Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20211208-101607.png
 
Pablo aende kwa kuiheshimu Yanga, pamoja na kwamba mechi za watani huwa haitabiliki lakini kuna nyakati lazima uheshimu form ya mpinzani wako kwa wakati huo.

Bahati nzuri kocha wa Simba ana machaguo mengi sana lakini lazima aende na tahadhari akijua Yanga ipo kwenye kiwango bora na ina wachezaji wazuri sana hasa katika eneo la kiungo na wanaweza kubadilika kulingana na mpinzani amekuja vipi.

- Edgar Kibwana.
Screenshot_20211211-090641_Instagram.jpg
 
Nadhani sehemu ambazo zitakuwa na mapambano ni sehemu za pembeni ya uwanja. Ndio sehemu ambayo hizi timu mbili zimekuwa na watu washindani zaidi.

Sioni utofauti wa madaraja [class] wa wachezaji wa Simba na Yanga isipokuwa ni viwango [form] ya wakati huu.

Yanga inafaida kwa kuwa wachezaji wake wapo kwenye form kwa wakati huu. Wachezaji wa Simba wanatafuta form yao ili kurudi walivyokuwa misimu mitatu iliyopita.

Pembeni Yanga inamtumia Djuma Shabani, Moloko, Shomari Kibwana au Fari sehemu ambazo kutakuwa na upinzani kutoka kwa Mohamed Hussein na Kapombe sehemu ambazo pia Simba inategemea hukohuko.

Ambaye atafanikiwa kwenye maeneo hayo ya pemebeni ndio naona italeta tofauti ya mchezo. Eneo la katikati Yanga wana faida ya kulimiliki lakini bado wanategemea kupeleka mipira pembeni.

- Amri Kiemba.
Screenshot_20211211-090808_Instagram.jpg
 
Kuelekea mchezo wa KariakooDerb kwangu Yanga ni favourites na sababu zipo mezani, ukizichambua unaona wazi kabisa Yanga ni favourites kwenye huu mchezo.

- Yanga inaongoza msimamo wa Ligi [pointi 19]

- Yanga imefunga magoli mengi zaidi kuliko Simba [Yanga imefunga magoli 12, Simba imefunga magoli nane].

- Kocha wa Simba Pablo Franco bado hajapata kikosi cha kwanza anachokiamini

Katika mechi kadhaa ambazo tayari Pablo ameiongoza Simba ametumia mifumo tofautitofauti na wachezaji tofauti, vs Ruvu 4-4-2, vs Geita Gold 4-3-3, vs Red Arrows 4-2-3-1.

Hata mashabiki wa Simba sasa hivi ukiwaambia wakutajie kikosi cha Simba cha Kocha Pablo Franco watatofautiana.

- Wilson Oruma, Mchambuzi wa Michezo.
Screenshot_20211211-091321_Instagram.jpg
 
KARIAKOO DERBY
.
SIMBA SC YANGA SC
17:00
Mkapa.
.
H2H:
Mechi 106. Simba imeshinda 31. Yanga imeshinda 38. Sare 37
.
Nani anapasuka leo __!
Screenshot_20211211-091731_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom