Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20220403-042319_Instagram.jpg
Screenshot_20220403-042340_Instagram.jpg
 
Kwenye tuzo za jana usiku, nimezitazama kwa umakini mkubwa sana ni kama ulikuwa usiku wa Ali Salehe Kiba akiokota hii na ile

Kwanza kabisa naamini ana fan base kubwa sana kuliko aliokuwa anashindana nao hivyo mtaji wa kura anao tena mkubwa tu

Pili mziki wa Kiba ni mkubwa sana, sidhani kama kuna tuzo ambayo hakustahili bali kuna zingine pia niliona alipaswa kuzikwapua

Ni bahati kuwa na Msanii kama Kiba, great talent na mziki wake unaishi sana, sidhani kama unachoka kuanzia hata Mac Muga mpaka Salute
Screenshot_20220403-085247_Instagram.jpg
 
Sarah Kitinga maarufu kama Saraphina, ni moja kati ya talent kubwa sana kwenye mziki wetu nchini na anafanya vizuri sana wa upande wa Wanawake

Silaha yake kubwa ni stage perfomance haswa kwenye kucheza (choreography) eneo hilo wasanii wengi wa kike hawakulipa uzito stahiki ila yeye kaamua kuwekeza zaidi hapo

Mhitimu wa Chuo kikuu cha Dar Es Salaam alieamua kuwa serious na mziki, binti mwenye energy kubwa stejini, manjonjo na ubunifu mkubwa, to me tuzo alizobeba jana alistahili hazina maswali

Kilichosalia sasa ni mwendelezo wa hiki anachofanya sasa, akikomaa zaidi basi sky is no longer the limit
Screenshot_20220403-085356_Instagram.jpg
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Real Madrid jana walipata faida ya penati tatu dhidi ya Celta Vigo, ambapo Karim Benzema aliweka penati mbili kimiani

Lakini kwa kumbukumbu ni kuwa msimu wa 2020/21, mchezo wa Valencia dhidi ya Real Madrid, miamba Valencia ilipata penati tatu na zote Carlos Soler alifunga

Kifupi ni kuwa Soler alipiga hatrick ya penati
Screenshot_20220403-085458_Instagram.jpg
 
Swali litabaki kuwa, huyu kinda Elanga licha ya kuwa anafunga ila anastahili kuanza kuvaa jezi mbele ya Marcus Rashford au Jesse Lingaard?

Swali litabaki kuwa, kwa maendeleo ya kinda kama yeye kutoka Carrington ni sahihi kucheza zaidi ya dakika 50? Jibu ni hapana, hawa makinda wanapaswa kuingia taratibu

Kwenye tukio hili pichani, Marcus Rashford angefunga kabisa kabla ya Elanga kumpiga tackling na kukosa nafasi adhimu

Sipingani na kuwapa nafasi makinda ila jezi hii ni nzito sana wakati mwingine

Screenshot_20220403-085553_Instagram.jpg
 
[emoji3578][emoji3578] Farhan Jr

Wakati wachezaji wa Liverpool wanashangilia ubingwa wa Carabao uwanjani pale Wembley, kila Mchezaji alikuwa na namna ya kuonesha furaha yake baada ya kuifunga Chelsea kwa penati

Mchezaji mmoja alishika chupa ya pombe na akataka aifungue kisha aimwage, ila pembeni yake alikuwepo Sadio Mane nyota ambaye ni muumini wa dini ya Kiislam ambaye pombe kwake ni haramu

Mane kwa haraka sana alimwomba mwenzie asifungue chupa ile ya pombe mbele yake, uungwana mkubwa pia kwa Mchezaji mwenzake ambaye nae alimuelewa Mane na akaacha kuifungua

Wakati wapo vyumbani wakiendelea na sherehe za ubingwa, picha nyingi sana za ndani Mane hakuonekana ila kulikuwa na footage moja tu ambayo Mane alikuwa ameshika mswala (mkeka wa kuswalia)

Kwenye video hiyo Mane alionekana anatoka anaelekea kwenye chumba kingine kwa ajili ya kukamilisha ibada ya swala ya Magharib baada tu ya mechi kuisha, ndio maana hakuonekana kabisa mwanzoni mwa sherehe

Sadio Mane huyu huyu baada tu ya kubeba ubingwa wa AFCON 2021, Liverpool ilikuwa tayari kumuandalia sherehe wakati anarejea ila yeye alituma ombi maalum kuwa wasimfanyie sherehe yoyote kwa heshima ya MO Salah wa Misri

Ikaja tena kuwa Mane na Senegal yake wamefuzu fainali za kombe la dunia, ni yeye tena akatuma ujumbe kuwa wasimfanyie sherehe yoyote kwakuwa ana heshima yake kwa Mohamed Salah na wachezaji wengine wa Afrika kikosini

Huyu ndie Sadio Mane ambaye Jurgen Klopp anasema sababu ya kumtumia Mane moja kwa moja kikosini akitoka michuano ya kimataifa ni kuwa, Mane hanywi kabisa pombe hivyo hana shida kwenye fitness

Niwatakie mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa hisani ya Ndugu yetu katika imaan, Ustadh Sadio Mane[emoji120]

We all dream to have the attitude like Sadio Mane
Screenshot_20220403-085859_Instagram%20Lite.jpg
 
MOYES ATAJA BILIONI 450 BEI YA RICE !!
.
Kocha wa West Ham United, David Moyes anaamini thamani ya kiungo Declan Rice ni zaidi ya Pauni 150 milioni (Sh 457 Bilioni) baada ya klabu kubwa za Ligi Kuu England kuonekana kusumbukia huduma yake.
.
Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 23 amekuwa akihusishwa na Chelsea, Manchester United na Manchester City.
Screenshot_20220403-090159_Instagram.jpg
 
FAINALI NI LEO KUNDI D [emoji91]
.
SIMBA [emoji1241] [emoji739] [emoji1183] US GENDERMARIE
[emoji354] 04:00 usiku
[emoji909] Benjamin Mkapa Stadium.

.
BERKNE [emoji1173] [emoji739] [emoji1081] ASEC
[emoji354] 04:00 usiku
[emoji909] Stade Municipal de Berkane.
.
Msimamo Kundi D
1. Asec Mimosas — 9
2. Berkane — 7
3. Simba — 7
4. US Gendermarie - 5
.
Kila la kheri @simbasctanzania [emoji1241]
Screenshot_20220403-090358_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom