Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,258
- 464,593
Shabiki mmoja Kijana wa Uingereza amehukumiwa kifungo cha wiki sita jela baada ya kupatikana na hatia ya kumtukana na kuonyesha ubaguzi wa rangi kwa Mchezaji wa Manchester United Marcus Rashford baada ya kushindwa kufunga penati kwenye mechi ya England katika fainali ya Euro 2020.
Kijana huyo Justin Lee Price (19) kutoka Worcester, Uingereza alikiri kosa katika Mahakama ya Kidderminster ya "shitaka moja la kutuma ujumbe wa kuudhi kwa mtandao wa mawasiliano ya umma".
Kijana huyo awali alikanusha mashtaka hayo wakati wa mahojiano na polisi, pia alibadilisha jina lake kwenye account yake ya Twitter ili kuepuka kutambuliwa lakini baadae alikiri kufanya kosa hilo, muda wa kifungo chake ulipunguzwa kwasababu alikiri kosa na kukubali mashtaka yake Mahakamani.