindani mkubwa ndani ya kiwanja na soka la kuvutia?Basi Nguvu yetu kubwa iwe kuinua Vilabu vingine vitishe Kimataifa.
Screenshot_20220404-161221_Instagram.jpg
 
Mshambuliaji Peter Banda wa Simba ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Machi baada ya kuwazidi kura Aishi Manula na Shomari Kapombe
Screenshot_20220404-161415_Instagram.jpg
 
Ameandika staa Bernard Morrison; "Tuliomba sapoti yenu jana usiku na mkaja kuliko tulivyotarajia, mlichofanya jana mashabiki ni upendo wa hali ya juu. Mtoto wangu ajaye nitamuita Mashabiki wa Simba Morrison,"
Screenshot_20220404-161743_Instagram.jpg
 
• Mashabiki wa Simba waliokuwa jana uwanja wa Mkapa kushuhudia timu yao ikifuzu robo fainali Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USGN, baada ya mpira kumalizika walilifuata basi la timu hiyo na kuanza kuimba jina la mshambuliaji hatari zaidi Victor Adebayor ambaye kuna tetesi anatajwa kutua Msimbazi.
Screenshot_20220404-161845_Instagram.jpg
 
• Droo ya robo fainali itafanyika kesho na Simba itapangiwa timh ambayo ilimaliza nafasi ya kwanza kati ya;

Al Ahli Tripoli ya Libya

Orlando Pirates ya Afrika Kusini

TP Mazembe ya DR Congo

[emoji777] Simba haitacheza dhidi ya RS Berkane kwasababu zinatoka kundi moja.

Screenshot_20220404-161221_Instagram.jpg
 
Basi mama hili sibadili tena

Naona mlikuwa mnanisagia kunguni we na dada ako mnaua brand mjue

Kuna watu humu wananionaga mtakatifu sana hivyo nimeona nitumie na jina la kitakatifu zaidi ili nitambae na beat lao

Kwahiyo msiniharibie tafadhali

Tuishi Humu [emoji3][emoji3] [emoji2][emoji2]
Mweeeh!! Mbona brand[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Basi tumeacha.
 
Back
Top Bottom