Makapuku Forum

Makapuku Forum

MSHAHARA WA MOSIMANE KUFURU
.
Miamba ya soka la Afrika, klabu ya Al Ahly imetangaza rasmi kumuongezea mkataba Kocha Pitso Mosimane (57) kwa miaka mingine miwili huku ikielezwa kuwa mshahara wake utaongezwa hadi dola za Marekani 185,000 kila mwezi sawa na Sh milioni 428.
Screenshot_20220310-041159_Instagram.jpg
 
PABLO: KAMA CHAMA ANACHEZA ATAPIGA PENATI ZOTE
.
“Ukiangalia wengi wanaonekana kuogopa, nafikiri inatokana na hii baadhi kuzipoteza karibuni.
.
“Angalia alivyojiamini (Chama). Nafikiri ni vyema kumpa mtu jukumu hili ambaye anaonyesha kujiamini na kama atakuwepo ndani ya uwanja chaguo la kwanza litakuwa kwake,” amesema Kocha Pablo Franco.
Screenshot_20220310-041307_Instagram.jpg
 
CAF YAIPA SIMBA MASHABIKI KIBAO
.
Simba wamepata mzuka wa aina yake baada ya CAF kuruhusu kuingiza mashabiki zaidi ya nusu kwenye Uwanja wa Mkapa Jumapili dhidi ya Berkane katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.
.
Iko hivi, Simba waliomba Shikirikisho la Soka Afrika (Caf) waingize mashabiki 60,000 ili kujaza uwanja katika mchezo wa wikiendi dhidi ya Berkane ya Morocco. Hata hivyo, Caf imewapa mashabiki 35,000 ambao ni zaidi ya nusu ya uwanja huo unaobeba 60,000.
Screenshot_20220310-041356_Instagram.jpg
 
IBENGE APEWA MECHI MOJA
.
Taarifa kutoka nchini Morocco zinasema kuwa endapo kocha wa RS Berkane, Florent Ibenge atashindwa kuifunga Simba atafukuzwa.
.
Simba itacheza mchezo wa marudiano Jumapili kwenye uwanja wa Mkapa katika kombe la Shirikisho Afrika.
Screenshot_20220310-041606_Instagram.jpg
 
Kiungo mshambuliaji wa Simba SC Hassan Dilunga ataendelea kukosekana kwenye kikosi cha Simba kitakachocheza dhidi ya RS Berkane siku ya Jumapili kwenye dimba la Benjamin William Mkapa.

Dilunga bado anaendelea kuuguza majeraha, Chama yeye anaendelea kukosekana kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa sababu za kikanuni.
Screenshot_20220310-041753_Instagram.jpg
 
Rais wa Ukraine Volodymir Zelensky ametoa wito hii leo wa kupata suluhu ya dharura kuhusu mvutano ulioibuka ya ombi la Poland la kuipelekea Ukraine ndege za kivita wazo ambalo Ujerumani, Canada na Marekani wamelipinga.

Jana Marekani nayo ilipingana na Poland kuhusu wazo la kupeleka ndege hizo aina ya MiG-29 za enzi ya kisovieti nchini Ukraine kupitia kambi ya jeshi la anga la Marekani iliyopo Ramstein Ujerumani, hata hivyo Marekani na Nchi nyingine za Ulaya waliipelekea Ukraine silaha ikiwa ni pamoja na vifaru lakini hawakupeleka ndege za kivita kwa wasiwasi wa kuchochea ugomvi zaidi na Urusi.

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akiwa Berlin na Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau wameonyesha kutokukubaliana na Poland kwenye wazo la kupeleka ndege hizo Nchini Ukraine wakisema wanataka vita hii imalizike na sio kuichochea.
Screenshot_20220310-042830_Instagram.jpg
 
Mpaka sasa kampuni zilizofikia 47 zimetangaza kusitisha biashara zao Nchini Russia na kuungana na Mataifa mbalimbali kupinga vita inayoendelea Nchini Ukraine baada ya Majeshi ya Russia kuanza kushambulia nchi hiyo zaidi ya siku 10 zilizopita.

Miongoni mwa Kampuni hizi ni DHL, Puma, Boeing, VISA, Heineken, Youtube, Fedex, Microsoft, Google, Uniliver, Cocacola, Pepsi, McDonald, Pizza hut, Bp, Maersk, Air BNB, UPS, Toyota, VW na Ford.
Screenshot_20220310-043009_Instagram.jpg
Screenshot_20220310-043221_Instagram.jpg
 
Mwanaume aitwae David Bennett mwenye umri wa miaka 57 kutokea Maryland nchini Marekani ambaye ndiye binadamu wa kwanza kupandikizwa moyo wa nguruwe, amefariki.... Kituo cha Matibabu cha Chuo Kikuu cha Maryland kimesema leo.

David amefariki leo Jumanne baada ya hali yake kuanza kuwa mbaya siku kadhaa zilizopita ambapo saa kadhaa kabla ya kifo chake aliwasiliana na familia yake "tumehuzunishwa na kumpoteza Bennett, alionesha kuwa Mgonjwa jasiri ambaye alipigana hadi mwisho" amesema Dr. Bartley P. Griffith ambaye ni Bingwa wa upasuaji ambaye alimpandikiza moyo wa nguruwe katika Chuo Kikuu cha Maryland Medical Center.

Bennett alikuwa na ugonjwa sugu wa moyo na alikuwa amepokea moyo wa nguruwe Januari 7. Bennett baada ya kuonekana kutostahili kupandikizwa moyo wa kawaida au pampu ya moyo za bandia baada ya ukaguzi wa rekodi zake za matibabu ambapo moyo wa nguruwe ndio lilikua chaguo pekee lililopatikana, taarifa ya kituo cha matibabu imeeleza pia kwamba hali yake ilikuwa nzuri wiki chache baada ya upasuaji ila hali yake ilibadilika.
Screenshot_20220310-043356_Instagram.jpg
 
Walimu zaidi ya elfu hamsini (50,000) Tanzania nzima wanatarajiwa kupanda madaraja mawili mfululizo yanayotambulika kama madaraja ya mserereko.

Hatua hii inakuja baada ya mwaka 2016/2017 Watumishi wa umma kupandishwa madaraja lakini kukatokea zoezi la uhakiki hivyo waliokua wamepewa barua hizo kusitishiwa upandaji wa madaraja kwa Waalimu.

Katibu Mkuu wa CWT Deus Seif akiwa mkoani Iringa amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuamua kuwapandisha madaraja mawili Walimu hao waliyoyaita madaraja ya mserereko.
Screenshot_20220310-043546_Instagram.jpg
 
Pamoja na kwamba Wanawake wa Ukraine wameruhusiwa kuondoka Nchini humo ili kuikimbia vita, ripoti mpya imesema kuna idadi kubwa ya Wanawake waliogoma kuondoka ili wajiunge na jeshi la Nchi yao kupambana na Urusi.

Wanawake mbalimbali wakiwemo wasio na uzoefu wa kutumia silaha wameweka mbele uzalendo kwa taifa lao na kuamua kuchukua silaha zinazomwagwa mtaani na Jeshi la Ukraine kwa ajili ya Wananchi waliokubali kuungana kupambana na Majeshi ya Russia ambayo yameivamia Ukraine kwa zaidi ya siku 10 sasa.

Katika idadi nzima ya Wanajeshi wa Ukraine Wanawake ni asilimia 15.
Screenshot_20220310-043804_Instagram.jpg
 
Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte ametia saini sheria ya kuongeza umri wa Msichana kutoa idhini ya kufanya mapenzi kutoka miaka 12 hadi miaka 16 ikiwa ni juhudi za kuwalinda Watoto dhidi ya ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia.

Wanaharakati nchini Ufilipino wamekuwa wakishinikiza kuongeza umri wa idhini tangu miaka ya 1980 kwani sheria ya zamani ililinda ‘Wanyama wanaokula wenzao ‘ na kwamba watoto wa miaka 12 mara nyingi wanaweza kulazimishwa au kutishiwa kunyamaza.

Hadi sasa Ufilipino imekuwa nchi mojawapo katika Nchi ambazo zina umri wa chini kabisa wa ridhaa ya kujamiiana, nyuma ya umri wa miaka 11 wa Nigeria, kulingana na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Kuhudumia Watoto (UNICEF).

Chini ya mswada huo ulioidhinishwa na Duterte ambao hauegemei jinsia Mtu mzima yeyote anayeshiriki ngono na Mtu yeyote mwenye umri wa miaka 16 au chini ya hapo atakuwa anafanya ubakaji.
Screenshot_20220310-043915_Instagram.jpg
 
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameagiza Hospitali zote za Rufaa nchini kuwa na huduma za kupima na kutoa chanjo ya homa ya manjano kwa wasafiri na wenye uhitaji na pia ameagiza maafisa wa afya mipakani kuhakikisha wasafiri wanaoingia kutoka nchi zenye maambukizi wanakua na vyeti vya chanjo.

Ummy ametoa agizo hilo wakati akitoa tahadhari ya kuzuka kwa ugonjwa wa Homa ya Manjano (Yellow Fever) ambapo amesema hadi kufikia tarehe 3 March 2022 nchini Kenya kulikua na Wagonjwa wa Homa ya manjano 15 na vifo vitatu (3) ambapo katika sampuli sita zilizopimwa maabara ya Kenya kwa kutumia vipimo vya serology na PCR sampuli 3 zilithibitika kuwa na maambukizi.

"Tutaboresha mifumo ya kutoa vyeti vya kielektroniki vya homa ya manjano mipakani ili kuzuia udanganyifu unaoweza kufanywa na maafisa kuwapa vyeti watu ambao hawajachoma chanjo"

Waziri Ummy amewataka Wananchi kuchukua tahadhari na kujua dalili za ugonjwa wa homa ya manjano kama homa, kuumwa kichwa, maumivu ya misuli na mgongo, mwili kutetemeka, kupoteza hamu ya kula, kichefuchefu na kutapika, mwili kuwa na manjano, kutokwa na damu sehemu za wazi.
Screenshot_20220310-044120_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom