Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20220227-064858_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20220227-064914_Opera%20Mini.jpg
 
TUNAMKOSEA HESHIMA SAIDO
.
Tangu Saido amerejea katika kikosi cha kwanza cha Yanga hakuna mchezaji aliyefanya vizuri zaidi yake. Labda Fiston Mayele tu.
.
Saido amekuwa na wastani mzuri wa mabao ya kufunga. Ndio mchezaji anayeamua Yanga ishambulie vipi. Ule ushawishi aliokuwa nao Feisal Salum mwanzoni mwa msimu sasa umehamia kwa Saido.
.
Anaisukuma timu mbele kwa kasi ya ajabu. Anatengeneza nafasi kwa wachezaji wenzake. Anakaa kwenye nafasi na kuifanya Yanga kuwa na utulivu wa kutosha katika eneo la kushambulia.
.
Kuanzia mwisho wa mwezi Novemba Saido amefunga magoli matano na kutoa pasi moja ya goli kwenye Ligi Kuu. Katika kipindi hicho Feisal amefunga goli moja tu na pasi moja ya goli.
.
Hii ndiyo sababu nasema kuna namna tunamkosea heshima Saido.
Screenshot_20220227-133029_Instagram.jpg
 
KHA! RONALDO AJIPA MIAKA MINGINE MITANO
.
Supastaa, Cristiano Ronaldo anataka kucheza kwa miaka mingine mitano zaidi kabla ya kuamua kutundika daruga. Staa huyo wa Manchester United, Ronaldo kwa sasa umri wake ni miaka 37.
.
“Ni ngumu kusema kwamba sihitaji zaidi, nipo kwenye klabu inayonipa nafasi ya kushinda mataji zaidi, kwanini isiwe? Nafahamu sina miaka mingi iliyobaki kwenye soka, inaweza kuwa miaka minne au mitano, tutaona. Nataka kushinda mataji zaidi.”
.
Ronaldo yupo katika ukame mkubwa msimu huu katika mechi 8 zilizopita amefunga bao moja tu kwenye mechi dhidi ya Brighton wiki iliyopita.
Screenshot_20220227-133216_Instagram.jpg
 
SIMBA WAPIGENI WAMOROCCO
.
BERKANE SIMBA SC
CAF CONFEDERATION CUP
22:00
Stade Municipal de Berkane
.
Tunaamini Simba leo itacheza kufa na na kupona kuhakikisha Haipotezi mchezo huu licha ya kuonekana ni mgumu kwao kutokana na uwezo wa Berkane.
.
Hata hivyo, kwa uwezo wa kikosi cha Simba na rekodi zao kwenye michuano hii na mechi zilizopita, hatuoni ikikosa nafasi ya kusonga kwani imekuwa ni moja ya timu tishio Afrika
.
Tunaitakia kila la kheri simba waibuke na ushindi kwenye mchezo huu wa leo kwani uwezo huo inao na Watanzania wana imani nao
Screenshot_20220227-133409_Instagram.jpg
 
Jumapili ya Soka

Saa 1:00 usiku ni Yanga vs Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar

Saa 1:30 ni pale Uwanja wa Wembley fainali EFL vigogo Chelsea dhidi ya Liverpool wanakiwasha..

Tunamalizia na saa 4:00 usiku ni RS Berkane vs Simba mechi ya 3 hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika.

Unashabikia timu gani leo?
Screenshot_20220227-133600_Instagram.jpg
 
Solid performance jana kutoka kwa Kennedy Mweene, golikipa namba mbili wa Mamelodi Sundowns ni raia wa Zambia

Vuta tu picha, ubora kama ule ni kipa namba mbili ambaye Onyango akirejea anapaswa kurejea bench

Investment, Investment, Investment! Hotel tu waliyofikia Mamelodi huko Alexandria ndio hotel waliyofikia Atletico Madrid pre season
Screenshot_20220227-133719_Instagram.jpg
 
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amesema yuko tayari kwa mazungumzo na Russia huku akikataa msukumo wa Moscow kutaka yafanyikie nchini Belarus kwamba huenda ikawa ni njia ya kuzindua majeshi ya uvamizi.
Screenshot_20220227-135004_Instagram.jpg
 
Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia mkazi wa mtaa wa Buguku kata ya Buhonga jijini Mwanza, Diana Bundala (39) maarufu kama "Mfalme Zumaridi" kwa kosa la usafirishaji haramu wa binadamu 149.

Pia limamshikilia kwa tuhuma zakuwatumikisha watu hao ambao kati yao kuna watoto 24 wenye umri kati ya miaka 4 hadi 17.

Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Ramadhani Ng'anzi amesema mtuhumiwa alikuwa akiwasafirisha watu hao kutoka maeneo mbalimbali nchini huku akiwaaminisha kuwa yeye ni Mungu anayeponya, kufufua watu na kutatua matatizo yao.
Screenshot_20220227-135307_Instagram.jpg
 
• Wanajeshi wa Urusi sasa wako ndani ya Mji wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine, Kharkiv, ambapo wanapambana na Wanajeshi wa Ukraine mitaani, Wanajeshi hao wa Ukraine wanaonekana wakijibu mapigo kwa kushambuliana kwa silaha na Wanajeshi wa Urusi.
Screenshot_20220227-174641_Instagram.jpg
 
Shirikisho la Kimataifa la Judo limemsimamisha Vladimir Putin kuwa Rais wake wa heshima na Balozi wa Judo, Rais Putin ana mkanda mweusi wa judo ambapo uamuzi huo ni miongoni mwa vikwazo vya michezo vilivyotangazwa katika siku za hivi karibuni.

Mashindano ya Formula 1 Grand Prix ya Urusi yaliyotarajiwa kufanyika kwenye Mji wa Sochi mwezi Septemba yameahirishwa na pia fainali ya ligi ya Mabingwa ya 2022 itachezwa Paris badala ya St Petersburg.
Screenshot_20220227-174809_Instagram.jpg
 
BREAKING: Rais wa Russia Vladimir Putin ametoa amri kwa Jeshi la Nchi hiyo kuweka vikosi vya kuzuia nyuklia vya Urusi katika hali ya tahadhari baada ya kauli zilizotolewa na Viongozi wa Nchi za NATO.

Akizungumza kwenye Televisheni ya Taifa Rais Putin amesema "Kama unavyoona, sio tu kwamba Nchi za Magharibi huchukua hatua zisizo za kirafiki dhidi ya Nchi yetu katika nyanja ya kiuchumi, namaanisha vikwazo haramu ambavyo kila mtu anavijua vyema lakini pia Maafisa Wakuu wa Nchi zinazoongoza NATO wanajiruhusu kutoa matamshi ya kichokozi kuhusiana na Nchi yetu"

Taarifa zaidi kukujia.
Screenshot_20220227-174920_Instagram.jpg
 
Naibu waziri wa Ulinzi wa Ukraine ametoa makadirio ya hasara anayosema kuwa Majeshi ya Nchi hiyo yameisababishia Urusi hadi sasa ambapo amesema mpaka sasa wamewaua Warusi 4,300 na kuziteketeza Ndege za Urusi 27,

Ukraine pia imesema imeziteketeza Helikopta 26, Vifaru 146, Magari 706 ya kivita , Mizinga 49, Mfumo mmoja wa ulinzi wa anga, Mifumo 4 ya kurusha roketi , Magari 30, Meli 60 za mafuta, Drone 2 na Boti 2.
Screenshot_20220227-175035_Instagram.jpg
 
Wakati mzozo wa Ukraine na Urusi ukiendelea kushika kasi, Korea Kaskazini imerusha kombora linalodhaniwa kuwa la masafa marefu kuelekea Baharini katika muendelezo wa majaribio yake ya silaha.

Majaribio hayo ni ya nane kwa mwaka huu pekee huku baadhi ya Watalaamu wakisema kwamba Korea Kaskazini inajaribu kukamilisha teknolojia yake ya silaha na kuishinikiza Marekani kutoa makubaliano kama vile kuiondolea vikwazo.

Wakuu wa vikosi vyote vya majeshi nchini Korea Kusini, wamethibitisha juu ya Korea Kaskazini kurusha makombora lakini hawakutoa maelezo zaidi, bado Korea Kaskazini haijato kauli kuhusu mzozo wa Ukraine na Urusi.
Screenshot_20220227-175228_Instagram.jpg
 
Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson amesema Uingereza imetuma Wanajeshi wa Ulinzi ili kwenda kutoa msaada nchini Ukraine huku ikiahidi kuipa nguvu zote Jumuiya ya Kujihami (NATO) katika kuidhibiti Urusi kufanya mashambulizi Ukraine.
Screenshot_20220227-175419_Instagram.jpg
 
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi amejitolea kuisaidia Ukraine katika juhudi za kuleta amani, Modi ameyasema haya wakati wa mazungumzo kwa njia ya simu na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy.

Kwa mujibu wa taarifa ya Serikali, India iko tayari kuchangia kwa njia yoyote kuelekea juhudi za amani wakati Rais Zelenskiy alipomweleza kuhusu hali ya mgogoro nchini Ukraine.

Siku ya Ijumaa, India, China na Falme za Kiarabu walijizuia kupiga kura kwa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kukataa uvamizi wa Urusi, hatua iliyosababisha ukosoaji mkubwa kutoka nchi za Magharibi na kupokea sifa kutoka kwa Urusi ambayo wamekuwa kwa muda mrefu na mahusiano ya ulinzi.

India imetuma vikosi maalum nchini Poland, Hungary na Romania kwenda kuwahamisha Raia wake kupitia Nchi hiyo jirani na Ukraine.
Screenshot_20220227-175539_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom