Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20211206-183059_Instagram%20Lite.jpg
 
Farhan Jr

Baada ya uwekezaji kufanyika kwenye Ligi Kuu soka Tanzania Bara ambapo NBC ndio main sponsors na baadae GSM kuweka pesa pia kama Co Sponsors

Klabu ya Simba ilipokea nembo kutoka Mamlaka za soka nchini kwamba kuelekea Derby wanapaswa kuvaa nembo nyingine ya Mdhamini mwenza kwenye Ligi

Simba waliandika barua Desemba 2, kueleka kwa Mamlaka husika kuhitaji ufafanuzi kuwa inawezekana vipi kisheria wakatekeleza hivyo na hawakupokea majibu zaidi ya kuambiwa wavae

Msimamo wa Simba mpaka sasa ni kuwa hawatotumia nembo hizo mpaka pale wakipata ufafanuzi wa kisheria na unaoleweka nje na hapo haiwezekani

Siku mbili kabla ya derby ya Kariakoo kutakuwa na kikao kati ya Simba, Yanga na TPLB kuelekea mchezo huo ila CEO wa Simba atafika na jopo la Wanasheria kuulizia Uhalali wa kutumia nembo nyingine tena kwenye jezi zao nje na ile ya NBC

CEO Barbra anafahamu vyema kuwa kupinga kuweka hiyo nembo nyingine ni faini ya million 3 kwa mechi moja mpaka tatu na kisha adhabu kubwa ni kushushwa daraja

Msimamo wa Simba ni kupata ufafanuzi wa kisheria na waambiwe wanatekeleza hivyo kwa kifungu kipi?? That's it for now

[Ufafanuzi wa Voicenote inayotembea kwenye WhatsApp ambayo wengi hawajaielewa taarifa kamili]

TUKUMBUKE| Takwa la GSM ilikuwa ni kukaa upande wa kushoto wa jezi za timu zote, ndivyo GSM walivyotaka na mkataba ulisainiwa kwa masherti hayo
Screenshot_20211207-191847_Instagram%20Lite.jpg
 
Farhan Jr

Just imagine mkataba ni siri kati ya TFF na GSM, just imagine klabu ambaye ambao ndio watekelezaji hawajui kama sisi tusivyofahamu

Just imagine Simba anadai ameona taarifa za udhamini huo mtandaoni kama ambavyo Wadau wengine walivyoona

Just imagine unaenda kutumikia mkataba ambao wewe hujui una masherti gani na unanufaikaje na mkataba huo, just imagine

Ngoja niwaambie TFF ni regulator ambaye anahakikisha mchezo wa mpira upo fair na unachezwa kwa haki ila jukumu la mikataba ni la bodi ya Ligi (TPLB)

TFF anasema klabu zikipata mikataba yoyote ya kibiashara wanapaswa kuipeleka TFF kuipitisha Ili kuhakikisha kama hakuna mgongano wa kimaslahi, kwanini wao hawatoi hiyo nafasi kwa klabu?

Naomba tuulizane je TFF wakishapata wadhamini kwanini wasikae chini na klabu kutazama kama hakuna migongano ya kimaslahi? Kwanini kuwe na double standards? Ipi nafasi ya Klabu?

Let me tell you! TPLB ndie ana dhamana ya Klabu zote, TFF ana dhamana ya mpira na timu za taifa, tuwe na mipaka itatusaidia sana, kwenye Ligi yeye ni regulator tu na kuoversee conducts

Screenshot_20211207-192248_Instagram.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom