Makapuku Forum

huyu kijana mikono yake na kichwa chake ni hatar
 
| ABDI BANDA
MTIBWA SUGAR

.
Done Deal. Beki Abdi Banda aliyekuwa anacheza soka la kulipwa nchini Afrika kusini amejiunga rasmi na klabu ya Mtibwa Sugar inayoshiriki Ligi Kuu nchini.

Huyu bwana asingetusemea hovyo simba tungemfikiria tungemuweka hata benchi
akiba ya maneno ni nzuri

Ooh sizitaki mbichi hizi haya kiko wapi mjifunze kwa banda jamani
 
| Wachezaji NANE raia wa Brazil wanaocheza katika Ligi Kuu England wamesimamishwa wikendi hii kuvitumikia vilabu vyao baada ya Shirikisho la soka la Brazil
kuweka pingamizi Fifa kuwazuia wasicheze.
.
  • T Silva
  • Fred
  • Firmino, Allison, Fabinho
  • Ederson, Jesus
  • Raphinha
.
(Richarlison anaweza kucheza)
 
Jeshi la Polisi Mkoani Manyara, linamshikilia Samwel Alfred (48), mkazi wa Kijiji cha Magara wilayani hapa kwa tuhuma za kumuua Michael Jackson (25) baada ya kumfumania akizini na mke wake, Habiba Saidi (22).

Mtuhumiwa huyo, inaelezwa kuwa alitekeleza mauaji hayo kwa kumkata kwa panga marehemu aliyemkuta akivunja amri ya sita na mkewe.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi (ACP), Merrison Mwakyoma amesema tukio hilo limetokea saa 10 alfajiri ya leo, Septemba 8.

Kamanda huyo amesema Alfred alimuaga mkewe Habiba saa 10 alfajiri kuwa anakwenda kukata kuni na kumuacha akiwa amelala lakini mkewe huyo akampigia simu hawara yake Michael Jackson aende nyumbani kwake wakafanye mapenzi.

“Baada ya Jackson kufika walizunguka kwenye banda la ng’ombe na kutandika mgorore chini na kuanza kufanya mapenzi ila ghafla mumewe akarudi na kuwafumania,” amesema Kamanda Mwakyoma.

Kwa sababu Alfred alikuwa na panga mkononi, kamanda alisema alilitumia kumkata sehemu mbalimbali za mwili mpaka akafariki dunia. Mkewe ambaye alikuwa anamzuia asiendelee kumjeruhi marehemu naye alikatwa mkono uliodondoka chini.
 
Mahakama Kuu imetupilia mbali pingamizi la awali Serikali dhidi ya maombi ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) ya kibali cha kufungua shauri la kupinga tozo kwenye miamala ya simu.

Hata hivyo wakati mahakama hiyo ikitupa pingamizi la Serikali, pia imeyatupa maombi kama hayo yaliyofunguliwa na Mwanaharakati Odero Charles Odero baada ya kukubaliana na hoja moja ya pingamizi la Serikali kuwa hati ya kiapo chake kilichokuwa kinaunga mkono maombi hayo ina kasoro za kisheria.

Uamuzi huo wa umetolewa leo Jumatano, Septemba 8,2021 na Jaji John Mgetta.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…