Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20220301-062820_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20220301-062837_Opera%20Mini.jpg
 
Kampuni ya Apple imesitisha kuuza simu za iPhone na bidhaa zake nyingine nchini Urusi na kujiunga na Kampuni nyingine mbalimbali ambazo zimetangaza kujiondoa Urusi baada ya kuivamia kijeshi Ukraine.

Wafanyabiashara wengine wakubwa wa teknolojia kama Google na Twitter pia wamepunguza biashara zao nchini Urusi ‘tunaungana na wote wanaotaka amani duniani’ imeeleza taarifa ya Apple.

Pamoja na kusitisha uuzaji wa bidhaa, Apple inasema duka lake la programu za simu linazuia upakuaji wa RT News na Sputnik News kutoka nje ya Urusi zikiituhumu mitandao hiyo kuwa inarusha habari za propaganda kutokea Ofisi za Serikali ya Urusi.

Apple pia imesitisha kutuma location za moja kwa moja kwenye ramani za Apple nchini Ukraine kama hatua ya usalama, sawa na hatua ambayo tayari Google imechukua.
Screenshot_20220302-105058_Instagram.jpg
 
Mtandao wa Instagram umefungia akaunti za Chombo cha Habari cha Urusi cha RT katika Nchi zote Wanachama wa EU baada ya kupokea taarifa kutoka Serikali za Nchi hizo zikidai Chombo hicho kinaeneza propaganda kuhusu mzozo wa Urusi na Ukraine.

Ufungiwaji huo unakuja baada ya Facebook na Youtube pia kukifungia Chombo hicho.
Screenshot_20220302-105425_Instagram.jpg
 
Meli ya mizigo iitwayo Felicity Ace iliyokuwa imebeba maelfu ya magari ya kifahari imezama katika visiwa vya Ureno vya Azores karibu wiki mbili baada ya kushika moto ilikuwa ikisafirisha magari ya kifahari 4,000 yakiwemo aina ya Porsches na Bentleys.

Meli hiyo ilikuwa njiani kuelekea Rhode Island nchini Marekani kutoka bandari ya Ujerumani ya Emden wakati moto ulipozuka, Wahudumu wote wa meli hiyo waliokolewa wakati moto huo ulipoanza Februari 16.

Joao Mendes Cabecas, Nahodha mmoja ya bandari iliyo karibu katika kisiwa cha Faial, amesema hakuna uvujaji wa mafuta ulioripotiwa hadi sasa lakini alisema kuna hofu kwamba matenki ya mafuta yanaweza kuharibika wakati chombo hicho kikiwa chini ya bahari ya Atlantic katika kina cha mita 3,500 (maili 2.17).
Screenshot_20220302-105536_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom