Makapuku Forum

Makapuku Forum

Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam wamemkamata Mohamed Omary (27), mkazi wa Chamazi kwa tuhuma za kushiriki katika matukio ya unyang’anyi wa Pikipiki kwa waendesha Bodaboda kwa kushirikiana na wenzake, Athuman Abdallah (29) mkazi wa Yombo na Hassan Twaha maarufu Dangote ( 21) Mkulima wa Mtongani Temeke

"Mbinu ambayo wahalifu hao wamekuwa wakiitumia katika unyang’anyi wa Pikipiki hizo ni kumtumia Mwanamke mmoja ambaye hujifanya mjamzito aliyefahamika kwa jina la Aziza Hamza (21), Mkazi wa Yombo ambaye hukodi bodaboda mpaka walipo wenzake kwa ajili ya kupora pikipiki"

"Tukio la uporaji likikamilika wahalifu hao huzipeleka pikipiki hizo kwa Omary Salum (30) , mkazi wa Tandika, Kilimahewa ambaye kazi yake ni kutoa GPRS/ ving’amuzi kwa pikipiki zenye ving’amuzi, Athuman Mohammed Bakari maarufuku BOKO ( 42) mkazi wa Kilwa Kivinje yeye hujihusisha na kuzitafutia kadi na kuziuza katika mikoa ya Mtwara na Lindi"

"Jeshi la Polisi limefanikiwa kumkamata Sophia Musa (28) mkazi wa Toangoma ambaye ndiye mpokea maombi ya kutengeneza kadi toka kwa BOKO na baadae kumpelekea Ibrahimu Ally (31) mkazi wa Buguruni ambaye hufanya kazi ya kudurufu kadi hizo za Pikipiki, katika katika upekuzi watuhumiwa hao wamekutwa na Pikipiki tatu (3) za wizi, (MC 292 DCE, MC 733CEG na MC 250 DBF), kadi za pikipiki (9) Kadi za Gari (11), vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya kumaliza elimu ya sekondari, stika za mamlaka ya mapato (TRA) na stika za Baraza la Mitihani vyote vinachunguzwa"
Screenshot_20220402-052305_Instagram.jpg
 
Vyombo mbalimbali nchini Msumbiji vimeripoti kwamba Eurélia Manuel Benjamim Raia wa Msumbiji ambaye alidhaniwa kuwa amefariki dunia na ambaye mazishi yake yalifanyika mwezi November mwaka jana ametokea kijijini kwao Lindi nchini Msumbiji.

Eurélia Manuel Benjamim anatajwa kama Mtu aliyefufuka kutoka kwa wafu lakini yeye mwenyewe anasema alikuwa ameenda tu kufanya kazi katika shamba la Mjomba wake kwa miezi michache.

Msimamizi wa eneo katika Wilaya ya Montepuez amesema Walifanya sherehe zote za mazishi, sherehe ya siku ya tatu na kutembelea kaburi na kaburi halijavunjwa.”

Kikosi cha wataalamu kinatumwa kwenye Kijiji cha Lindi nchini humo kufanya uchunguzi ili kuona ni nani au nini kilizikwa kaburini.
Screenshot_20220402-052552_Instagram.jpg
 
Imeripotiwa kuwa mashine maalum ya VAR (Video Assistant Referee) iliyokuwa imewekwa Abuja Nigeria kwa ajili ya kusaidia waamuzi wa mchezo wa play off wa kufuzu Kombe la Dunia kati ya Ghana na wenyeji Nigeria imeibiwa uwanjani hapo.

Mchezo huo Ukimaliza kwa sare 1-1 ambapo goli la ugenini likaipa nafasi ya kufuzu Ghana, ziliibuka vurugu kwa mashabiki wa Nigeria kuingia uwanjani baada ya matokeo kutokuwa rafiki.

Hata hivyo mapema leo FIFA imetangaza kuufungia uwanja huo wa MKO Abiola uliopo Abuja kutokuchezwa kwa michuano/mechi za Kimataifa
Screenshot_20220402-053138_Instagram.jpg
 
Makamu Mwenyekiti mpya wa CCM Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana amemuhakikishia Mwenyekiti wa Chama hicho (Rais Samia) kwamba hatomuangusha "Juzi jioni Rais Samia uliniita nikawa najiuliza naitiwa nini?, nilipofika Rais akaniambia nataka uwe Makamu Mwenyekiti nikamwambia sina hiari zaidi ya kusema nakubali, nakuhakikishia Mwenyekiti (Rais Samia) nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kufikia matumaini yako, kufanya kazi kwa bidii na kwa lugha nyingine kwa kifupi niseme sitokuangusha"

"Nawashukuru Wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa kunipa kura zote mmenitwisha mzigo mzito, mmeonesha imani yenu kwangu na imani huzaa imani na Mimi nitaitumikia CCM na Watanzania"

"Nakupongeza Mzee Mangula kwa kustaafu kwa heshima, umefanya kazi iliyotukuka kwa Chama chetu, Mimi ni Mwanafunzi wa Mzee Mangula wakati akiwa Kivukoni Mimi nilikuwa Mwanafunzi"
Screenshot_20220402-053250_Instagram.jpg
 
Unamtenga Van Djik[emoji23][emoji1787][emoji1787]?

Senegal ni ya sisi non fan’s wa liver
Mbele ya Senegal anisamehe tu
Na yule kipa wenu wa Chelsea aiseee hii timu ni unbeaten[emoji1787]

Nasimama na rangi[emoji16] ..mablack wenzangu[emoji110]
 
Rais Samia wakati akiwaapisha Viongozi mbalimbali Ikulu,Chamwino Dodoma leo amesema hali ya Utumishi wa Umma sio nzuri sana na kwamba katika awamu ya tano baadhi ya Watumishi walisifiwa kwa heshima ambayo haikutoka moyoni bali ilitokana na uoga.

"Tunasifiwa kwamba adjustments tuliyoyafanya awamu ya tano imeleta heshima ndani ya utumishi wa umma, heshima iliyokuzwa ni ya uoga kwasababu kulikuwa na Simba wa Yuda ambaye alikuwa ukigusa sharubu anakurarua lakini hata hivyo hatukukua kivile, heshima inayotakiwa iwe ya moyoni, kila mmoja awe na itikadi moyoni kwake kwamba Mimi ni Mtumishi wa Serikali majukumu yangu ni haya, kila mmoja aheshimu laini ya mwenzie hicho tunakosa Serikalini"

“Unaangalia kila siku unasika Waziri kaparurana na katibu wake, katibu kaparurana na waziri wake naibu hamueshimu nani hakuna hiyo kitu nadhani kuna kitu tunakosa mahali"
Screenshot_20220402-132303_Instagram.jpg
 
Baada ya kumpiga Mtangazaji Chris Rock jukwaani katika Tuzo za Oscar weekend iliyopita, Mwigizaji Will Smith ametangaza kujiuzulu kutoka ‘The Academy of Motion Pictures Arts & Sciences” ambacho ndio Chuo kinachoandaa tuzo za filamu za Oscar.

"Ninajiuzulu uanachama katika Chuo cha Sanaa na Sayansi ya Picha na nitakubali matokeo yoyote ambayo bodi itaona yanafaa, mabadiliko huchukua muda na nimejitolea kufanya kazi ili kuhakikisha kwamba sitaruhusu tena vurugu kutokea"

Baada ya tukio zima katika Tuzo za Oscar jumapili iliyopita, Chuo hicho kilitangaza tarehe 30 March kwamba kimeanzisha kesi za kinidhamu dhidi ya Smith.
Screenshot_20220402-132625_Instagram.jpg
 
Rais Samia Suluhu Hassan amewaapisha Viongozi mbalimbali Wateule leo Ikulu Chamwino Dodoma ambapo amewataka wakafanye kazi kwa kufuata miongozo na sheria za nchi huku akisisitiza kuwa yeye sio Mtu wa kufokafoka bali atatumia kalamu kuwachukulia hatua wanaokosea.

"Msiende kuendekeza nafsi zenu, katika utendaji kazi 70% inachukua miongozo, dira na sheria za Nchi na 30% unasikiliza nafsi yako na nafasi yako ukiisikiliza ikupeleke kwenye malengo mazuri sio malengo mabaya wote lengo letu kukuza uchumi na ustawi wa Nchi yetu na kukuza jina la Tanzania, mkaheshimu viapo mlivyoapa"

"Huko nyuma nilisema sitofoka nitafanya kazi kwa kalamu, nitawakumbusha lakini sitofoka kwasababu hata ukinitazama sijaumbwa kufokafoka na Mimi ni Mama ni Mlezi nitajaribu kuwalea lakini ulezi utakaponishinda nitachukua hatua, niwaombe sana mkanisaidie sio mkaharibu mkanisaidie"
Screenshot_20220402-132735_Instagram.jpg
 
• Mapadre 50 wa jimbo Katoliki la Moshi wanashiriki ibada ya mazishi ya Profesa wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa Honest Ngowi aliyefariki dunia Machi 28, 2022 kwa ajali ya gari wakati akielekea kwenye shughuli zake za kikazi.

Screenshot_20220402-132955_Instagram.jpg
 
Mahaba.

Huyu ni shabiki wa klabu ya Konkola ambayo inashiriki ligi kuu nchini Zambia, tukio hili lilitokea wakati wa mchezo ambao uliihusisha timu yake ambapo alifanikiwa kuruka fensi ya uwanja na kwenda katika benchi la wachezaji wa akiba kuwaomba waipambanie timu hiyo ili isishuke daraja.

Konkola inashika nafasi ya 18 kwenye msimamo ikiburuza mkia, wamefanikiwa kukusanya alama 24 tu katika michezo 28 waliyoshuka dimbani mpaka sasa huku zikisalia mechi nane kabla ya ligi kutamatika.
Screenshot_20220402-133202_Instagram.jpg
 
“Kama huwezi kukaba kama wengine basi hakikisha unafunga bao kila mechi ili usikabe, tofauti na hapo utakaba kama wengine”-Antonio Conte alimwambia Eden Hazard, wakati yeye ndie Kocha pale Chelsea.
Screenshot_20220402-133357_Instagram.jpg
 
All the way up, alicheza Azam akaenda kwa mkopo Biashara United, akatwaa tuzo ya mchezaji chipukizi wa ligi kuu bara

Akapanda ndege kuelekea Ulaya, akakomaa kwenye mazoezi na sasa ni panga pangua Tel Aviv, akirejea nchini ni majukumu ya timu ya taifa tu

Ni stori fupi ya the Pitbull @nover_d_40 mtalaam wa geoni ya leo

We all love need to have team of the Novas
Screenshot_20220402-133516_Instagram.jpg
 
Tuzo za muziki za Tanzania zinatolewa usiku huu ikiwa ni miaka 7 imepita bila uwepo wa Tuzo hizi nchini Tanzania, tuzo za mwaka huu zinatolewa kwenye Ukumbi wa JNICC Dar es salaam na tayari zimeanza kutolewa ambapo Watu watano wa kwanza kupewa tuzo ya heshima ni Rais Samia, Mkuu wa Majeshi Mabeyo, Marehemu Ruge Mutahaba, Marehemu Bibi Kidude na Mwimbaji Diamond Platnumz.

“Mh. Rais Samia ameupiga mwingi sana, miaka 7 ya Tuzo kukosekana ametenga zaidi ya bilioni 1.5 kwa ajili ya Wasanii na tasnia hii na sasa zinafanyika tena Serikali ikigharamia tukio hili kwa zaidi ya 90%”

Tuzo kwa Marehemu Ruge: “Tuzo hii inatolewa kwa sababu Marehemu Ruge alianzisha na kuibua vipaji mbalimbali kwa Wasanii, atakumbukwa sana kwa mchango wake mkubwa kwenye muziki wa Tanzania hivyo Baraza limeamua kumpa Tuzo ya heshima”

Tuzo nyingine ya heshima imekwenda kwa Diamond Platnumz "Tuzo hii inatolewa kwake kwa sababu ni Msanii ambaye alileta mabadiliko katika tasnia kwa kuongeza thamani ya muziki hasa katika dhana ya sanaa ni biashara, Diamond ameonesha kwa vitendo na kwa kuwekeza zaidi kwenye matumizi ya digitali, kujibrand na kuseti viwango vya malipo vyenye tija katika kazi zake lakini kubwa zaidi kuuza muziki nje ya Tanzania"
Screenshot_20220403-034125_Instagram.jpg
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Video Queen of the year 2021 - Feven Reuben ( Fevushka), Video King of the Year 2021 - Selemani Masenga, Dancer bora wa kike 2021 - Baby Drama, Dancer Bora wa kiume 2021 - Kukaye moto Culture Centre, Mwimbaji bora wa kike nyimbo za asili 2021 - Shoninda Kilasi, Mwanamuziki bora wa kiume wa muziki wa asili 2021 - Msafiri Zaosa, Wimbo bora wa asili 2021 - asili yetu ya Sholo Mwamba.
Screenshot_20220403-034313_Instagram.jpg
Screenshot_20220403-034333_Instagram.jpg
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Back
Top Bottom