Makapuku Forum

Makapuku Forum

Darassa kutumbuiza Simba DAY 2021
.
SA tunaweza kukuthibitishia kuwa Mwimbaji mkali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ramadhani Shariff ‘Darassa’ atakuwa mmoja wa wasanii watakaotumbuiza katika tamasha la Simba Day litakalofanyika Septemba 19 katika Uwanja wa Mkapa.
Screenshot_20210916-050115_Instagram.jpg
 
Pichani ni Ofisa vipimo wa Uviko-19 aliyepangwa na CAF kusimamia mchezo wa marudiano kati ya Rivers Utd vs Yanga utakaopigwa Nigeria akiwa na Afisa habari wa Rivers Utd, Charles Mayuku.
Screenshot_20210916-050223_Instagram.jpg
 
Solskjaer amepoteza mechi SABA (7) kati ya 11 kwenye Ligi ya Mabingwa akiwa kocha wa Man Utd. Van Gaal na Mourinho kwa pamoja walipoteza mechi sita kati ya 20 wakiwa makocha wa United.
.
Ole OUT au Tumpe muda apate muunganiko __!!

Mimi kama shabiki wa man u nasema atokeeeee
Screenshot_20210916-050702_Instagram.jpg
 
Farhan Jr

MZEE HASSAN DALALI 'FIELD MARSHAL' NURU KWENYE GIZA LA SIMBA

Mchana wa leo tulifika pembezoni kidogo mwa Jiji la Dar Es Salaam, mpaka Mbagala huko Majimatitu kuonana na Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba, HASSAN DALALI

Baada ya interview nzuri sana na CLOUDS FM, tukapata wasaa wa kupiga stori na Mzee huyu mwenye historia kubwa ya klabu ya Simba, nami nitakuwa nawamega kidogo kidogo

Mzee Hassan Dalali mwenyewe anapenda kujiita 'Darasa la saba' katika maswali yangu nikataka kujua kitu kuhusu yale alowahi kuyafanya kwenye kipindi cha Uongozi wake kama Mwenyekiti Simba

Anaanza kunipa stori kwanza kuhusu ule uwanja wa Bunju! Anasema jumla ya hekari za uwanja ule ni 25 ambapo aliununua enzi za uongozi wake 2007, ikiwa ni kiasi cha takribani million 106

Kutokana na ukata mkubwa enzi zile akalazimika kutoa kwanza kiasi cha Tshs 4,000 (Elfu nne) kama kishika uchumba wa kile kiwanja anasema ndoto yake kubwa ilikuwa ni kuona Simba inamiliki uwanja wake

Nikamuuliza hivi karibuni umewahi kufika Bunju? Akacheka na kusema amefika mara nyingi na mpaka halisi wa uwanja ule anaufahamu huku akisema kwa macho tu anajua kuna baadhi ya nyumba zipo ndani ya kiwanja cha Simba (zimejengwa kimakosa)

Hii kitu hata serikali walipokuja kupima wameamuru baadhi ya nyumba zipo ndani ya himaya ya Simba hivyo, zinapaswa kubomolewa! Kifupi Mzee Dalali anaujua ule uwanja, anakwambia hata akisimama tu anajua kila mpaka

Wakati tukiendelea na mazungumzo yetu ya kawaida nje ya MIC, nikamuuliza ana kumbukumbu gani juu ya uwanja ule? Basi hapa ananipa mkasa mkubwa sana

Anasema siku ya kwanza baada ya klabu kuununua uwanja huo akalazimika kwenda kukagua mipaka ya uwanja akiwa kama Mwenyekiti! Mzee Dalali anasema wakati anakatiza kwenye pori (kumbuka Bunju ilikuwa pori haswa) kwa mshangao mkubwa...

ITAENDELEA......Simulizi za Mzee Dalali, mtazipata na yale msoyajua hapa
Screenshot_20210916-050908_Instagram.jpg
 
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefanikiwa kupata mkopo nafuu kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa( IMF) wenye thamani ya shilingi trilion 1.3 kwa ajili ya kukabiliana na athari za Covid- 19 katika Sekta ya Uchumi na Kijamii.

Akizungumza Dodoma leo, Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Mwigulu Nchemba amesema kuwa fedha hizo zitatumika katika Sekta ziliozoathiriwa na Covid-19 ikiwemo Sekta ya Utalii, Elimu, Afya, Maji pamoja na kusaidia kaya maskini kupitia TASAF.View attachment 1939663
Sasa Chanjo unaenda kua lazima...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom